Serikali yawa bubu kuhusu vyombo vya dola kumdhalilisha mbunge arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yawa bubu kuhusu vyombo vya dola kumdhalilisha mbunge arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Dec 21, 2010.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Rais, wabunge na madiwani ni wachaguliwa na wananchi, na wanalindwa na vyombo vya dola kimsingi tokana na wajibu wa kazi zao wakiwa ndio sauti za wananchi. Vyombo vya dolla vina utararatibu na sheria kiutendaji katika utekelezaji wa wajibu wao kadiri ya nafasi na mazingira waliyo nayo. Sheria nazo ambayo ndiyo kinga na mwongozo katika utendaji wa kila siku ndiyo dira ya namna elekezi ya utekelezaji wa kila mhusika awe kiongozi au chombo cha dola bila kumweka kando raia.

  Kuna sheria za jumla (universal law) ambazo ni chimbuko na msingi wa nchi nyingi duniani kutunga sheria, ndizo zinazolinda zaidi haki za binadamu na wajibu na utaratibu wa vyombo vya dola katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

  Raia wa kawaida wana uhuru katika kufuata itikadi za sera za kisiasa iwe kwa kushabikia au kuwa wanachama kwa kufuata taratibu zainazokubalika kwa ajili ya kujenga hoja ya kuleta haki na usitawi wa jamii katika mazingira yao. Lakini vyombo vya dola vinavyolinda haki ya jamii havijiungi au kushabikia sera au chama cho chote cha siasa, kwa vile huwa kuna itikadi tofauti baina ya vyama vya siasa, kwa maana hiyo walio katika vyombo vya dola hawaruhusiwi kushiriki ili kutojihusisha na masuala ya kiitikadi badala yake wasimamie sheria za nchi na za mahali zifuatwe bila kujali itikadi za vyama vya siasa.

  Sheria ya jumla ninavyoifahamu haimruhusu polisi kumpiga raia au kiongozi ye yote, isipokuwa kama amekosea sheria atashikwa kwa utaratibu unakubaliwa na jeshi la polisi. Polisi huweza kutumia nguvu za kumshika mtu ambaye anatumia nguvu kujikinga asishikwe. Hali kadhalika polisi anaweza kumpiga mtu anayeshikwa kama kinga asidhurike iwapo huyo anayeshikwa anampiga polisi, hivyo polisi hutumia njia za kujihami asipigwa. Polisi hawezi tumia silaha dhidi mtu isipokuwa pale tu polisi atatumia silaha kama mtu atatumia silaha kutaka kumdhuru polisi.

  Polisi hupata mafunzo ya elimu ya jamii na falsafa ya kikazi na kuishia kidipolomasia, ili wafanye kazi zao kiufanisi zaidi. Kama polisi anakuwa mwerevu katika kutumia mafunzo yake vizuri aliyopata chuoni katu hatadiriki siku moja kutumia hisia tu za kishabiki na kuanza kumpiga buti raia au kiongozi.

  Cheo cha mbunge ni kikubwa na kwa mantiki hiyo chombo cha dola kinapomdhalilisha mbunge au mchaguliwa na wananchi anayedhalilishwa ni mwananchi aliyemchagua. Na mazingira yanayotokana na udhaliliswaji huo ni dhahiri ushabiki wa kisiasa badala ya taratibu na wajibu wa kazi yao. Na kama udhalilishwaji huo wa kumpiga mbunge ungefanywa na polisi wa cheo cha chini wakubwa wangekuwa na kisingizio cha uelewa mdogo wao, lakini kufanywa na polisi mwenye kutoa maelekezo ya utekelezaji kwa polisi wa cheo cha chini ambao ndio watendaji wa kila siku kulinda amani mitaani, ni aibu na inatoa taswira mbaya mno katika uongozi wa serikali tuliyo nayo.

  Polisi anapojichukulia sheria na kuitumia atakavyo bila kufuata utaratibu na miiko ya kazi yake ni matokeo ya mfumo wa viongozi wa serikali usivyokuwa wa kufuata sheria na utaratibu ambao umewekwa kwa manufaa ya nchi. Wanachojali zaidi ni maslahi binafsi badala ya umma uliowaweka madarakani. Ndio maana utakuta kila kiongozi anatoa tamko tofauti na mwingine katika nafasi mbalimali katika suala moja, hapo inaonyesha wazi udhaifu wa uongozi uliopo usivyokuwa na mshikamano, na tafsiri yake ni kwamba kila kiongozi yupo kwa maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.

  Serikali makini na viongozi makini katika utawala bora ulitakiwa kutoa tamko la kilichotokea Arusha mbunge kupigwa na polisi wakati mbunge hakutumia nguvu hakumpiga polisi na wala hakuwa na silaha ya kumtishia polis. Polisi mwenye ujuzi wake angetumia njia ya kistaarabu na kidiplomasia kumweka sawa mbunge na kunyoosha mambo yaende sawa badala ya kutumia hoja ya nguvu badala ya nguvu ya hoja. Ni aibu kutumia nguvu kunyamazisha madai ya haki badala ya kufuata sheria muafaka ili kulinda haki nchini.

  Nini maana ya utawala bora? Nini kazi ya Rais, Waziri mkuu, waziri wa Tumisheni, waziri wa utawala bora, waziri wa katiba na sheria, waziri shughuli za bunge na Spika wbunge wamefumba vinywa katika kutolea ufafanuzi, au kulaani kitendo kilichofanywa na polisi Arusha? Huo ndio utawala bora wa CCM? Hiyo ndio njia ya kuua demokrasia au kuvuruga upinzania nchini?

  Nahitimisha kwa kusema maji hufuata mkondo. Huwezi kulazimisha maji kwenye mto eti yarudi yalikotoka, hata kwa mwenye akili ndogo hatakubaliana nawe kabisa. Ukifunga njia ya maji leo kesho utakuta yametoboa njia na yanaendelea na safari yake kuelekea baharini au ziwani. Kumbuka kama huwezi lazimisha maji yarudi yalikotoka, hapana budi kuyaacha yaendelee kule yanakoelekea, na kama una akili iliyopevuka endeleza mkondo wa maji yaendako badala ya kuyapinga.
  WAKATI UKUTA!
   
 2. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Una uhakika na unachosema? nani alifanya fujo? alifanya fujo kwa namna gani?

  Hoja ya sasa haipo katika suala la kumshughulikia aliyefanya fujo bali ni juu ya serikali kukaa kimya juu ya hicho kilichotendeka.
   
 3. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Walipomruhusu mbunge wa viti maulum kutoka Tanga kuingia kwenye kikao cha madiwani wa Manispaa ya Arusha hiyo siyo fujo? Au wewe fujo unaiona kwa miwani ya CCM?
   
 4. Gwaje

  Gwaje JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 271
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 45
  tuwe makini na ccm
   
 5. Fabolous

  Fabolous JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 1,302
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  Una ugonjwa wa akili wewe si bure
   
 6. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  nyoooo!
   
 7. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,535
  Trophy Points: 280
  Kwani Marekani ndo nini? Na ni wapi? Malaria Sugu ana maajabu! Na utazijua tu akili za wale wanaopenda kushinda gengeni tu na kisha kucheza bao!
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Huyu Yaya naona hapa si mahali pake na wala si kosa lake kuenenda jinsi anavyofanya. Ni Makosa ya akina ndugu Invisible na Maxence Melo kutokumelekeza JF-Jukwaa la UMBEA ambako ni RUKSA mtu kupenda na / au kuchukia jambo bila kusumbuliwa na mtu kwamba akatoe sababu au kithibitisho cha madai yake.

  Modes, hebu msaidieni huyu ndugu au akapelekwe kwa Rev Masanilo atamkumbuka KWA MAOMBI sawa sawa na jinsi alivyomkumbukua MTUNDU WETU MMOJA (japo sasa hivi nam-misi misi hivi na mizaha yake) hivi kwa jina la MALARIA SUGU mpaka akapata kutulizwa tulii mpaka leo hii.
   
 9. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Yaya unaakili timamu kweli wewe? Mi sikuelewi. Unatoa judgement utadhani ulikuwepo kwenye kikao hicho huko Arusha. Nilikuonya usiwe mnazi uwe na fact na tumia busara unapochangia kitu humu jamvini.Your so foolish. Kijijini kwetu yaya ni kibarua wa kulea watoto.
   
 10. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakirudia naomba tushikamane tutangaze uasi dhidi ya hao mapolisi,kwanza ni wachache hawawezi kutuzidi,pili wanaishi wengi uraiani hivo tuna uwezo wa kusort mmojammoja,tuweke woga pembeni tupambane na hawa vibaraka wasiojua sheria
   
 11. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  HIVI HUYU YAYA ANAKAA WAPI MAANA NINGEMFAHAMU NINGEMZABA VIBAO VYA NGUVU SANA! Hivi yule Mgombea wa ubunge kule Maswa alivyo mpiga mtama mkuu wa Polisi bila kuchukuliwa hatua! Alikuwa juu ya sheria au kwakuwa yeye CCM??
   
 12. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  yaya
   
 13. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wewe una ubongo kweli, au ndio pesa za mafisadi bado zinakusumbua. Unamaanisha nini unaposema mbunge ndio kaleta vurugu wakati CCM hadi wameazima mbunge kutoka tanga kupiga kura ya kumchagua meya jiji la arusha.

  Acha uzembe fikiria vizuri na usiropoke. Siamini kama CCM mnaodhani mnadumisha amani ya nchi hii mnafanya mambo kama hayo na kuwadanganya waTZ eti nyie ndio waasisi wa amani iliyoko inchin
  i.
   
 14. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hiyo ndio dawa ya wafanya fujo, next time atakuwa na akili sawasawa na kujua nchi hii ina dola
   
 15. P

  Proud Patriot JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 220
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  punguani, NA YULE WA CCM ALIYEMPIGA MTAMA MKUU WA POLISI? jipange zezeta we
   
 16. e

  emma 26 Senior Member

  #16
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  polisi ipo kwajili kulinda amani haijalishi hiyo amani ilikuwa inavunjwa kwa namna gani, sidhani kama huyo mbunge alikuwa akidumisha amani na sidhani kama angekuja kisitalabu angepigwa na polis! Kwanini yeye tu apigwe ananini?
   
 17. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Alaa!! Kwa hiyo nyinyi wabunge wa upinzani mnawaona kama majambazi sivyo???? I think you must be under influence of alcohol or something!!...
   
 18. K

  KIBE JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana jf msameheneni tu huyu anayejiita yaya nafikiri elimu kama anayo basi haijamsaidia katika maisha yake hasa katika kufikiri na kutafsiri mambo. Hawa ndo wale wa udom elimu bila vitendooo sawa sawa na 00000000000!!!!!!!!
   
 19. Offline User

  Offline User JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 3,769
  Likes Received: 1,462
  Trophy Points: 280
  unatumia kamasi siyo akili hiyo
   
Loading...