Serikali yawahamisha kwa nguvu na kuwachomea moto nyumba wakazi wa Chanika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yawahamisha kwa nguvu na kuwachomea moto nyumba wakazi wa Chanika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MwanaHaki, Feb 26, 2011.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Breaking News: Habari zilizothibitishwa hivi punde ni kwamba, siku moja kabla ya mambomu kulipuka kutoka kambi ya Jeshi ya Gongo la Mboto, Serikali, kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, imewahamisha kwa nguvu wananchi waliokuwa, wakazi wa eneo la Chanika, kwa kisingizio kwamba eneo hilo ni sehemu ya Hifadhi ya Msitu wa Kazimzumbwi, ambao kisheria upo Wilaya ya Kisarawe. Chanzo cha habari hizi kinasema kwamba, wananchi wanaoishi kwenye eneo hilo wamethibitisha kwamba eneo hilo halipo Kisarawe bali lipo Wilaya ya Ilala, na kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2010, walipiga kura wakiwa Jimbo la Ukonga.

  Habari zaidi zinasema kwamba, licha ya Waziri Maige kukataa kusema chochote juu ya sakata hilo, fununu zaidi zimetamka kwamba eneo hilo lina mafuta na madini mengi, na wakati alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Da es Salaam, Kanali Mstaafu Yussuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM, aliliuza eneo hilo kwa mzungu anayeitwa Anna Thomas, katika mazingira ya kutatanisha, bila kuishirikisha Serikali ya Mtaa huo.

  Hivi sasa, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa anashikiliwa na vyombo vya dola, baada ya mmoja wa Askari wa Maliasili aliyehusika katika zoezi la kuwahamisha kwa nguvu wananchi hao, pamoja na kuwachomea moto nyumba zao, kuuwawa na wananchi hao, katika mapigano na vurugu hizo zilipotokea.

  Kwa taarifa zaidi, waandishi wa habari mnaombwa kuwasiliana na wakazi wa eneo hilo, mmojawapo akiwa Zorab Masimba, ambaye sasa amehamia Masaki kutokana na sakata hilo. Masimba anapatikana kwa namba 0717-084647.
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Naota nadanganywa, kwamba uchaguzi uliopita walipiga kura wakiwa jimbo la ukonga?!
   
Loading...