Serikali yawataka watalii waliopanga kuja nchini kuahirisha safari hadi hapo Corona itakapodhibitiwa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,889
141,824
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Kanyasu amewataka watalii waliopanga kutembelea Tanzania kuahirisha safari zao hadi pale ugonjwa wa Corona utakapokuwa umedhibitiwa.

Mh Kanyasu amewataka watalii hao kutofuta safari zao bali waahirishe kupisha hili janga linaloisumbua Dunia kwa sasa.

Source: ITV habari!

======

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amesema mlipuko wa virusi vya #Covid_19 ni tishio kwa sekta ya Utalii nchini
-
Amewataka Watalii wa Mataifa mbalimbali waliokuwa wamepanga kuja nchini kutositisha safari za kuja nchini bali wasogeze mbele
-
Tanzania hadi sasa imeripoti Wagonjwa 6 waliopata maambukizi ya virusi hivyo ambapo mgonjwa mmoja yupo Arusha, wawili wapo Jijini Dar na mmoja yupo visiwani Zanzibar

utalii.jpg
 
Kwani hivi sasa kuna watalii gani wanaokuja hapa nchini wakati karibu kila nchi inajihami?

Lengo ni serikali inataka kuonyesha kuwa inachukua hatua au ndio wanarekebisha kauli ya Polepole yaani wanafanya damage control?

Kama wana dhamira ya kweli,basi wazuie wageni wote wasio na ulazima kuingia nchini kama nchi zingine wanavyofanya maana corona hailetwi na watalii peke yake.
 
Mmmh siamini maana polepole si alisema hawawezi kustopisha safari za watalii
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii mh Kanyasu amewataka watalii waliopanga kutembelea Tanzania kuahirisha safari zao hadi pale ugonjwa wa Corona utakapokuwa umedhibitiwa.

Mh Kanyasu amewataka watalii hao kutofuta safari zao bali waahirishe kupisha hili janga linaloisumbua Dunia kwa sasa.

Source ITV habari!

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Siasa hazina maana ya upumbavu.
Ni makosa makubwa sana kufikiria kuwa siasa inahusika na udanganyifu, ujinga, uongo na upumbavu.
Na ndio maana unapata tabu kuelewa kwani na hujui 3 inaweza kuwa 2!!
Siasa sio njia nyoofu ya hakika ndio maana unaona mapindo mengi na utashuhudia mipindo kwani anaepinda ni yuleyule alietengeneza njia inayoweza kupinda hivyo imepinda njia ndio maana wapitao wanapinda pia.

NB: Usitumie nguvu kubwa kunielewa hapa😏
 
Back
Top Bottom