Serikali yawapandisha madaraja watumishi wa umma 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939

Serikali imewapandisha madaraja watumishi wa umma 113,520 walioajiriwa mwaka 2012 katika awamu tatu, ambapo ya kwanza walipandishwa vyeo Watumishi 28,049 waliokuwa wameidhinishiwa vyeo kabla ya zoezi la uhakiki wa watumishi hewa na uhakiki wa vyeti kuanzia mwezi Juni, 2016, awamu ya pili ilianza mwezi Novemba, 2017 na ilihusisha watumishi 59,967 ambao taarifa zao zilikuwa kwenye Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kabla ya zuio na awamu ya tatu ilianza mwezi Aprili, 2018 na ilihusisha Watumishi 25,504 ambao barua zao zilikuwa hazijaingizwa kwenye Mfumo.

Ufafanuzi huo, umetolewa Bungeni jana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) wakati akijibu swali la Mhe. Joram Hongoli (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililohusu watumishi wa umma walioajiriwa 2012 kutopandishwa madaraja mpaka hivi sasa.

Dkt. Mwanjelwa alisema, watumishi walioajiriwa Mwaka 2012 walistahili kupandishwa madaraja kuanzia mwaka 2016/2017 kipindi ambacho Serikali ilikuwa ikifanya zoezi la uhakiki wa watumishi hewa na uhakiki wa vyeti, hivyo mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Serikali ilianza kuwapandisha watumishi hao kwa awamu hizo tatu kwa kuzingatia vigezo stahiki na kuongeza kuwa watumishi wengine ambao wamekidhi vigezo wataendelea kukasimiwa katika bajeti ya mishahara ili waweze kupandishwa vyeo katika mwaka huu wa fedha 2018/2019.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa aliainisha kuwa, watumishi 31,188 walioajiriwa na TAMISEMI mwaka 2012, kati ya hao watumishi 15,320 wamepandishwa vyeo na kubadilishiwa mishahara, na watumishi 3,349 waajiri wao wamewapandisha vyeo lakini majina yao yapo UTUMISHI kwa ajili ya kupitia taarifa zao kabla ya kuwabadilishia mishahara na watumishi 1,064 waliopandishwa vyeo wamebainika kuwa na hoja mbalimbali ambazo waajiri wanapaswa kuzikamilisha na kurejesha majina yao UTUMISHI kwa ajili ya kuwaidhinishia mishahara.Watumishi 4,552 hawapo tena katika Utumishi wa Umma na watumishi 6,903 bado hawajapandishwa vyeo ambapo Serikali inatarajia kuwapandishwa vyeo wakati wowote katika mwaka huu wa fedha 2018/19.

Suala la upandishwaji vyeo kwa Watumishi wa Umma linazingatia vigezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na utendaji kazi mzuri, kukidhi sifa zilizoainishwa katika Miundo ya Maendeleo ya Utumishi, uwepo wa nafasi wazi na bajeti iliyotegwa.

Kwa mujibu wa Miundo ya Maendeleo ya Utumishi, mtumishi anapaswa kutumikia cheo kimoja si chini ya miaka mitatu kabla hajafikiriwa kupandishwa cheo.

Aidha, iwapo mtumishi ameajiriwa kwa mara ya kwanza atapaswa kumaliza mwaka mmoja wa kuthibitishwa kazini kisha ndipo atumikie cheo hicho si chini ya miaka mitatu, hivyo kwa kuzingatia sifa mtumishi anaweza kupandishwa cheo baada ya miaka 3, 4, 5 au hata saba kutegemea na kukidhi vigezo stahiki.

Imetolewa Na:
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi Ya Rais (Utumishi)
Tarehe 15 Novemba, 2018.
 
Duh! Hongereni kwa watumishi mlioula. Angalau sasa nafuu ya maisha itapatikana baada ya mshahara mpya kuanza ku reflect kwa watumishi hao.

Labda unaambie kuwa hii kejeli nitakuelewa! Hivi nikikuambia kuna watu walipandishwa january 2016 wakanyang'anywa wakapewa tena nov. 2017 wapokwa kisha wakapewa barua ya tatu ya April 2018 hadi leo hawajabadilishiwa mshahara utaamini? Hii nchi sasa imezidisha masihara kwa watu wazima! Kama hawana pesa wajinyamazie badala ya hizi drama!
 
Inakatisha tamaa sana! Kuna mwalimu alipandishwa daraja tangu mwaka jana baadae wakamnyang'anya kwa madai ya uhakiki, mwezi April mwaka huu akapewa daraja lake tena, lakini mshahara haujabadilishwa mpaka leo. Kuna jambo haliko sawa waliseme tu.
 
Mkuu uzalendo umeanza kupotea!?

Uzalendo wangu upo Kwa kiwango kisichomithilika

Kama kipimio Ni Mlima Basi Ni Everest , Kama Ni Bahari Ni Atlantik

Kama Ni mbuga Basi Serengeti

Uzalendo namba Moja ni Kuwa mkweli Na ndio funzo kuu tangu enzi na enzi

Sheikh wangu Usihofu Mie sio CCM deadline or CCM vyeo mie Ni CCM itikadi
 
Back
Top Bottom