Serikali yatoa vigezo vya kupandisha vyeo na mishahara watumishi wa umma

Siku moja nilishangaa sana baada ya kuona jamaa niliyesoma naye chuo mwaka mmoja, tukapangwa kazi kituo kimoja na kufundisha darasa moja ila masomo tofauti, amenizidi 190,000 ilihali mimi nimefaulisha somo langu kwa 90%.....Niliacha kabisa hiyo kazi na kupambana na Maisha yangu kivingine!

Leo namshukuru Mungu, nayamudu maisha yangu kwa ujasiriamali. Nahata niliowaajiri wanamzidi mshahara yule jamaa!!! Ukiona mambo hayaendi mlima huu, hamia mwingine...Milima haitaisha hadi Yesu arudi mara ya pili
 
****Siku moja nilishangaa sana baada ya kuona jamaa niliyesoma naye chuo mwaka mmoja, tukapangwa kazi kituo kimoja na kufundisha darasa moja ila masomo tofauti, amenizidi 190,000 ilihali mimi nimefaulisha somo langu kwa 90%.....Niliacha kabisa hiyo kazi na kupambana na Maisha yangu kivingine!

Leo namshukuru Mungu, nayamudu maisha yangu kwa ujasiriamali. Nahata niliowaajiri wanamzidi mshahara yule jamaa!!!

Ukiona mambo hayaendi mlima huu, hamia mwingine...Milima haitaisha hadi Yesu arudi mara ya pili***
Hizo zilikuwepo na labda bado zipo kuna Jamaa alikua amepandishwa madaraja kama matatu mbele yaani yeye bats tu na shangwe ila uhakiki ulivyoanza alifuatwa na Afisa mwajiri na baada ya hapo ile Hela anakatwa iliyokua imezidi .

Rushwa ilikua inaharibu pakubwa
 
Tuliambiwa mishahara ya November itakuwa mipya, sasa wanakuja na hizi habari ili watuambie kwamba bado wanafanya assessment ya walevi na wavivu, hili nalo litachukua mwaka mzima.
Kama uhakiki wa vyeti na watumishi hewa umechukua miaka miwili sembuse kutafuta walevi na wazembe!Nyongeza na madaraja tarajieni 2019/20!Muda huo mkiongezewa na mkipewa kazi ya kusimamia uchaguzi naamini wala hamtakumbuka mtakayokuwa mtendewa kati ya 2015/16-2018/19!
 
Mada mbili kuchanganywa pamoja na kuifanya ni mada moja ni kebehi kwa watumishi wa serikali.
Hivi kupandishwa madaraja ndiyo kunakosemwa kupandishwa kwa mishahara?
Mantiki ya kupandisha madaraja kwa baadhi ya watumushi wenye sifa stahiki,kunatafsiriwaje kama ni kupandisha mishahara ya watumishi wote wa umma?
 
Sina hakika, Mimi nigedhami, wawapandeshe wote waliostaili kupanda halafu huo mfumo ndio uanze
 
Swali la msingi ni je , mishahara wanayolipwa watumishi hao wa ngazi za chini inaendana na hali ya maisha?

Kuna tatizo kwenye suala zima la maslahi ya watumishi wa umma kuwa madogo sana ukilinganisha na gharama za maisha.
Watu wengine wanakua walevi kutokana na kukata tamaa ya kimaisha anapoangalia ugumu wa maisha na mshahara anaolipwa haviendani.

Mtu anatokea Ruvuma anapangiwa kazi Longido mshahara laki 350,000/-
Nyumbani kwao kuna wadogo zake wanasoma kila siku wazazi wanampigi simu mara matumizi ,mara ugonjwa ,mara msiba n.k. Akiangalia hata nauli ya kwenda Ruvuma na kurudi kazini hana. Wakati huo huo na yeye mwenyewe ana mahitaji yake muhmu kama kupanda nyumba,simu ,umeme,maji,kulipia king"amuzi ,nauli ya boda boda kwenda kazini mana jirani na ofisi hakuna nyumba ya nzuri ya kupanga.
Akiomba uhamisho ili arudi nyumbani au karibu na mazingira ya nyumbani ananyimwa.
Akienda kumopa benki kamashahara kake ni kadogo anaishia kupewa mil.4 na riba 21%. Pesa ambayo atairudisha kwa miaka 3 na haitoshi kujenga hata msingi wa nyumba bora.
Hali kama hiyo inawakumba wafanyakazi wengi sana sana. Matokeo yake wanaamua kuwa walevi na mara nyingine wanashindwa kuwajibika ipasavyo.

Kwa kweli wafanyakazi wa nchi za kiafrika wanafanya kazi kwenye mazingira magumu sana huku wanasiasa wakiendelea kuwanyanyasa na kuwakejeli kwenye majukwaa ya kisiasa bila wao kuangalia tofauti kubwa iliyopo kato ya mishahara ya wanasiasa na wafanyakazi.

Unakuta mwanasiasa darasa la saba lakini analipwa mshahara mkubwa kuliko mfanyakazi ambaye ni Daktari au Engineer.
 
Huo sio utaratibu mpya bali ndio utaratibu uliokuwepo. Mamlaka za nidham na maadili ndizo zenye jukumu lakupandisha vyeo sifa mojawapo ikiwa ni uadilifu
 
Mbona hamna jipya hapo, opras si zinajazwa tangu enzi zileee!!
Wanatafuta visingizio sio!! Time will tell.
 
Serikali iliyoshinwa kuongoza huanza kugombana na wananchi wake.Iposiku watasema watumishi Wa uma wenye vitambi hawastahili kuongezewa mshahara.
 
Wanatafuta namna ya kukimbia jukumu.
Term hii sheria na kanuni zimekanyagwa na bahati mbaya wenye nafasi ya kuwapazia sauti nao wapo chini ya uvungu

Watanzania,
Hii Serikali kila siku inaibuka na jipya..!!!Figisu zeshaanza.Ukisoma katikati ya mistari utagundua kwamba hawana nia ya dhati ya kupandisha mishahara watumishi wa umma..!!Yaani hapa panatengenezwa mazingira ya kuwanyima Watumishi haki yao ya msingi ya kupandishwa mishahara.

Hizi sheria zipo tangu miaka na miaka. Kama mtumishi ni mlevi, mvivu,mtoro,mwizi, fisadi n.k kwanini humchukulia hatua za kinidhamu???Ni mwajiri kichaa tu ndiye huwa anasubiri kuwalima watumishi wakti wa kuwa-recommend kupanda madaraja na mishahara kwa nia ya kuwakomoa au kwa vile hana fedha ya kulipa anatafuta visingizio...!.

Tunaomba Vyama vya Wafanyakazi chini ya TUCTA wakatae hizi sababu za kipuuzi za kutaka kuwanyima watumishi haki zao. Mbona PAYE wanakata kwa asilimia lukuki na Watumishi hawapigi kelele??
Hii awamu nafikri inaongozwa na viongozi walio chini ya laana.....!!!
 
Naimani hawa serikali hawana hela ya kupadisha/kuongeza mishahara. Hakuna mtumishi mlevi, mvivu. Kwanini wasifukuzwe kazi? Wanafanyaje kazi na mlevi? Sheria za utumishi wa umma unaeleza sifa za mtumishi na adhabu za walevi kazini. Ni kufukuza kazi. Waache siasa kwenye maslai ya watu. Wakiri hela hawana
 
Serikali ya drama kila siku. Hivi sii utakuwa wendawazimu kuiunga mkono serikali inayofanya mambo utazani tuko karnrne ya 19? Wakubali kuwa kila sekta wameshindwa ndani ya miaka hii miwili na mwelekeo ni kuwa hakuna matumaini kabisa ya hali kutengemaa kwa vile wenyewe wanaona (au wanatuaminisha) kuwa hali ni njema kabisa na kujisifu hadharani
 
Mfalme juha wananchi wake walikufa na njaa na tabu nyingi huku yeye akiwa na ratiba ya kutega na kutegua vitendawili kila Siku.
 
Back
Top Bottom