Serikali yawapoza wahisani kwa hoja za ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yawapoza wahisani kwa hoja za ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by never, May 14, 2011.

 1. n

  never JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  TUHUMA za ufisadi zinazoikabili serikali zimechukua sura mpya baada ya Rais Jakaya Kikwete kuagiza ripoti ya tathmini ya rushwa ianikwe mbele ya umma ili uweze kufahamu kabla ya kujadiliwa na Baraza la Mawaziri.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika mkutano wa pamoja na nchi wahisani.

  Wakati hayo yakiendelea ndani ya serikali wadau wa kimataifa wa maendeleo kutoka nchi 12 duniani wameamua kuchangia bajeti ya serikali ya Tanzania kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 dola za Marekani milioni 580 sawa na sh bilioni 840 kwa ajili ya shughuli za maendeleo huku nchi za Uholanzi na Uswisi zikitangaza kijitoa kuchangia bajeti kutokana na mtikisiko wa uchumi.

  Fedha hizo ni nyingi ukilinganisha na sh bilioni 814 zilizotolewa mwaka wa fedha uliopita huku wadau kutoka nchi mbili wakijitoa.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, serikali imejigamba kuwa pamoja na kujitoa kwa nchi ya Uholanzi na Uswisi bado imeweza kufanikiwa kupata kiasi kikubwa cha fedha.

  Hata hivyo nchi hizo zimesema kuwa zitaendelea kufadhili miradi yao ya maendeleo nchini.

  Akitetea mbele ya wahisani hao, ambao mara kwa mara wamekuwa wakitishia kusitisha kuchangia bajeti kutokana na kuwapo kwa tuhuma za rushwa dhidi ya serikali, Waziri Mkuu Pinda alisema ripoti ya hali ya rushwa nchini imetoa picha halisi ya hali ya rushwa na inatarajiwa kutolewa wakati wowote baada ya taratibu kukamilika ili iweze kutangazwa kwa umma na kisha wananchi waijadili kwa kina.

  Pinda alisema alikuwa hajui suala hilo lakini kwa siku ya jana alibahatika kuongea na Rais Kikwete na ndipo aliporuhusu tathmini ya ripoti hiyo itolewe kwa Watanzania na hakuna sababu ya kusubiri hadi kujadiliwa na Baraza la Mawaziri.

  Alisema ufadhili wa kukamilisha tathmini hiyo ulifanywa na wadau hao wa maendeleo kutoka nchi mbalimbali duniani ambao walitaka kufahamu kiwango cha rushwa na maeneo ambayo inaonekana kuota mizizi huku wananachi wakiendelea kuwa maskini.

  Alisema baada ya kutolewa kwa fedha za ufadhili huo kazi ikaanza kwa waliopewa jukumu hilo ambao ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) kwa kuzunguka kwa wananchi.

  Pinda alisema serikali inaendelea kukabiliana na kupambana kwa nguvu zote na rushwa nchini lakini akaongeza kuwa ni wakati muafaka kuhakikisha mianya ya rushwa iliyopo katika maeneo mbalimbali inazibwa na kuiwezesha nchi kupata mapato.

  “Wadau wa maendeleo wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza juhudi katika kupambana na rushwa na hata kutoa fedha kiasi kikubwa kama hicho ni wazi wamefurahishwa na kazi nzuri tunayoifanya.Hivyo tutaendelea na kazi hiyo,” alijitetea Pinda.

  Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo alisema fedha hizo zilizotolewa kwa ajili ya kuchangia bajeti ya mwaka wa fedha ujao ni hatua nzuri inayoonesha bado wafadhili wana matumani makubwa katika kusaidia maendeleo ya wananchi na kuongeza kuwa safari hii wahisani hao wameamua kuongeza ufadhili ukilinganisha na mwaka uliopita.

  Nchi zilizochangia kusaidia bajeti ni Canada , Demark, Umoja wa Nchi za Ulaya (EU), Finland, Ireland, Japan, Norway, Sweden, Uingereza, na Benki ya Dunia (WB).

  Naye Mwenyekiti wa Wadau Maendeleo wa Kusaidia Bajeti Kuu ya Serikali (GBS) anayemaliza muda wake, Balozi wa nchi ya Norway, Ingunn Klepsvik, alisema pamoja na kutoa kwa fedha hizo bado kuna maeneo ambao Serikali ya Tanzania inatakiwa kuweka kipaumbele katika kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa.

  Aidha alisema hata kama kuna masuala ya changamoto katika utekelezaji bado wanasisitiza kuwa iko mbele zaidi ya nchi nyingine za bara la Afrika.

  Mwenyekiti huyo alisema kuwa bado Tanzania haijaweza kugharamia shughuli za maendeleo kwa kutumia makasanyo yake ya ndani.

  Alisema kuna uhitaji wa kuongeza makusanyo katika mapato ya ndani ili kuiwezesha serikali kujiendesha kwa kutumia fedha zake.

  Alisisitiza umuhimu wa kuongeza kodi kutoka sekta ya madini kwa sababu sasa hivi makusanyo yanyotokana na sekta hiyo yanaendelea kuwa chini.

  Klepsvik alisema serikali inatakiwa kuweka mkazo katika maeneo matatu ambayo ni kutoa huduma ya jamii kwa usawa na ubora.

  Maeneo mengine aliyoishauri serikali kuweka mkazo ni ukuaji endelevu katika sekta ya kilimo ambayo inabeba watu wengi walio maskini.

  Pia alishauri serikali akisema kuwa ni lazima ibadilishe mazingira ya biashara na uwekezaji.

  Kati ya maeneo mengine ambayo alishauri kuboreshwa ni katika utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa.

  chanzo Tanzania daima ya leo
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  May 14, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wahisani jitoeni kutusaidia ili tutumie rasilimali zetu zinatosha sana! Tatizo tulilo nalo ni managementi!
   
 3. R

  Red one Member

  #3
  May 14, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Pinda ni mnafiki sana, asichojua ninini? Kwani kilcho mfanya mwenzake ajiuzulu uwaziri mkuu ilikuwa ni usafi? Nyambafu zao nchi imewakalia pabaya wanahaha sasa,
   
 4. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Wahisani wanatudumaza.waondoke tujitegemee.
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  na hilo ndo lengo lao tuendelee kuwa masikini wa milele!
   
 6. F

  Froida JF-Expert Member

  #6
  May 14, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Mambo ya kudhalirishwa hayo unapewa fedha kwa masharti wakati tunauwezo kabisa wakujisimamia tukiamua na kuendesha mambo yetu wenyewe bila vitisho vya aina yeyote,wanalo lao hao wafadhili makampuni yao ndio yanavuna madini,samaki,ndio wenye vitalu vya uwindaji,maNGO makubwa yanayosimamia miradi ya elimu,afya,mazingira ,utawala bora wakilipwa mishahara ya kukufuru,hawana maana
   
 7. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #7
  May 14, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  JK na chama tawala CCM:Mbele ya wahisani"TUNAPAMBANA NA RUSHWA NA UFISADI"Mbele ya Walalahoi"HATUNA RUSHWA WALA UFISADI NI UZUSHI WA WAPINZANI"
   
 8. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #8
  May 14, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mbona siamini kama ni kweli hatuna uwezo wa kupata bil 840 tofauti na makusanyo ainishwa mpaka tuwanyenyekee haya majambazi kutoka magharibi.
   
Loading...