Serikali yawataka wanaotoa tiba kwa kutumia vyakula kuendesha shughuli hizo kwa kibali cha Wizara ya Afya

dope bwoi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
234
591
Dodoma. Serikali imesema watu wanaojiita watoa tiba kwa kutumia vyakula wanatakiwa kuendesha shughuli hiyo kwa kibali cha Wizara ya Afya.

Katazo hilo limetolewa na mganga mkuu wa Serikali, Dk Aifello Sichwale jana Ijumaa Septemba 11, 2021 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu magonjwa yasiyoambukiza ambayo baadhi amesema yanatokana na ulaji wa vyakula usiofaa.

Dk Sichwale amesema kumeibuka wimbi kubwa la wanaojiita watoa tiba mbadala kwa wananchi wakitumia mchanganyiko wa vyakula na hawana utaalamu wowote.

Amesema siyo dhambi mtu kutoa elimu ya mchanganyiko wa chakula lakini anapaswa kuwa amepewa kibali na Wizara ya Afya.

“Hatuwezi kuruhusu watu wakaendelea kujitangaza katika mambo yenye kuhatarisha afya za watu, kama kuna mtu ana uwezo wa kutoa elimu ya mchanganyiko huo aje kwetu na tutakapojiridhisha kuwa anaweza kusaidia jamii, tutampa kibali cha kufanya hivyo ili asisumbuliwe,” amesema Dk Sichwale.

Ameeleza sababu za kutoa zuio hilo ni kutokana na kuibuka kwa magonjwa yasiyoambukiza yanayotokana na ulaji wa vyakula usiofaa chanzo kikiwa washauri wa mchanganyiko wa chakula.

Chanzo: Mwananchi
 
😂😂 Mwaka sijui itakuaje mana wamemsagia kungun na huku sijui atakuja na style gan
 
Jamaa wanatengeneza hypothetical super foods.....simply kwa kupiga ramli...
 
Wameanza vita kupiga vita dawa yetu ya lishe ya Corona in watulazimishe hiyo chanjo ya johnson ya wa marekani
 
Mngeanza na Dorothy alikuwa anasaga vitunguu, malimau, tangawizi na pilipili ili kutibu corona
IMG_20210209_162802.jpg
 
Tiba mbadala zimesaidia sana sie wa Uswahilini kwny Janga la Corona hadi sasa ndio sababu ya sisi 'Wajinga wajinga' kupuuza chanjo zao…sasa hivi wameamua kuangamiza silaha zetu za asili kutukomesha
 
Nchi yetu ya ajabu sana kwani imezubaa kwa muda mrefu watu wameibiwa na wanaendelea kuibiwa sana huko kwenye tiba mbadala na vijikanisa vya upigaji mitume na manabii wanazuka kila kukicha na wanafanya mambo ya ajabu halafu hawataki kuguswa wanadai kinachosemwa na roho mtakatifu akijadiliwi.
 
Back
Top Bottom