RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Serikali imewapa miezi miwili wananchi waishio katika kijiji cha michezo cha Changamani kilichopo Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam kuhama katika eneo hilo kupisha uendelezwaji wa kijiji cha mchezo.
Agizo hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge alipokutana na wananchi hao katika kikao cha kujadili na kukubaliana muda wa kuhama katika eneo hilo leo Jijini Dar es Salaam.
“Ndugu zangu tumejadiliana wote na kukubaliana kuwa baada ya miezi miwili mtakuwa mmeshaama katika eneo hilo kupisha uendelezwaji wa kijiji cha michezo kwa ajili ya shughuli za mbalimbali za michezo” alisisitiza Bw. Nkenyenge.
Naye Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw.Julius Mgaya amesema kuwa mpango wa kuwahamisha wananchi hao unalenga kutekeleza mradi wa kijiji cha michezo kitakachojengwa kwa ajili ya kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo mbalimbali.
Kwa upande wake mmoja ya wawakilishi wa wananchi hao Bw.Atillio Mballa amesema wamekubaliana na muda huo waliopewa na watafikisha ujumbe huo kwa wenzao na kabla ya muda hujafika watakuwa wameshatekeleza agizo hilo.
Katika mpango wa kukuza na kuendeleza michezo nchini Serikali imejipanga kukuza sekta ya michezo nchini na kuifanya kuwa moja ya rasilimali itakayochangia katika pato la taifa.