Serikali yavunja rekodi ya ukusanyaji mapato na akiba ya dola! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yavunja rekodi ya ukusanyaji mapato na akiba ya dola!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee wa Rula, Feb 4, 2011.

 1. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wana JF kuna habari katika gazeti la habari leo linalosema kuwa serikali ya JK imevunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato mwezi Dec, 2010 kwa kukusanya 587bill kati ya malengo ya 570bill na huku ikionyesha kuwa saizi serikali ina akiba ya dola 3.8bill, kiwango hiki ni kikubwa kuliko nchi zote za Afrika Mashariki kwa sasa.
  Hoja yangu iko hapa, kama ni kweli basi serikali ya JK inahitaji pongezi kwa kazi nzuri iliyofanya lakini inahitaji kuthamini hasa mfumuko wa bei ambao kwa kiasi kikubwa umesababishwa na kushuka kwa thamani ya Tshs ambayo imesababisha uagizaji wa bidhaa kutoka nje kuwa ghali zaidi hususani mafuta ambayo yanamekuwa yakipanda kila kukicha.
  Athari ya kupanda kwa mafuta kutokana na kushuka kwa Tshs kuna dirct impact kwenye ongezeko la bei ambalo ndilo kilio cha wananchi wengi kwa sasa.
  Hakuna haja ya kujisifu kwenye makaratasi wakati hali halisi ni mbaya.
  Source: HabariLeo | BoT yavunja rekodi akiba ya dola na HabariLeo | TRA yavunja rekodi,yakusanya bil. 580/-.
  Nawakilisha kwa mjadala zaidi.
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,848
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Watakusanya toka mifuko ya nani? waongo wale tunao jamaa zetu TRA wanasema wafanya biashara wakubwa hawataki kulipa kodi kisa walitoa pesa nyingi wakati wa kampeni za CCM .Kwa sasa wako na TAX HOLIDAY kwa muda kadhaa ndiyo maana serikali imechacha kifedha.Kama ni kweli iweje wakate posho za nyumba kwa askari polisi na magereza huku wakiziacha za jeshi la wananchi.Subirini muda si mrefu askari polisi wataungana na nguvu ya umma kudai haki
   
 3. D

  Dunder Member

  #3
  Feb 4, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee wa Rula naelewa hoja yako juu ya inflation. Lakini ninamashaka na hawa jamaa wa Habari Leo maana inawezekana kabisa wanatumika kueneza propaganda zisizo na tija kwa taifa letu. Ukizingatia Umeme wetu ni wa mawazo na hii imepelekea production kushuka mno ikiwa na maana hata mapato yameshuka kwa maana ya wazalishaji na ambao ni kati ya walipaji wazuri wa kodi, sasa sidhani kama wanaweza kubreak through kwa staili hii!
   
 4. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli this is an achievement that deserves to be lauded. tatizo letu sisi ni kwamba mara zote tunakuwa critical na kusahau au kupuuza mengi tu yanayofanywa na Serikali yetu.
   
 5. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Does it have any direct impact to a normal Tanzanian who lives in Tandaimba etc? Ok record imevunjwa ya kukusanya kodi SO WHAT Mtanzania anafaidika vipi? Mapato juu lakini pia sukari petrol viko juu.
   
 6. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Unataka na sisi tunaokula mlo mmoja kwa siku pia tu ji proud? Huko kuvunja record kunatusaidia nini wakati hatuwezi kununua hata sukari?
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  usanii wa kwenye pool table ukiingizwa kwenye masuala ya kitaifa ni hatari sana. Huwa siamini kama kweli Habari leo linamilikiwa na serikali maana habari zake maranyi ni either uongo, fitina, majungu au udaku.

  Ni kigazeti cha udaku cha serikali. Sasa hapo ndiyo wanam-promote Kikwete baada ya kuona mambo yameanza kuharibika?
  They are very late.
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  sasa kwa nini serikali inashindwa kulipa mishahara? Kwa nini walikwapua posho za polisi? Kwa nini huduma haziboreki? kwa nini...
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,860
  Trophy Points: 280
  Mbona husemi kuvunja rekodi ya matumizi EA?
   
 10. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #10
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Wajinga ndo waliwao. Hakuna rekodi yeyote. Fedha inashuka thamani kwa kasi ya ajabu. Kama wangekuwa na dola kiasi hicho kuna haja gani basi ya kuhitaji fedha zaidi za nje? Mtu anayekuheshimu akikwambia kitu cha kipumbavu halafu ukakubali, anakudhara!
  Wanaweza kusema wamekusanya kodi nyingi kumbe wameprint hela nyingi. Si tunawajua, wamekaa kiasara asara tu. Hana jema wanalofikiri kwa ajili ya nchi yao bali kwa ajili ya matumbo yao tu.
  Sukari leo inauzwa shilingi 2000 kwa kilo, mchele 1500, viazi mafuta ya kula 3500. halafu wanatuambia wana dola za kutosha, na wathibitishe.
   
 11. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #11
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nadhani la muhimu ni kujua kuwa hizi fedha zinakusanywa zinatumika kufanyia nini kwa manufaa ya wananchi .....Hapa ndio serikali inafeli. Juzi juzu tu nimeasikia kuna mpango wa kuwajengea wabungue nyumba ingawa watatumia fedha za NHC lakini eventually serikali italipa kupitia makusanyo ya kodi.

  Kama wanakusanya mabilioni yote hayo kwa mwezi (TShs .570bill ) wakati Mwinyi alikuwa anakusanya TShs 25bi,l halafu hatuoni mabadiliko si kwenye huduma za afya, elimu, etc ...then kuna tatizo. Serikali kama wanajali inabidi kujitathmini. Au ndio makusanyo makubwa lakini na ufisadi umeongezeka by same percentage kama ugunduzi wa karibuni wa Magufuli kuhusu zaidi wa TShs 5bil walizotaka kujichotea kutokana watumishi wa manispaa kupitia mlango wa fidia za waathirika wa upanuzi wa barabara?
   
 12. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Swali mimi nilijiuliza kwa nini data hizi zitoke katika kipindi hiki ambapo tunaambiwa serikali ina hali mbaya kifedha na hilo lina shabihiana na hali halisi ilivyo mtaani.
   
 13. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #13
  Feb 4, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  anafaidika bwana si ndo tunalipa DOWANS NA lazima tulipe!
   
 14. A

  Anaruditena Member

  #14
  Feb 4, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiyo record kwenye mifuko ya mafisadi - ukweli unafahamika serikali hiko hoi tabani
   
 15. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #15
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sina source mkuu juu ya sentensi yako ya juu.
   
 16. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #16
  Feb 4, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mkuu pesa yooote hiyo inakwenda wapi sasa!?? siyo kuwa tunapuuza ila tunataka matokeo yake!
  Unajua kama vitu ni vizuri vinaonekana na kila mtu mkuu sasa mbona hatuoni mpaka tuambiwe!
   
 17. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hilo nalo neno. mimi najua njia mojawapo na kudeal na kushuka kwa thamani ya fedha yetu ni serikali kuingilia kati, sasa mbona ipo kimya wakati Tshs yetu kushuka kwake ndiyo songombingo linapoanzia. Hapo tu ndipo ninaposhangaa, tibu kwanza tatizo kwenye shina matawi yatanawiri tu.
   
 18. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #18
  Feb 4, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  upuuzi mtupu hakuna kitu km hicho, hazina yenyewe imekauka mishahara wafanyakazi wanakopwa na kukatwa posho zao. kuna cheki ya mzee wangu ipo hazina toka mwaka jana mwezi wa kumi tunaambiwa pesa hakuna tusubiri januari, januari nimeenda yule jamaa ananiambia hali ni mbaya mnoooo hajui lini pesa itapatikana. sasa leo eti dola imekusanywa kuvuka kiwango duuuu. ma propaganda ya KIZAMAANI ENZI ZA NCHI ZA KIKOMUNISTI.
   
 19. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #19
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nadhani kwa sababu polisi na Magereza hawamiliki vifaru na ndege na silaha nzito nzito za kivita ndiyo maana wakakwenyua posho zao kwa kisingizio cha computer kama ilivyo ada yao hata kwenye uchaguzi si walisema system ipo down kujumlisha matokeo ya Ubungo!
   
 20. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #20
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Mie huwa nasema watu humu JF sio great thinkers at all, ni Great Tanker. Kwa mujibu wa Takwimu za TRA mapato mengi hukusanywa mwezi March, June, Sept. na Dec. Hili linatokana na makampuni mengi kulipa zile ‘ Quarterly Provisional Tax’ kutokana na sheria ya kodi Income Tax Act No. 11 ya 2004. Kwa hiyo ni kweli kabisa hizo pesa zimekusanywa na mfanye tafiti sio kujibu humu kibubusa tu
   
Loading...