Masanilo
Platinum Member
- Oct 2, 2007
- 22,286
- 4,493
Wana JF kuna habari katika gazeti la habari leo linalosema kuwa serikali ya JK imevunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato mwezi Dec, 2010 kwa kukusanya 587bill kati ya malengo ya 570bill na huku ikionyesha kuwa saizi serikali ina akiba ya dola 3.8bill, kiwango hiki ni kikubwa kuliko nchi zote za Afrika Mashariki kwa sasa.
Hoja yangu iko hapa, kama ni kweli basi serikali ya JK inahitaji pongezi kwa kazi nzuri iliyofanya lakini inahitaji kuthamini hasa mfumuko wa bei ambao kwa kiasi kikubwa umesababishwa na kushuka kwa thamani ya Tshs ambayo imesababisha uagizaji wa bidhaa kutoka nje kuwa ghali zaidi hususani mafuta ambayo yanamekuwa yakipanda kila kukicha.
Athari ya kupanda kwa mafuta kutokana na kushuka kwa Tshs kuna dirct impact kwenye ongezeko la bei ambalo ndilo kilio cha wananchi wengi kwa sasa.
Hakuna haja ya kujisifu kwenye makaratasi wakati hali halisi ni mbaya.
Source: HabariLeo | BoT yavunja rekodi akiba ya dola na HabariLeo | TRA yavunja rekodi,yakusanya bil. 580/-.
Nawakilisha kwa mjadala zaidi.
Gazeti la habari leo! Mhhhhh siamini