Serikali 'yawavutia pumzi' wageni kuajiriwa kiholela!

Mkuu mie nimeenda spain na italy na wanasafe ya kuweka vitu vya thamani na wanakuuliza hivyo hivyo kwamba if you have any jewellery please let us know we have a safe for our clients. Je nikuulize kule nako ni wezi? Nadhani suala la wadokozi ni la dunia nzima but kisiwe kigezo cha kuwanyima wazawa kazi ama sivyo haina maana basi ya kuitwa mzawa.
Udokozi unaweza kuwepo sehemu yoyote, ila bongo wanaona udokozi ni halali kwao, mpaka kufikia hatua ya kuupa majina mazuri ili kuuharishisha!

Kuna siku moja nilipata wageni kumi na moja, hawakupenda kukaa hoteli(kwa ajili ya usalama), hivyo waliniomba niwatafutie nyumba kubwa ambayo kwao. Nilipata nyumba ya ghorofa mbili katika eneo la Mji Mkongwe(ZNZ). Wageni wakaja na kuhifurahia nyumba hiyo. Asubuhi yake waligundua kuwa wameibiwa.

Ilikuwa ni kazi kweli kweli kwani wengine waliibiwa plastic zao za fedha na wengine hadi pasi za kusafiria. Huku na kule baada ya polisi waliweza kupata baadhi ya vitu na ni baada ya wageni hao kuondoka. Mbaya zaidi mchongo mzima ulifanywa na mwenye nyumba!
 
suala la wageni kuajiriwa ni dogo mno ukilinganisha na masuala ya ukosefu wa umeme, ufisadi na rushwa kubwakubwa ambazo serikali imeshindwa kuzitatua
 
suala la wageni kuajiriwa ni dogo mno ukilinganisha na masuala ya ukosefu wa umeme, ufisadi na rushwa kubwakubwa ambazo serikali imeshindwa kuzitatua

Wewe unadhani swala la ajira kiholela ni la kubeza? Nikuulize unadhani kwanini uhalifu unaongezeka dar? Nikuulize kwanini watoto wa mitaani wako wengi miji mikubwa? Nikuulize, kwanini ufisadi unakua kila siku kuanzia ngazi ya chini mpaka juu? Ukishajua haya ndio utajua kwanini hizi ajira za foreign nationals ni balaa kwetu. Ama sivyo basi wewe kama alivyosema Kibunango you have a problem katika uelewa wako.
 
Mi nilikuwa nafanya kazi kwa wahindi kila kitu anakuuliza umsaidie ili ajue lakini mshahara anachukua mara mbili yako.
 
Mi nilikuwa nafanya kazi kwa wahindi kila kitu anakuuliza umsaidie ili ajue lakini mshahara anachukua mara mbili yako.

Hilo mbona linajulikana na ni kwasababu wanakuwa hawajui kitu wakija wanajifunza kutoka kwako ili wapate kuwafurahisha waliowaleta and then wanakuja kukuondoa kwa fitina kwani bosi anaweza akageuza jicho kwako akikupenda kutokana na utendaji wako. Linalokera ni hili mnafanya kazi sawa mwenzio anachukua mshahara mara mbili yako na analipwa in foreign currency wewe Tanzania shillings. Ndio maana jamaa yangu yalimshinda akaishia zake.
 
hakuna lolote hapo..

wahindi wanachangia sana CCM na si wahenga walisema mkono mtupu....

haya ndiyo malipo ya mkono uliojaa.

waanze na Manji...Mo Enterprises...Jeetu Patel pale Azania na wengine kibaoooooooooooo
 
Kutokana na wageni amabo wapo tayari kufanya kazi kwa masaa mengi na katika mazingira magumu...wafanya biashara wageni wamependelea sana kuajiri wageni. Ukiangalia hoterini...wadada wa hausi kipin ni wakenya..nenda kunduchi, na hoteri za unguga.

Angaria maduka ya waparestina..wauzaji ni wakenya, nenda ata pare spanisi tails...wauzaji ni wakenya. Je ni kweli watanganyika atuwezi kutandika vitanda? kuuza tails?
 
Back
Top Bottom