Serikali yawasilisha mapendekezo ya bajeti ya 2022/2023 ya Tsh trillioni 41.06

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,872
Waziri wa fedha Dr Mwigullu Nchemba leo amewasilisha mapendekezo ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ya tsh 41.06 trillioni.

Dr Mwigullu amesema Kilimo kitapewa kipaumbele.

======

SERIKALI YAPENDEKEZA BAJETI YA SH TRILIONI 41

WAZIRI wa Fedha, na Mipango, Mwigulu Nchemba amewasilisha mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Ukomo wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 ambapo serikali inakusudia kukusanya na kutumia Sh trilioni 41.06.

Katika Taarifa ya Nchemba, kiasi cha Sh trilioni 28 sawa na asilimia 70 ya mapato kitatokana na makusanyo ya ndani.

Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha, Bajeti ya mwaka ujao itagusa maendeleo ya Jamii hususani sekta ya Kilimo ambayo itatengewa kiasi kikubwa.

Makadirio ya mwaka wa fedha 2022/203 ni ongezeko la asilimia 13 ya makadirio ya mapato kwa mwaka wa fedha 2021/2022, ambapo serikali ilitarajiwa kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 36.33.

Kati ya fedha hizo mapato ya ndani yalitarajiwa kuwa shilingi trilioni 26.03 sawa na asilimia 71.7 ya bajeti yote.
 
Back
Top Bottom