Entim
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 4,021
- 2,253
So dawa ni kuwanyang'anya mashine zote ili vitunguu vikauke? Au wangeregulate maji kwa kutumia gate? Unazungumziaje issue ya mvua kuchelewa?Iko hivi jamani, kiutaratibu mtu anapochukua/kuhitaji maji toka mtoni ,ziwani,chemchem na hata tu kuchimba kisima chake mwenyewe, NI LAZIMA apate kwanza kibari cha kutumia maji (water permit).
Kwakuwa wao wapo kwenye kikundi kilichosajiliwa, walitakiwa (na wanajua) kwenda Ofisi ya Bonde la mto Pangani (Moshi) kwa ajili ya kupewa ridhaa ya kutumia kiasi MAALUMU cha maji toka mtoni kwa kuangalia ukubwa wa eneo lao na aina ya mazao wanayolima (Vitunguu/mbogamboga).
Hiyo ni sheria kabisa ya maji iliyopitishwa na Bunge. Usipowabana, wanachukua pump kubwa tena nyingi na wanyonye maji mtoni bila utaratibu,kitu ambacho hukausha au kupunguza maji mtoni.
Ikumbukwe pia, upande wa chini ya mto (downstream point) kuna watumiaji wengine wa mto na kuna viumbe hai wanaotegemea huo mgao wa maji.
Mfano:
Ziwa jipe (Wilayani Mwanga) ndo chanzo cha mto Kifaru ambao hupeleka maji Bwawa la Nyumba ya Mungu ambapo ndo mto Pangani (unaoenda mpaka baharini) umeanzia hapo.
Sasa ukiwaruhusu ovyo wananchi wakanyonya maji ya mto Kifaru, nn kitatokea?
Tatizo tu elimu na mkazo vitolewe kwa wananchi hao,siyo kulalama.