Serikali yaweka Shilingi bilioni 12 kwa utekelezaji wa miradi ya maji Mtwara

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Serikali kupitia Wizara ya maji imetenga jumla ya Sh 12,523,727,274.27 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ambazo ni kwa ajili ya kujenga, kukarabati na kufanya, upanuzi wa miradi mbalimbali ya maji katika Mkoa wa Mtwara.

Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) Mkoa wa Mtwara, Primy Damas alisema hayo jana Machi 27, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji katika mkoa huo.

Alitaja mgawanyo wa fedha hizo kwa kila wilaya kuwa Masasi Sh 2,484,329,885 Mtwara imepokea Sh 3,367,250,973.27, Nanyumbu Sh 2,132,694,811, Wilaya ya Newala Sh 2,079,857,372 na Tandahimba imepokea Sh 2,459,594,233.

Damas alieleza kuwa kwa sasa katika mkoa huo wananchi wanaopata huduma ya maji kwa wakazi wa vijijini ni 672,672 sawa na asilimia 60.16 na mijini watu 282,945 sawa na asilimia 82.

Alisema vyanzo vyote vilivyoendelezwa kwa pamoja vina uwezo wa kuzalisha lita 21,186,300 kwa siku ukilinganisha na mahitaji ya maji ambayo ni lita 46,088,340 ambapo uzalishaji huo ni sawa na asilimia 46 ya mahitaji.

Alisema uwezo wa vyanzo vya maji vilivyopo ni kuzalisha maji mita za ujazo milioni 14.947 kwa mwaka na maji yanayotumika ni mita za ujazo milioni 2.661 kwa mwaka sawa na asilimia 17.80.

Meneja huyo alisema ongezeko la utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi waishio vijijini imekuwa inaongezeka kwa kasi kidogo ikilinganisha na kasi ya ongezeko la watu na hali hiyo inatokana na uwekezaji mdogo uliokuwa unafanywa na serikali katika sekta ya maji.

Anabainisha kuwa mkoa ulikuwa na lengo la kufikisha asilimia 64 ya utoaji wa huduma ya maji kwa wakazi waishio vijijini, hata hivyo katika kipindi husika hali imeongezeka kutoka wastani wa asilimia 59.53 (Mwezi Juni 2020) hadi kufikia asilimia 60.16.

Kwa mujibu wa Damas, hatua hiyo inatokana na nguvu kubwa ya uwekezaji wa miundombinu ya maji unaofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluh Hassan kutekeleza mipango mbalimbali katika mkoa huo.

Alisema kutokana na uwekezaji unaofanywa katika sekta ya maji mkoani Mtwara, ni matumaini ya Ruwasa kwamba huduma ya maji itazidi kuongezeka hadi kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali pamoja na llani ya Uchaguzı ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa miradi mingi imeanza kutekelezwa.

Damas alisema katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi unaendelea kuboreshwa, Ruwasa inaendelea kuwezesha, kusimamia ujenzi na kukamilisha miradi ya vijjini katika maeneo mbalimbali ya wilaya husika kupitia fedha za Mfuko wa Taifa wa Maji (NWIF) na mipango ya lipa kwa matokeo (P4R} na lipa kabla ya matokeo (PbR).

Source: Majira
 
Back
Top Bottom