Serikali yawaangushia rungu wakazi wa mabondeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yawaangushia rungu wakazi wa mabondeni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Dec 29, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280

  [​IMG]
  Mkuu wa Mkoa wa Da es Salaam, Said Meck Sadiki


  Serikali imewaamuru waathirika wote wa mafuriko jijini Dar es Salaam waliohifadhiwa katika makambi ya shule za msingi na sekondari waondoke mara moja ikikapo Desemba 5, 2012.

  Kuamuriwa kuhama tarehe hiyo kuna lengo la kuwapisha wanafunzi wa shule hizo ambazo zitafunguliwa Januari 9, mwakani.

  SERIKALI HAITAWAJENGEA NYUMBA

  Kadhalika, Serikali imesema haina mpango wa kuwapa fedha za kwenda kujengea nyumba kwenye viwanja ilivyowapa katika maeneo ya Mabwepande kwa kuwa sio wajibu wake.

  Agizo hilo la Serikali lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Da es Salaam, Said Meck Sadiki, jana kwa waandishi wa habari.

  Sadiki alisema wapangaji wote walioathirika na mafuriko ambao kwa sasa wanahifadhiwa katika makambi na sehemu nyingine waondoke mara moja na kwenda kupanga sehemu nyingine kwani serikali haitawahudumia tena ifikapo Januari 5.

  Alisema watu wote waliojenga na kuvamia maeneo ya bonde la mto Msimbazi, viwanja vya Jangwani na maeneo mengine ya mabondeni waondoke mara moja kabla ya nguvu ya dola haijaanza kutumika kwani maeneo hayo ni hatari kwa maisha yao.

  VIWANJA 700 VIMESHAPIMWA

  Mkuu huyo wa mkoa alisema, Serikali imetenga maeneo katika eneo la Mabwepande jirani na kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill, ambako viwanja 700 kati ya 2,400 vimeshapimwa na taratibu za ugawaji zitafuata.

  Aidha, Sadiki alitaja kifungu kidogo cha sheria kinachowazuia wakazi wote wa mabondeni wasijenge wala kuishi katika maeneo hayo.

  Alitaja sheria hiyo kuwa ni namba 40 ya mwaka 1993, ambayo inasema kuwa, maeneo ya mabondeni yatachukuliwa na Halmashauri ya Jiji yakiwemo ya viwanja vya Jangwani, bonde la mto Msimbazi na maeneo yote yaliyopo mabondeni.

  Aliongeza kuwa, watu wote waliopewa vibali vya kujenga mabondeni serikali haivitambui na kuwataka wawatafute waliowapa.

  Alisema serikali haiwezi kuwaachia wananchi hao warudi maeneo ya mabondeni kwa kuwa vifo vya watu 40 vilivyotokana na mafuriko ya wiki iliyopita ni vingi na kwamba haitawavumilia tena.

  Kwa upande wa wapangaji waliokumbwa na mafuriko hayo, Sadiki, alisema: “Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi hairuhusu mpangaji yeyote kulipa kodi ya pango ya mwaka mzima, hivyo malalamiko yao hayatasikilizwa.”

  NIPASHE ilipita katika baadhi ya makambi ya waathirika hao na kuwashuhudia wakiendelea kuishi hapo, huku huduma za kijamii zikiendelea.

  Mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam kwa siku tatu mfululizo kuanzia Jumanne hadi Almahisi wiki iliyopita, zilisababisha maafa makubwa katika maeneo mbalimbali, ambapo barabara zilifungwa kutokana na kujaa maji, makazi ya watu kuzingirwa na maji, madaraja kukatika na watu 40 kufariki dunia.

  TMA: MAFURIKO MENGINE YAJA

  Katika hatua nyingine, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imewatahadharisha wakazi wa mabondeni kuwa mvua nyingine kubwa zinatarajiwa kuanza kunyesha kuanzia leo katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kusababisha mafuriko mengine.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi, mvua hizo pia zinatarajiwa kuharibu miundombinu.

  Dk. Kijazi, alisema kuna ongezeko la joto katika ukanda wa Bahari ya Hindi na kwamba hatua hiyo itasababisha kuwepo kwa mvua kubwa katika kipindi cha kuelekea mwaka mpya wa 2012.

  Alisema licha ya ongezeko la joto, lakini pia kuna unyevunyevu unaotoka ukanda wa misitu ya Kongo, hali ambayo pia itachangia kunyesha mvua kubwa.

  Alitaka tahadhari za haraka kuchukuliwa hasa kwa wananchi wanaoishi mabondeni, ili kuepuka uharibifu wa mali na vifo ambavyo vinaweza kusababishwa na mafuriko.

  Aliahidi kuwa TMA itaendelea kutoa taarifa mbalimbali zinazohusiana na mvua kwa kadri watakavyopata taarifa za utafiti wa kitalaam.  CHANZO: NIPASHE


   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Yani hii serikali, natamani kungekua na uwezekano wa kuondokana nayo.

  Kwanza inaacha watu wajenge alafu sasa hivi wanadai hawatambui vibali walivyopewa?Kama kweli walikua hawavitambui kwanini hawakuingilia kati wakati watu wanaanza kujenga? Kama watu walipewa vibali na manispaa (hata kama wanadai sio halali) ina maana kwamba serikali inafanya mambo hovyo, kwamba yeyote anaweza kufanya chochote hata kama sio sahihi.

  Ningependa sana kuona upinzani toka kwa hao wananchi waliojibanza hapo shuleni alafu tuone hiyo serikali uchwara itafanya nini.Alafu hili nalo liwe somo kwa wale wadanganyika wanaoumizaga watu na vikofia vyao vya njano.Ukikubali kununuliwa kwa bei rahisi, kubali kutumiwa na kutupwa kirahisi!!!
   
Loading...