huu ni ujumbe au mchango wangu kwa Sirikali
Naomba waziri na Serekali ya Tanzania waelewe , sio kwamba watu wanapinga huo mswada, bali timining yake ndio mbaya, kwa sababu wameua shirika la TANESCO kwa maksudi nna baadhi ya watu kujipatia mitaji/mtaji wa kuwekezea kwenye umeme nk halafu watu hao hao wanakuja na mswada wa umeme.Kwa maana nyingine mswada huu unakuwa kama si endelevu , au competitive , kwa sababu mwekezaji moja kashikiliwa chini, i.e kafilisiwa na wakati mwekezaji mwingine anawezeshwa anafungliwa njia. Na anaye fanya hivyo ni mtu huyo huyo, i.e aliye mnyonga mwingine ndio anapata nafasi ya kuwekeza iwe directly or indirectly.
hivyo ni vizuri tuka shughulikia matatizo ya huyu ndugu yetu TANESCO na sababu zilizo mfikisha hapo kabla ya kwenda hatua nyingine.
Hivyo ni juu ya serekali kuharakisha mapitio ya mikataba mibovu iwe ya Tanesco au ya madini kabla hatujapelekana Mbele, kama wanaona kuna umuhimu wa kupitisha huu mswada huu wa Sasa.
Ya Chni ni maelezo ya Sirikali
Serikali yautetea Muswada wa sheria ya Umeme
*Yadai hauna harufu ya rushwa
Na Kizitto Noya
WIZARA ya Nishati na Madini imemsafisha aliyekuwa waziri wake Nazir Karamagi na kusema, hakuna msukumo wowote wa kifisadi katika kutengeneza muswada wa Sheria Mpya ya Umeme na Mafuta ya Petroli unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni mwezi ujao.
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa fikra zilizojengeka kwamba kuna ujanja katika kutengeneza muswada huo hazina mantiki wala ukweli wowote.
"Wazo kwamba kuna kitu 'nyuma ya pazia' katika kutengeneza muswada huo ni potofu. Napenda kuueleza umma na ndugu zangu (waandishi) mnisaidie kwamba sio kweli, wizara inafanya hivyo kwa maslahi ya Taifa, kusiwe na wazo kwamba msukumo huo wa muswada wa Sheria mpya ya Umeme una maslahi kwa mtu," alisema Ngeleja.
Kauli ya Ngeleja imekuja juma moja tangu wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waukatae tena muswada huo wenye lengo la kufungua milango kwa wawekezaji wa nje kuwekeza katika sekta ya umeme wakidai kuwa bado una harufu ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi.
Ngeleja aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa kukataliwa kwa muswada huo kwa sababu yoyote ile, hakutaondoa umuhimu wa kuifanyia marekebisho sheria ya umeme ya mwaka 1931 ambayo kulingana na mabadiliko ya kijamii, imepitwa na wakati.
"Sheria hii ya Umeme ilitungwa mwaka 1931 na ina upungufu mwingi, ni lazima ifanyiwe marekebisho ili iende na wakati,"alisisitiza Ngeleja na kuendelea:
"Hoja kwamba sekta binafsi kwenye umeme itakwamisha mpango wa serikali kupeleka nishati hiyo vijijini siyo kweli kwani hata Tanesco haiwajibiki kupeleka umeme vijijini,"
Alisema hoja hiyo imepitwa na wakati kwani hata Tanesco haiwajibiki kupeleka umeme vijijini bali Serikali kupitia Wakala wa Umeme vijijini (REA) katika mkataba ulioingiwa mwaka 2005.
"Tutunge sheria hii au tusitunge, Tanesco siyo suluhu la tatizo la umeme vijijini, kazi hiyo ni ya serikali kupitia Wakala wa Kusambaza Umeme (REA) tangu mwaka 2005," alisema.
Alisema katika muswada huo wa sheria hiyo mpya, serikali imejitahidi kukwepa kubinafsisha huduma ya umeme kwenye maeneo yanayoweza kuliathiri taifa kama ubinafsishaji wa miundombinu yake.
Alieleza kuwa katika sheria hiyo mpya serikali iliruhusu uwekezaji katika uzalishaji na usambazaji wa umeme maeneo ambayo tayari yamekuwa yakiendeshwa na kampuni za nje.
"Sisi tunaruhusu soko huria katika uzalishaji na usambazaji na siyo usafirishaji na hili sio jambo geni kwani hata sasa maeneo haya tayari yako huru kwa wawekezaji,"alisema.
Hata hivyo alibainisha kuwa kauli za wabunge hao kuhusu muswada huo hazikutolewa ili kuukubali wala kuukwamisha bali ni mapendekezo yatakayotumika kuuboresha zaidi kabla haujaingia bungeni.
"Kukataliwa kwa Muswada huo ni changamoto kwa serikali katika kuuboresha zaidi kwani hayo ni mapendekezo tu na sio msimamo wa mwisho wa wabunge," alisema.
Wabunge hao walionyesha kukerwa na muswada huo katika mjadala uliofanyika Machi 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam kuhusiana na mapendekezo ya serikali kutunga sheria mpya ya umeme itakayoruhusu uwekezaji katika sekta hiyo.
Wabunge hao walisema hawajaona tofauti yoyote katika muswada huo na uliowasilishwa mara ya kwanza ambao ulipitiwa na kutolewa mapendekezo ya mabadiliko katika baadhi ya vipengele. chini ya aliyekuwa na waziri wa wizara hiyo, Nazir Karamagi
Walisema muswada huo pia hauonyeshi mpango wowote wa kuweka umeme maeneo ya vijijini ambako ndio kuna wananchi wengi.
Mbunge wa Karatu Dk Willibrod Slaa alitoa angalizo kuwa kwa sasa hakuna kampuni yoyote ya uwekezaji inayoweza kupeleka umeme vijijini na kuitaka serikali kuhakikisha inatekeleza jukumu hilo yenyewe na kuongeza kuwa kuukubali mswada huo ni sawa na kuiweka nchi mikononi mwa wawekezaji.