Serikali yatoa trilioni moja za kununua dawa

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939

AHADI ya serikali ya kuanza kusambaza dawa katika hospitali zote nchini kutokana na madai ya kuwepo kwa uhaba wa dawa za aina mbalimbali, imeanza kutekelezwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ziarani mkoani Arusha amesema Serikali imetoa Sh trilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa dawa na kuhakikisha pia madaktari 8,000 wanasambazwa kwenye hospitali mbalimbali za mikoa na wilaya ili kutatua changamoto za afya na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Katika hatua nyingine, Majaliwa amewataka watendaji wa Idara ya Uhamiaji kufanya misako kwenye nyumba za wageni na kudhibiti wageni wanaoingia kwenye mipaka mbalimbali nchini kutokana na kushamiri kwa wahamiaji haramu.

Aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa idara na taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na Wilaya ya Arusha.

Ukosefu wa dawa.
Akizungumzia upatikanaji wa dawa, Majaliwa alisema serikali imetoa Sh trilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa dawa za aina mbalimbali ili kuondoa upungufu wa dawa kwenye hospitali nchini.

Akieleza namna serikali ilivyo na nia ya dhati ya kumaliza tatizo la dawa nchini, Majaliwa alisema; “Awali tulitoa Sh bilioni 40 kwa ajili ya dawa na sasa tumeongeza fedha hadi kufikia shilingi trilioni moja.

“Tunataka kero ya upungufu wa dawa hospitalini iishe. Naagiza kila hospitali kuhakikisha inakuwa na dirisha la huduma za bure kwa wazee pamoja na duka la dawa,” alisema.

Chanzo: ITV
 
Tatizo ni kuongea bila kutenda....

Hivi mngenunua dawa kimya kimya watu wakazikuta hospital si wangekuja hapa kuwasifia wenyewe bila kujitangaza.......

Masikini majariwa naye kaambukizwa kuongea sana bila kutenda......
Ilisha tangazwa na upande wa pili kuwa dawa hakuna... ili isiendelee kueleweka hvyo... n jukumu lao kusema hvyo... vile vile n kwa faida yao kisiasa
 
Hizo hazipaswi kuwa ahadi hayo ni mambo yalazama serikali ifanye.

Sasa kama inakusanya kodi kwanini wasihakikishe dawa zinapatikana kwa wakati na ziwe zinatosha?

Nashangaa sana serikali inataka ionekane inachapa kazi wakati hayo mambo ndio wajibu wake kutimiza.....hakuna jipya hapo. Watu tutashangaa tu huku tunasema aaah hatimaye hawa jamaa wamekumbuka wanachotakiwa wafanye
 
Zilongwa mbali zitendwa mbali

Sasa kama hela ya dawa imepelekwa leo vipi wagonjwa wa juzi je walipaswa kuvumilia ugonjwa hadi hii leo ambapo serikali itanunua hizo dawa au zilitakiwa zipewe kipaumbele kwa kununuliwa kabla hata ya vitu vingine?
 
afadhali! tumechoka kupewa
IMG_20161203_203719.jpg
 
AHADI ya serikali ya kuanza kusambaza dawa katika hospitali zote nchini kutokana na madai ya kuwepo kwa uhaba wa dawa za aina mbalimbali, imeanza kutekelezwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ziarani mkoani Arusha amesema Serikali imetoa Sh trilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa dawa na kuhakikisha pia madaktari 8,000 wanasambazwa kwenye hospitali mbalimbali za mikoa na wilaya ili kutatua changamoto za afya na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Katika hatua nyingine, Majaliwa amewataka watendaji wa Idara ya Uhamiaji kufanya misako kwenye nyumba za wageni na kudhibiti wageni wanaoingia kwenye mipaka mbalimbali nchini kutokana na kushamiri kwa wahamiaji haramu.
Aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa idara na taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na Wilaya ya Arusha.
Ukosefu wa dawa.
Akizungumzia upatikanaji wa dawa, Majaliwa alisema serikali imetoa Sh trilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa dawa za aina mbalimbali ili kuondoa upungufu wa dawa kwenye hospitali nchini.
Akieleza namna serikali ilivyo na nia ya dhati ya kumaliza tatizo la dawa nchini, Majaliwa alisema; “Awali tulitoa Sh bilioni 40 kwa ajili ya dawa na sasa tumeongeza fedha hadi kufikia shilingi trilioni moja.
“Tunataka kero ya upungufu wa dawa hospitalini iishe. Naagiza kila hospitali kuhakikisha inakuwa na dirisha la huduma za bure kwa wazee pamoja na duka la dawa,” alisema.

Chanzo: ITV
Kwanza tulitoa 40 billion = USD 20 million
Sasa 1trillion = USD 500 million

Bomoa kichwa
 
Hivi bajeti ya dawa ilikuwa shilingi ngapi... mbona kama tumevuka lengo au tunampango wa kuteketeza dawa?
 
  • Thanks
Reactions: 999
Back
Top Bottom