Serikali yatoa vigezo vya kupandisha vyeo na mishahara watumishi wa umma

Awamu hii siipatii majibu! yaani kila siku yanakuja mengine. Kwani siku zote si vigezo hivyo vinatumika kupandisha watumishi vyeo? da! kazi ipo!
 
Na maneno yanayowasononesha watumishi hasa walimu kwa sababu angeambiwa athibitishe kuwa huyu mwalimu ambaye hajapandishwa daraja hawajibiki ipasavyo, sidhani kama angethibitisha. Pengine ametoa majibu ya jumla yasiyojitosheleza.
 
Hawaaminiki vp mikopo mlibadili gia angani maana sheria inaanzia pale inapopitishwa ila kwetu ikarudi nyuma Kibabe na kwavile vyombo vya haki WANAOGOPA KUNYIMWA MISHAHARA AU WASIPANDE VYEO AU WAKIJIPENDEKEZA WAWE MAJAJI kwa wenzetu wangekwenda mahakani mfano Trump suala la uhamiaji
Hili limeumiza wengi aisee hasa ile riba ati tumechelewa kulipa. Ila basi tumeshaumia.
 
serikali aina ela wala senti ya kuongeza mishahara na wala msilitegemee kwa sasa,poleni sana watumishi wa uma

Ati wasema serikali aina ela wala senti ya kuongeza mishahara lakini ukweli ni kwamba serikali haina hela ya kuongeza mishahara ya wazembe na walevi. Nyakati za SU (Sina Uchungu) na ST (Sitaki Shida) fanya utakavyo ni mali ya umma[/B] zimepitwa na hapa kazitu.

Tujifariji mitandaoni kwa kauli za kejeli na lawama, lakini mwisho wa siku mhusika ama anapandishwa daraja na mshahara au la.

KUPANGA NI KUCHAGUA
 
nawackitikia sana wanaotafta ajra wangeyajua haya wacngsubutu kuomba bora ujiajiri mwnywe
Kama mwombaji ajira anategemea kupanda cheo na kupandishwa mshahara pasipo kuwajibika, awamu hii atafute kazi kwingine na siyo serikalini na taasisi zake.
 
Mtumishi mvivu, mzembe na mlevi unabaki naye tu ili usimpandishe cheo si umfukuze kama unaushahidi??

Adhabu kwa mfanyakazi ni pamoja na onyo, ikiwemo kukatwa mshahara, kuteremshwa cheo, kutokupandishwa mshahara au cheo. Inaposhindikana anafukuzwa kazi.
 
Naiona rushwa ya fedha na ngono,ubabe kazini na miungu kazi vikitamalaki sehemu za kazi

Serikali ijiandae na changamoto hizo
 
Hatimae serikali imetoa vigezo vinavyotakiwa kutumika kama vipaumbele wakati wa kuwapandisha watumishi wa umma mshahara hivyo walevi, wavivu, wasio na nidhamu na uadilifu kutopandishwa

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk Laurean Ndumbaro ndiye aliyetangaza vigezo hivyo vinavyopaswa kutumiwa na waajiri katika utumishi wa umma kuwapandisha watumishi mishahara.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Ndumbaro, suala la upandishwaji vyeo kwa watumishi wa umma litazingatia zaidi utendaji kazi wa mtumishi husika na si suala la sifa ya Muundo wa Utumishi (Scheme of Service) pekee kwa maana ya muda wa kutumikia miaka mitatu mitatu kama wengi wanavyodhani.

Aliyasema hayo kwa wakati tofauti katika Halmashauri za Wilaya ya Nyasa, Namtumbo na Manispaa ya Songea katika ziara yake ya kikazi ya siku tano ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma.

Katibu Mkuu Ndumbaro alisisitiza kuwa mtumishi wa umma anayewajibika vizuri katika utendaji kazi wake wa kila siku ndiye atakayepandishwa cheo na si vinginevyo. Alilazimika kutoka ufafanuzi huo, kufuatia baadhi
ya watumishi katika halmashauri hizo kulalamika kutopandishwa madaraja (vyeo) kwa wakati kwa muda mrefu sasa wakati wenzao walioanza nao kazi wameshapandishwa vyeo, hivyo kusababisha uwepo wa tofauti kubwa ya mishahara baina yao.

“Haiwezekani Serikali ikapandisha mishahara kwa watumishi wasiowajibika, walevi na wasio na nidhamu na uadilifu katika utendaji wao wa kazi, atakayewajibika katika utendaji wake ndiye atakayepandishwa ngazi ya mshahara,” alisisitiza.

Katibu Mkuu huyo aliainisha kuwa, malalamiko mengi ni ya walimu ambao wamekuwa wakidhani kuwa kila baada ya miaka mitatu lazima wote wapandishwe vyeo (madaraja) hata kama hawajawajibika ipasavyo, suala ambalo si sahihi.

“Haiwezekani Mwalimu anayefundisha vizuri darasani na wanafunzi wake wanafaulu vizuri masomo yake akapandishwa daraja sawasawa na yule ambaye ufundishaji wake hauridhishi na ni mlevi wa kupindukia hali inayochangia wanafunzi wengi kutofaulu somo lake.”

Aidha alisema hivi karibuni, ofisi yake inatarajia kukutana na Tume ya Utumishi wa Walimu na kuzungumza na Walimu ili kutoa elimu na ufafanuzi yakinifu wa vigezo vya msingi vinavyozingatiwa katika suala la upandishaji vyeo kwa watumishi wa umma nchini kwa lengo la kuepukana na malalamiko yasiyo ya lazima.

Habari Leo
Hayo ayasemayo huyo katibu ni sheria zake na sio za serikali tena kuna roho mbaya ndani yake
 
Awamu hii siipatii majibu! yaani kila siku yanakuja mengine. Kwani siku zote si vigezo hivyo vinatumika kupandisha watumishi vyeo? da! kazi ipo!

Ukweli ni kwamba huu Utawala ni wa vichaa na malimbukeni wa madaraka....!!!!!
Ni shida sana lakini Mungu anawaona hawa wendawazimu.......!!!
 
Katibu Mkuu Ndumbaro alisisitiza kuwa mtumishi wa umma anayewajibika vizuri katika utendaji kazi wake wa kila siku ndiye atakayepandishwa cheo na si vinginevyo. Alilazimika kutoka ufafanuzi huo, kufuatia baadhi
ya watumishi katika halmashauri hizo kulalamika kutopandishwa madaraja (vyeo) kwa wakati kwa muda mrefu sasa wakati wenzao walioanza nao kazi wameshapandishwa vyeo, hivyo kusababisha uwepo wa tofauti kubwa ya mishahara baina yao.

Mtumishi hapelekewi vitendea kazi halafu unasema hafanyi kazio unategemea nini?
Huu ni upuuzi mtupu
 
Kwahiyo wanataka kumaanisha kwamba watumishi wote hawapati increment kwasababu ya uvivu na kukosa nidhamu kazini?

Poor Africa
 
Hakuna jipya hapo,hata zamani ilikuwa ni hvyo hvyo hata kama kigezo cha miaka 3 kimefikwa,vitu vngine vilikuwa vinaangaliwa pia
 
Hivi kwa watumishi wa zamani waliokwisha thibitishwa kazini miaka kadhaa nyuma moja ya vigezo vya kupanda kwao cheo ni kuhudumu kwenye cheo hicho cha sasa kwa miaka mitatu au minne?
 
Kumbe zamani wavivu na walevi walipandishwa vyeo?? Ni vyema kwanza ukaanza uhakiki kwa hao wenye vyeo...
 
Hivi kwa watumishi wa zamani waliokwisha thibitishwa kazini miaka kadhaa nyuma moja ya vigezo vya kupanda kwao cheo ni kuhudumu kwenye cheo hicho cha sasa kwa miaka mitatu au minne?

Wamejifanya kuongeza kipengere cha miaka minne ili kubuy time,na ikifikia hiyo miaka minne bado usumbhfu upo pale pale,jamaa wanatapa tapa sana mkuu
 
Hatimae serikali imetoa vigezo vinavyotakiwa kutumika kama vipaumbele wakati wa kuwapandisha watumishi wa umma mshahara hivyo walevi, wavivu, wasio na nidhamu na uadilifu kutopandishwa

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk Laurean Ndumbaro ndiye aliyetangaza vigezo hivyo vinavyopaswa kutumiwa na waajiri katika utumishi wa umma kuwapandisha watumishi mishahara.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Ndumbaro, suala la upandishwaji vyeo kwa watumishi wa umma litazingatia zaidi utendaji kazi wa mtumishi husika na si suala la sifa ya Muundo wa Utumishi (Scheme of Service) pekee kwa maana ya muda wa kutumikia miaka mitatu mitatu kama wengi wanavyodhani.

Aliyasema hayo kwa wakati tofauti katika Halmashauri za Wilaya ya Nyasa, Namtumbo na Manispaa ya Songea katika ziara yake ya kikazi ya siku tano ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma.

Katibu Mkuu Ndumbaro alisisitiza kuwa mtumishi wa umma anayewajibika vizuri katika utendaji kazi wake wa kila siku ndiye atakayepandishwa cheo na si vinginevyo. Alilazimika kutoka ufafanuzi huo, kufuatia baadhi
ya watumishi katika halmashauri hizo kulalamika kutopandishwa madaraja (vyeo) kwa wakati kwa muda mrefu sasa wakati wenzao walioanza nao kazi wameshapandishwa vyeo, hivyo kusababisha uwepo wa tofauti kubwa ya mishahara baina yao.

“Haiwezekani Serikali ikapandisha mishahara kwa watumishi wasiowajibika, walevi na wasio na nidhamu na uadilifu katika utendaji wao wa kazi, atakayewajibika katika utendaji wake ndiye atakayepandishwa ngazi ya mshahara,” alisisitiza.

Katibu Mkuu huyo aliainisha kuwa, malalamiko mengi ni ya walimu ambao wamekuwa wakidhani kuwa kila baada ya miaka mitatu lazima wote wapandishwe vyeo (madaraja) hata kama hawajawajibika ipasavyo, suala ambalo si sahihi.

“Haiwezekani Mwalimu anayefundisha vizuri darasani na wanafunzi wake wanafaulu vizuri masomo yake akapandishwa daraja sawasawa na yule ambaye ufundishaji wake hauridhishi na ni mlevi wa kupindukia hali inayochangia wanafunzi wengi kutofaulu somo lake.”

Aidha alisema hivi karibuni, ofisi yake inatarajia kukutana na Tume ya Utumishi wa Walimu na kuzungumza na Walimu ili kutoa elimu na ufafanuzi yakinifu wa vigezo vya msingi vinavyozingatiwa katika suala la upandishaji vyeo kwa watumishi wa umma nchini kwa lengo la kuepukana na malalamiko yasiyo ya lazima.

Habari Leo
[/QUOTE
hebu tujikumbushe baadhi ya kauli kutoka serikalini
;tunasubiri uhakiki ili tuwaongeze mishahara,
;serikali itapandisha mishahah kulingananahali na uchumi,
;kipaumbele ni kununua ndege kwanza na standard gauge ikilipa vizuri tutaongeza mishahara
SIKU YA KUFA NYANI MITI YOTE HUTELEZA
 
Wamejifanya kuongeza kipengere cha miaka minne ili kubuy time,na ikifikia hiyo miaka minne bado usumbhfu upo pale pale,jamaa wanatapa tapa sana mkuu
Na suala la kuwa kama Mtumishi alikuwa masomoni hata kwa ruhusa rasmi miaka yake ya masomo haitahesabiwa ndani ya kazi je ni kweli Mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo haihesabiwi mkuu,itaanza kuhesabiwa baada ya kumaliza chuo,yaani ni shida,kila sehemu ni kubanwa tu wakati wao wananunua bombadia bila bunge kupitisha na hasi leo hoja ya CAG ya 1.5T bado haijajibiwa
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom