Serikali 'yawavutia pumzi' wageni kuajiriwa kiholela! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali 'yawavutia pumzi' wageni kuajiriwa kiholela!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Dec 30, 2010.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  NAIBU Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro Mahanga, mapungufu yaliyoko katika sheria za kazi hapa nchini, yanasababisha baadhi ya kampuni binafsi, kuajiri watu wageni hata kwa kazi zinazostahili kufanywa na Watanzania.

  Dk Mahanga aliyasema hayo juzi kufuatia hoja iliyowasilishwa na Ofisa Kazi wa Mkoa wa Mara,Venance Kadago, ambaye alisema idara yake imekuwa ikifanya ukaguzi katika kampuni binafsi na kukuta wafanyakazi wa kigeni walioajiriwa kwa mikataba ya muda mfupi bila kuwa na vibali kutoka Wizara ya Kazi.

  Ofisa huyo alisema vibali wanavyopewa wageni ili kuwaruhusu kuishi nchini, vinatoa mwanya kwa watu hao, kufanya kazi ambazo vinginevyo, zinaweza kufanywa na Watanzania.

  "Mapungufu yaliyoko katika sheria ya sasa ndiyo yanayosababisha matatizo haya yote. Maofisa uhamiaji huko mikoani, wamekuwa wakitoa vibali vya kuwaruhusu wageni kuishi nchin," alisema Dk Mahanga.
  Alisema kwa kutambua tatizo hilo, wizara yake inaandaa marekebisho ya sheria za kazi, itakayoainisha vizuri majukumu ya wizara katika kutoa vibali vya kazi na majukumu ya maofisa uhamiaji katika kutoa vibali vya wageni kuishi nchini.

  Alisema hatua hiyo itasaidia kuondoa mwingiliano na mgongano wa majukumu ya wizara na uhamiaji.

  Dk Mahanga alikuwa akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo wa Mkoa wa Mara ambapo alisema pamoja na utandawazi na nchi kuingia kwenye ushirikiano wa kikanda wa kiuchumi, biashara na ajira, si vyema kuruhusu kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania, kufanywa na wageni.

  Alitumia mwanya huo kutoa rai kwa Wizara ya Mambo ya Ndani, kupitia Idara ya Uhamiaji, kushirikisha na wizara yake, kushughulikia matatizo yanayohusu ajira kwa wageni hata kama sheria bado zina mapungufu.

  Source: Mwananchi.

  Mtazamo: Hili jambo serikali yetu isiendeleze siasa kwa wingi na kusababisha jamii yetu iangamie. Latest statistics zinasema kila mwaka it is estimated around 700,000 graduates wanamaliza vyuoni na just 5.7% ndio wanaajiriwa katika kazi za maana (World Bank Figures). ILO wanasema kuwa 40% of youth population katika maeneo ya mijini kama Dar hawana kazi.

  Wenzetu in developed economies wanakuwa na mikakati inaoleweka kuhusu hili swala hasa likija katika maendeleo ya nchi. Wazawa wanapokuwa na kazi unaongeza kiwango cha watu wenye kuwa na uwezo wa kumudu gharama za maisha na hilo linaongeza pia kiwango cha watu wenye kufanya matumizi na pia kuchangia katika kukua kwa sekta za viwanda na kilimo. Kutokana na hilo basi ajira ni sekta muhimu sana nchini kuweza kutoa nafasi ya maendeleo ya kweli kwa watanzania.

  Tukiangalia dunia ya leo ajira za nchi zilizoendelea huwa zinaenda kwa mpangilio unaoeleweka. Kuna ajira wanaweza kupewa wazawa kwani supply yake iko kubwa sana. Mfano sekta ya kilimo (casual labourers) Serikali ingelitoa kipaumbele zaidi kwa wazawa kupewa hizo kazi ili kupunguza hili tatizo la watu kukosa kazi.

  Vile vile kazi za maofisini kuna sekta kama biashara, Information technology particularly katika user-end services, Engineering, wazawa wangelipewa mkazo na makampuni binafsi yangeliambiwa kuwa watoekipaumbele kutoa ajira kwa watoto wetu wanaomaliza vyuoni kupata kazi katika maeneo hayo. Kukitokea makampuni binafsi yanadai hawajapata mtu wangelitakiwa wamfanyie recruitment mzawa wakati wamemuajiri mgeni ili akimaliza katika kipindi maalum aje kurithi nafasi ya yule expatriate.

  Kuna sekta zina mapungufu ya wafanyakazi kwasababu soko la wafanyakazi halikidhi mahitaji. Mfano waalimu hasa waalimu wa masomo ya hisabati na kiingereza hapo wangeliruhusu kuleta foreign nationals waje kufundisha (kwa limited period mfano 5 years basi). Hilo lingelisaidia kutoa nafasi ya wazawa yaani waalimu wetu kuwa wamesomea wakafuzu kuja kufidia hii kiu ya mahitaji ya watu katika sekta hiyo. Pia sekta nyengine kama kilimo pia wangelifanya hivyo hivyo.

  Wawekezaji nadhani ni wakati muafaka serikali yetu ikafafanua nani anaweza kujulikana kama muekezaji tanzania. Wawekezaji njaa kama wachina wanaofanya biashara za umachinga kariakoo ni wakati muafaka wangelidhibitiwa kutoa nafasi kwa vijana wetu waweze kujiajiri. Pia small scale business should be protected ili wapate vijana wetu waweze kujiajiri na kutoa nafasi ya kukua kwa mzunguko wa pesa. Binafsi wawekezaji Tanzania wangelitakiwa wawe na si chini ya milioni 100 na wawe wanaajiri wazawa katika shughuli zao. Hili lingelisaidia kuondoa tatizo.

  Naibu waziri angelitakiwa kufahamu kuwa ijapokuwa analivutia pumzi swala hili pia afahamu kuwa vijana wengi hawana kazi. Director wa Youth Development kutoka wizara kazi alisema 60% ya vijana wengi hawana kazi Tanzania. Hili sio jambo zuri kwani hawa vijana ndio nguvu kazi ya taifa inayopotea na kodi inayoyoma. Ni vema serikali ikajaribu kuwatafutia namna waweze kupunguza hili tatizo at the same time walinde zile kazi chache zilizopo nchini.

  Failure do this inapelekea kuongezeka kwa vijana mitaani wasio na shughuli maalum, kukua kwa uhalifu nchini kwasababu hawana njia za kujipatia kipato, Kuongezeka kwa maradhi kama vile ukimwi kutokana na wengine kujitafutia riziki kwa njia zisizo rasmi (ukahaba), Kukua kwa watoto wengi mitaani kutokana na wazazi kushindwa kumudu gharama za maisha, na mwisho wa siku jamii yetu kupotea kwasababu nguvu kazi haijatumika kabisa. Ni mtazamo tu. Nilikuwapo!!!!
   
 2. D

  Derimto JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hili linakera sana hasa pale ambapo inafikia hata wanaanza madharau kwa wenyeji wao
   
 3. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mie nilienda ofisi mmoja nikakuta wakenya watupu mtanzania mpokea simu front desk nikajiuliza hawa watanzania wameshindwa vipi kukosa kazi hapa. Well nikaja kuconclude sijui sheria za kazi hazipo au hazisimamiwi but sidhani kama mimi na wewe tukienda Kenya tunaweza kukuta ofisi nzima imejaa watanzania litakuwa jambo la ajabu sana. Serikali needs to protect hizi kazi kwa faida ya vizazi vyetu otherwise tusilalamike uhalifu na ukahaba ukizidi mijini.
   
 4. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Hapo Mahanga anacheza makida makida kabisaa, kwanini nasema hilo nakumbuka JK wakati anafungua Snowcrest Hotel Kule Arusha akawasaga sana watanzania kuwa hatufai still twahitaji watu wa kutuongoza kwa ajira hizi, Jamani hata Front Office Manager au Executive Housekeeping nao atokeee India Duuuuh,

  Kwanza uhalalai wa ajira za wageni nyingi ni za kuchakachua ukitizama wengi walikuja TZ kwa njia za kutembea na kumbe baada ya miezi 2 au 3 wanapewa work permit sasa sielewi hao uhamiaji huwa wanafanya kazi gani na kwanini huwa hawakagui watu International Airport?? nenda India kama utapata kazi kirahisi muone hakuna wao wenyewe tu wanatuambia kupata kazi india kwa mwafrika ni shughuri pefu. sasa leo huku kwetu mmh

  Alafu mkataba wa ajira za wageni huwa ni mwisho miaka mingapi maana kuna wengine wako zaidi ya miaka 6 ndani ya nchi cheo kile kile sasa huyu Mtanzania ambae anamaliza Chuo hajui kuifanya hiyo kazi au hawa wageni wanapo fanya hizi kazi huwa hwatoi proper training kwa wa TZ ili wakimaliza mudawao wa kibari cha kufanya kazi wawaachie waTZ waendeleee?? Tatizo kubwa ni kwa wamiliki wakubwa wa makampuni haya kwani huwahonga sana watu wa UHAMIAJI na hili liko wazi kabisaa
   
 5. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kigezo cha kikubwa wanachodai viongozi wetu ni kwamba:-
  a. Watanzania wavivu
  b. Watanzania wamesoma lakini hawajaelemika yaani sio wabunifu.
  c. Elimu yao si ya kimataifa yaani hawana exposure.

  Sasa cha kushangaza angalia wanaowaajiri ndio mie huwa nashindwa kuelewa wanamaanisha nini.
  Wakenya:-
  a. Wengi wao wanatuhumiwa kuwa ni wasanii maneno mengi lakini they lack creativity.
  b. Wengi wamesoma lakini elimu yao ni below standard ukicompare na graduate wa UDSM au vyuo vengine vya tanzania (ukiachilia University of Nairobi).
  c. Wengi wako willing kufanya kazi hata katika mazingira magumu yaani wako tayari kwa lolote (Hili linaeleweka kama unataka mtu wa kufanya kazi kwa bei chee).


  Wahindi na wapakistani:-
  a. Wengi hawajasoma unakuta ni kiingereza tu kwa wingi. (Kuna muhindi nilikutana nae Oxford alinambia muhindi aliyesoma kwao lulu na wengi wakikosa kazi wanaenda ulaya na canada kutafuta masilahi na wanalipwa vizuri sana sasa kwa mtazamo wangu inaelekea wanaokuja kwetu wengi ni makapi, Pia kuna jamaa yangu alishafanya kazi na wahindi fulani hawana hata degree ndio unaambiwa madirector sasa nikacheka sana jamaa yalipomshinda akajiondokea zake).
  b. Wengi wa wahindi wanajua kutunza siri (Yuko tayari afe na siri yake) .
  c. Wahindi wanauadilifu wa kutumia pesa vizuri wakikopa.
  d. Wasanii hasa katika masuala yanayohusu mahusiano yao na serikali.

  Wachina:-
  a. Wengi wanaokuja hawajasoma.
  b. Wanafanya kazi muda mrefu (hata masaa 24 wakiweza watafanya).
  c. Hawapendi kujihusisha mambo ya siasa za ndani wao wako after their priorities.
  d. Wengi wasanii yaani waongo waongo.

  Wazimbabwe:-
  a. Hawa jamaa wamesoma wengi wao hivyo wanakuja kutafuta maslahi.
  b. Wanapenda kupokea mawazo.

  Wanigeria:-
  a. Wasanii.
  b. Wamesoma vizuri sana ila matapeli.


  Makaburu:-  Sasa hivi vitu ukiangalia ni vitu vinavyotokana na mazingira kwanza ni kwamba makampuni binafsi mengi Tanzania yanamilikiwa na watu hawa wa kiasi kikubwa hivyo basi ni vema hivi vitu vikadhibitiwa kuokoa ajira za vijana wetu.
  a. Kama wanatafuta vijana kwa mshahara wa chini basi ni vyema Serikali ikasema kuwa nchini kiwango cha chini cha mshahara kiwe hivi na serikali iweke sheria ya kufatilia hili jambo kwa waajiri wa binafsi.

  b. Ajira za vibarua zidhibitiwe maana makampuni mengi ya kiasia hutumia loophole hii kutoa ajira za temporary ili kwanza wawalipe wafanyakazi mshahara mdogo au kukwepa kodi.

  c. Ajira za vibarua zipelekwe kwa recruitment agencies ambao watakuwa rahisi kuwamonitor na pia kuongeza pato la kodi la nchi (maana kule watawakata kodi vibarua).
   
 6. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mdondoaji,
  Umechambua vizuri sana hapa chini, binafsi nimewahi kufanya kazi na wahindi tena kwa muda mrefu na ni sahihi kwa ulichokieleza.

   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  d. Kuna kiongozi mmoja alikwenda mbali zaidi katika ajila za mahotelini kwa kudai "Watanzania ni wezi"
   
 8. c

  chamajani JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yes, S/he was right-JK, EL, RA, N.Mkono, Ngeleja, Chenge, Werema + + +huoni kuwa wezi tu!!!?
   
 9. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Umechambua vizuri ila TATIZO lako ni UDSM syndrome. Unadhani chuo kikuu bora ni UDSM tuu Tanzania? Are u insane? Kuna vyuo kama SUA, Muhimbili etc nadhani wana mazingira mazuri kutoa highly qualified graduates kuliko udsm kwa sasa even before. Usitegemee mwanafunzi anayehudhuria lecuture yuko nje amesimama hana hata exposure nzuri ya field work (hand on activity), hajui pa kulala (refer mabango yao kwa Waziri mkuu), kudesa mitihani kuwa a good substance.
   
 10. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Tehe tehe kazi ipo tunaiba sana sie kushinda wasomali na wakenya kule arusha au kesi zao hazijakuwa report in public??? Nenda nairobi simu mfukoni wanakuibia utafikiri wanavyombo vya kuscan nilikwenda karibuni mwenyeji wangu akanitonya na kuniambia kama sina shughuli maalum na simu niiache nyumbani nikasema duh!!!
   
 11. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #11
  Dec 30, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu samahani sana kama imekukera but nadhani hujanipata vizuri nanukuu sentensi niliyosema:-

  Wengi wamesoma lakini elimu yao ni below standard ukicompare na graduate wa UDSM au vyuo vengine vya tanzania (ukiachilia University of Nairobi).


  Sasa ukiangalia nimeitaja UD kwa mapenzi yangu lakini vile vile kuna vyuo vyengine Tanzania elimu wanayotoa ni bora kuliko ya Kenya. Pia sio univerisities tu bali hata Institutions like IFM, IA (Institute of Accountancy) na venginevyo ni bora zaidi kuliko kuliko hivyo vya huko kenya.

  Hivi unajua UDSM is the highest ranked university in East Africa? Sawa kama una ugomvi na UDSM but mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Turudi katika mada swali ni je kweli watanzania wana elimu ya chini kuliko hawa wageni wetu? Wanasema hatuna uwezo wa kudeliver but hao wenye uwezo wa kudeliver vp? Unakuta it all goes down to nani anamuamini (trust).

  Makampuni mengi binafsi na hata projects za serikali tumekuwa na imani ya kuwaamini wazungu na wageni kuliko wazawa kwa kigezo kuwa wanauwezo wa kufanya kazi wanayopewa. Sasa mie siamini hili kwani kuna graduates wa kitanzania wamekuwa wanadeliver mfano, Nehemiah Mchechu, Lawrence Mafuru, na Dr Kimei ni watu wamesoma these so called sub-standard universities je inakuwaje?
   
 12. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #12
  Dec 30, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Ni kweli kuna wengi(si wote) ambao si waaminifu, mifano mingi sana. MImi nimeona wengi tu wezi. Lakini hii haina maana kuwa kazi zetu wapewe wengine, wadhibiti wizi na kazi ziendelee.

  Anachosema Mahanga ni kuongea tu, lakini nina ukakika wa asilimia 150 hakuna kitakachofanyika, hii si mara ya kwanza na si mara ya pili kusikia maneno kama hayo. Miaka miwili ijayo utasikia issue hii hii kwenye JF.

  Ni sawa na katiba, tuliiongelea tukaiundia tume ikakusanya maoni na kutoa mapendekezo, sasa tunaanza kuongea upya, tutaunda tume tena, itakusanya maoni na kutoa mapendekezo halafu hayatatekelezwa, same vicious circle. Hii ni Tanzania.
   
 13. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #13
  Dec 30, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Tatizo la viongozi wetu wengi wana degree za pass na PhD za kununua. Sasa wakikutana na wenzao wa kenya na Uganda wanawazidi kwenye critical thinking, creactivity and argument sasa wanafikiri wanaturepresent waTZ wote na wote tuko kama wao.

  Tatizo letu wasomi wazuri na viongozi wazuri hawapewi nafasi TZ ila vilaza na wababaishaji ndiyo wanatutawala. Experience yangu toka Primary school mpaka University jamaa ambao walikuwa briliant na wenye leadership qualities hawakuweza kuingia kwenye siasa. Ila wale wapiga poroja design za kina Makamba ndiyo wanafanikiwa kwenye siasa za nchi yetu.
   
 14. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #14
  Dec 30, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hili ndio tatizo la nchi yetu kila mahali ni siasa halafu wakizidiwa huja kusema watanzania kazi yetu kulalamika. Hili suala ukiangalia ndio kiini cha kukua kwa uhalifu katika miji mfano ya Dar na Arusha. Sasa hivi watu wanaibiwa asubuhi saa mbili mwishoe tutakuja kukuta hata kwenda kazini mtu unaogopa. Something needs to be done.
   
 15. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #15
  Dec 30, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145

  Wana JF,

  Mwataka kuniambia katika huko kunyamburishwa hao raia wa nchi hizo sio weziiiii? Duniani kuna wezi na kila nchi inawezi tuuuu, Hakuna wezi kama hao waajiriwa wageni esp wahindi wakija huku after 2yrs amenunua nyumba India na wakikuonyesha ni kweli sasa sijui ni mishahara wenzetu hao wa india wanayopewa ndio mizuri sn au Government yao huko inaendesha uchumi vizuri kwa hiyo hukuti vitu expensive kama kwetu au ndio nini?
   
 16. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #16
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Niliwahi kuchukua chumba katika hoteli moja jijini Mwanza, Kaunta akaniambia kama nina vitu vya thamani nikabidhi hapo kaunta ikiwa ni pamoja na fedha...

  Hii ilikuwa na maana gani? Kuna wezi wa kuvamia hoteli hiyo? Ama wasafishaji wa hoteli hiyo ni wezi?
   
 17. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #17
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kuna wezi na mafisadi... Naona bandiko lako limehusu mafisadi.

  Hapa issue ni kwenye ajira! Je ni sahihi kuwanyima wazalendo kazi kwa sababu wana tabia ya udokoaji?
   
 18. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #18
  Dec 30, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Jethro hilo unalolisema ni kweli kabisa wanaofanya kazi kwa wahindi wanakuambia expatriate wa kihindi anakuja hata chips hajawahi kula kama sio kuziona. After six months analeta familia yake. After a year ametuma pesa za kufungua account India. in two years kanunua nyumba tuambiane basi mshahara wake kiasi gani? Unakuta hapa mwajiri wake (ambaye ni muhindi pia) anachokifanya ni kumlipa salary kubwa huyu jamaa especially in foreign currency, ikisha anafidia ile gap kwa kuwaajiri wafanyakazi wazawa kama vibarua kwa kuwalipa kwa siku na mshahara kiduchu. Au akiwapa ajira utasikia anawalipa laki kwa mwezi.

  Sasa kama mzawa analipwa laki moja kwa mwezi bila ya any other terminal benefits na mzungu au muhindi analipwa kwa dola unadhani kuna fairness??? Mbaya zaidi muhindi hajui au pengine hajasoma kabisa anafanya kazi tu ya kuhakikisha siri za mwajiri wake hazivuji kwa wazawa basi hiyo ndio kazi yake kubwa. Nafikiri serikali inahitaji kuwa na database ya kujua mishahara ya hawa so called expatriates na hizi kazi wapige marufuku kabisa kupewa mgeni yeyote ndio itakuwa wamesaidia sana.
   
 19. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #19
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Na bado!!! Na hii Jumuia ya Afrika Mashariki ndo itatumaliza kabisaaaaa!!!!!!
   
 20. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #20
  Dec 30, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu mie nimeenda spain na italy na wanasafe ya kuweka vitu vya thamani na wanakuuliza hivyo hivyo kwamba if you have any jewellery please let us know we have a safe for our clients. Je nikuulize kule nako ni wezi? Nadhani suala la wadokozi ni la dunia nzima but kisiwe kigezo cha kuwanyima wazawa kazi ama sivyo haina maana basi ya kuitwa mzawa.
   
Loading...