Serikali yawanyang'anya mashine za maji wakulima na kusababisha kukauka kwa ekari 200 za vitunguu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Kazi ya mkuu wa wilaya
Screenshot_2016-11-27-20-33-24.png
Screenshot_2016-11-27-20-33-24.png
Screenshot_2016-11-27-20-24-21.png
 
Hakuna. Mungu hayupo. Tufanye dhambi halafu tumsingizie Mungu? Inaendelea kula kwetu.
 
Iko hivi jamani, kiutaratibu mtu anapochukua/kuhitaji maji toka mtoni ,ziwani,chemchem na hata tu kuchimba kisima chake mwenyewe, NI LAZIMA apate kwanza kibari cha kutumia maji (water permit).

Kwakuwa wao wapo kwenye kikundi kilichosajiliwa, walitakiwa (na wanajua) kwenda Ofisi ya Bonde la mto Pangani (Moshi) kwa ajili ya kupewa ridhaa ya kutumia kiasi MAALUMU cha maji toka mtoni kwa kuangalia ukubwa wa eneo lao na aina ya mazao wanayolima (Vitunguu/mbogamboga).

Hiyo ni sheria kabisa ya maji iliyopitishwa na Bunge. Usipowabana, wanachukua pump kubwa tena nyingi na wanyonye maji mtoni bila utaratibu,kitu ambacho hukausha au kupunguza maji mtoni.

Ikumbukwe pia, upande wa chini ya mto (downstream point) kuna watumiaji wengine wa mto na kuna viumbe hai wanaotegemea huo mgao wa maji.

Mfano:

Ziwa jipe (Wilayani Mwanga) ndo chanzo cha mto Kifaru ambao hupeleka maji Bwawa la Nyumba ya Mungu ambapo ndo mto Pangani (unaoenda mpaka baharini) umeanzia hapo.

Sasa ukiwaruhusu ovyo wananchi wakanyonya maji ya mto Kifaru, nn kitatokea?

Tatizo tu elimu na mkazo vitolewe kwa wananchi hao,siyo kulalama.
 
Back
Top Bottom