Serikali yawataka wakulima wa korosho kurudisha fedha, korosho zao hazina ubora

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
2,368
2,000
Mbunge wa Tandahimba Katani Ahmed Katani amefunguka na kusema serikali imewataka baadhi ya wakulima kurudisha fedha walizolipwa baada ya korosho zao kuonekana hazina ubora

Amesema korosho hazijawahi kuwekewa madaraja tangia waanze kuzalisha korosho ila serikali ilipoamua kununua ndipo ikajitokeza korosho nyingine kuitwa za daraja la pili

Korosho zinazofikikia tani 50 zimerudishwa kwa wananchi na huku zaidi ya tani 2, 000 zikisemwa ni daraja la pili

 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,522
2,000
Ina maana walinunua bila ya kuhakikisha ubora?

Sasa Kwanini walishinikiza Wafanyabiashara binafsi wanunue korosho zote kwa bei Moja Elekezi wakati Korosho wametambua zina Madaraja?

Tatizo la Wanasiasa wetu wanaamini wao wana weledi wa Biashara, Uvuvi , kilimo, uimbaji, uchezaji Mpira , U DJ , n.k

Eneo pekee wanaloheshimu taaluma Ni Uchawi ndio sababu wachawi hawabughudhiwi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom