pilipili kichaa
JF-Expert Member
- Sep 3, 2013
- 17,628
- 13,690
Awamu hii siipatii majibu! yaani kila siku yanakuja mengine. Kwani siku zote si vigezo hivyo vinatumika kupandisha watumishi vyeo? da! kazi ipo!
Hili limeumiza wengi aisee hasa ile riba ati tumechelewa kulipa. Ila basi tumeshaumia.Hawaaminiki vp mikopo mlibadili gia angani maana sheria inaanzia pale inapopitishwa ila kwetu ikarudi nyuma Kibabe na kwavile vyombo vya haki WANAOGOPA KUNYIMWA MISHAHARA AU WASIPANDE VYEO AU WAKIJIPENDEKEZA WAWE MAJAJI kwa wenzetu wangekwenda mahakani mfano Trump suala la uhamiaji
serikali aina ela wala senti ya kuongeza mishahara na wala msilitegemee kwa sasa,poleni sana watumishi wa uma
Kama mwombaji ajira anategemea kupanda cheo na kupandishwa mshahara pasipo kuwajibika, awamu hii atafute kazi kwingine na siyo serikalini na taasisi zake.nawackitikia sana wanaotafta ajra wangeyajua haya wacngsubutu kuomba bora ujiajiri mwnywe
Mtumishi mvivu, mzembe na mlevi unabaki naye tu ili usimpandishe cheo si umfukuze kama unaushahidi??
Tar 15 utasikia siongezi mshahara ikifika tar 2/12 utasikia mwakani tutaongezaSarakasi zinaanza taratibu,ifika tarehe 15 yasemwa makubwa
Hayo ayasemayo huyo katibu ni sheria zake na sio za serikali tena kuna roho mbaya ndani yake
Hatimae serikali imetoa vigezo vinavyotakiwa kutumika kama vipaumbele wakati wa kuwapandisha watumishi wa umma mshahara hivyo walevi, wavivu, wasio na nidhamu na uadilifu kutopandishwa
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk Laurean Ndumbaro ndiye aliyetangaza vigezo hivyo vinavyopaswa kutumiwa na waajiri katika utumishi wa umma kuwapandisha watumishi mishahara.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Ndumbaro, suala la upandishwaji vyeo kwa watumishi wa umma litazingatia zaidi utendaji kazi wa mtumishi husika na si suala la sifa ya Muundo wa Utumishi (Scheme of Service) pekee kwa maana ya muda wa kutumikia miaka mitatu mitatu kama wengi wanavyodhani.
Aliyasema hayo kwa wakati tofauti katika Halmashauri za Wilaya ya Nyasa, Namtumbo na Manispaa ya Songea katika ziara yake ya kikazi ya siku tano ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma.
Katibu Mkuu Ndumbaro alisisitiza kuwa mtumishi wa umma anayewajibika vizuri katika utendaji kazi wake wa kila siku ndiye atakayepandishwa cheo na si vinginevyo. Alilazimika kutoka ufafanuzi huo, kufuatia baadhi
ya watumishi katika halmashauri hizo kulalamika kutopandishwa madaraja (vyeo) kwa wakati kwa muda mrefu sasa wakati wenzao walioanza nao kazi wameshapandishwa vyeo, hivyo kusababisha uwepo wa tofauti kubwa ya mishahara baina yao.
“Haiwezekani Serikali ikapandisha mishahara kwa watumishi wasiowajibika, walevi na wasio na nidhamu na uadilifu katika utendaji wao wa kazi, atakayewajibika katika utendaji wake ndiye atakayepandishwa ngazi ya mshahara,” alisisitiza.
Katibu Mkuu huyo aliainisha kuwa, malalamiko mengi ni ya walimu ambao wamekuwa wakidhani kuwa kila baada ya miaka mitatu lazima wote wapandishwe vyeo (madaraja) hata kama hawajawajibika ipasavyo, suala ambalo si sahihi.
“Haiwezekani Mwalimu anayefundisha vizuri darasani na wanafunzi wake wanafaulu vizuri masomo yake akapandishwa daraja sawasawa na yule ambaye ufundishaji wake hauridhishi na ni mlevi wa kupindukia hali inayochangia wanafunzi wengi kutofaulu somo lake.”
Aidha alisema hivi karibuni, ofisi yake inatarajia kukutana na Tume ya Utumishi wa Walimu na kuzungumza na Walimu ili kutoa elimu na ufafanuzi yakinifu wa vigezo vya msingi vinavyozingatiwa katika suala la upandishaji vyeo kwa watumishi wa umma nchini kwa lengo la kuepukana na malalamiko yasiyo ya lazima.
Habari Leo
Awamu hii siipatii majibu! yaani kila siku yanakuja mengine. Kwani siku zote si vigezo hivyo vinatumika kupandisha watumishi vyeo? da! kazi ipo!
Katibu Mkuu Ndumbaro alisisitiza kuwa mtumishi wa umma anayewajibika vizuri katika utendaji kazi wake wa kila siku ndiye atakayepandishwa cheo na si vinginevyo. Alilazimika kutoka ufafanuzi huo, kufuatia baadhi
ya watumishi katika halmashauri hizo kulalamika kutopandishwa madaraja (vyeo) kwa wakati kwa muda mrefu sasa wakati wenzao walioanza nao kazi wameshapandishwa vyeo, hivyo kusababisha uwepo wa tofauti kubwa ya mishahara baina yao.
Hivi kwa watumishi wa zamani waliokwisha thibitishwa kazini miaka kadhaa nyuma moja ya vigezo vya kupanda kwao cheo ni kuhudumu kwenye cheo hicho cha sasa kwa miaka mitatu au minne?Hakuna jipya hapo,hata zamani ilikuwa ni hvyo hvyo hata kama kigezo cha miaka 3 kimefikwa,vitu vngine vilikuwa vinaangaliwa pia
Hivi kwa watumishi wa zamani waliokwisha thibitishwa kazini miaka kadhaa nyuma moja ya vigezo vya kupanda kwao cheo ni kuhudumu kwenye cheo hicho cha sasa kwa miaka mitatu au minne?
Hatimae serikali imetoa vigezo vinavyotakiwa kutumika kama vipaumbele wakati wa kuwapandisha watumishi wa umma mshahara hivyo walevi, wavivu, wasio na nidhamu na uadilifu kutopandishwa
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk Laurean Ndumbaro ndiye aliyetangaza vigezo hivyo vinavyopaswa kutumiwa na waajiri katika utumishi wa umma kuwapandisha watumishi mishahara.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Ndumbaro, suala la upandishwaji vyeo kwa watumishi wa umma litazingatia zaidi utendaji kazi wa mtumishi husika na si suala la sifa ya Muundo wa Utumishi (Scheme of Service) pekee kwa maana ya muda wa kutumikia miaka mitatu mitatu kama wengi wanavyodhani.
Aliyasema hayo kwa wakati tofauti katika Halmashauri za Wilaya ya Nyasa, Namtumbo na Manispaa ya Songea katika ziara yake ya kikazi ya siku tano ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma.
Katibu Mkuu Ndumbaro alisisitiza kuwa mtumishi wa umma anayewajibika vizuri katika utendaji kazi wake wa kila siku ndiye atakayepandishwa cheo na si vinginevyo. Alilazimika kutoka ufafanuzi huo, kufuatia baadhi
ya watumishi katika halmashauri hizo kulalamika kutopandishwa madaraja (vyeo) kwa wakati kwa muda mrefu sasa wakati wenzao walioanza nao kazi wameshapandishwa vyeo, hivyo kusababisha uwepo wa tofauti kubwa ya mishahara baina yao.
“Haiwezekani Serikali ikapandisha mishahara kwa watumishi wasiowajibika, walevi na wasio na nidhamu na uadilifu katika utendaji wao wa kazi, atakayewajibika katika utendaji wake ndiye atakayepandishwa ngazi ya mshahara,” alisisitiza.
Katibu Mkuu huyo aliainisha kuwa, malalamiko mengi ni ya walimu ambao wamekuwa wakidhani kuwa kila baada ya miaka mitatu lazima wote wapandishwe vyeo (madaraja) hata kama hawajawajibika ipasavyo, suala ambalo si sahihi.
“Haiwezekani Mwalimu anayefundisha vizuri darasani na wanafunzi wake wanafaulu vizuri masomo yake akapandishwa daraja sawasawa na yule ambaye ufundishaji wake hauridhishi na ni mlevi wa kupindukia hali inayochangia wanafunzi wengi kutofaulu somo lake.”
Aidha alisema hivi karibuni, ofisi yake inatarajia kukutana na Tume ya Utumishi wa Walimu na kuzungumza na Walimu ili kutoa elimu na ufafanuzi yakinifu wa vigezo vya msingi vinavyozingatiwa katika suala la upandishaji vyeo kwa watumishi wa umma nchini kwa lengo la kuepukana na malalamiko yasiyo ya lazima.
Habari Leo
[/QUOTE
hebu tujikumbushe baadhi ya kauli kutoka serikalini
;tunasubiri uhakiki ili tuwaongeze mishahara,
;serikali itapandisha mishahah kulingananahali na uchumi,
;kipaumbele ni kununua ndege kwanza na standard gauge ikilipa vizuri tutaongeza mishahara
SIKU YA KUFA NYANI MITI YOTE HUTELEZA
Na suala la kuwa kama Mtumishi alikuwa masomoni hata kwa ruhusa rasmi miaka yake ya masomo haitahesabiwa ndani ya kazi je ni kweli Mkuu?Wamejifanya kuongeza kipengere cha miaka minne ili kubuy time,na ikifikia hiyo miaka minne bado usumbhfu upo pale pale,jamaa wanatapa tapa sana mkuu
Na suala la kuwa kama Mtumishi alikuwa masomoni hata kwa ruhusa rasmi miaka yake ya masomo haitahesabiwa ndani ya kazi je ni kweli Mkuu?
Sent using Jamii Forums mobile app