Serikali yatoa trilioni moja kununua dawa

mkadiriajimajenzi

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
549
608
AHADI ya serikali ya kuanza kusambaza dawa katika hospitali zote nchini kutokana na madai ya kuwepo kwa uhaba wa dawa za aina mbalimbali, imeanza kutekelezwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ziarani mkoani Arusha amesema Serikali imetoa Sh trilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa dawa na kuhakikisha pia madaktari 8,000 wanasambazwa kwenye hospitali mbalimbali za mikoa na wilaya ili kutatua changamoto za afya na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Katika hatua nyingine, Majaliwa amewataka watendaji wa Idara ya Uhamiaji kufanya misako kwenye nyumba za wageni na kudhibiti wageni wanaoingia kwenye mipaka mbalimbali nchini kutokana na kushamiri kwa wahamiaji haramu.

Aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa idara na taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na Wilaya ya Arusha.

Ukosefu wa dawa.

Akizungumzia upatikanaji wa dawa, Majaliwa alisema serikali imetoa Sh trilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa dawa za aina mbalimbali ili kuondoa upungufu wa dawa kwenye hospitali nchini.

Akieleza namna serikali ilivyo na nia ya dhati ya kumaliza tatizo la dawa nchini, Majaliwa alisema; “Awali tulitoa Sh bilioni 40 kwa ajili ya dawa na sasa tumeongeza fedha hadi kufikia shilingi trilioni moja.

“Tunataka kero ya upungufu wa dawa hospitalini iishe. Naagiza kila hospitali kuhakikisha inakuwa na dirisha la huduma za bure kwa wazee pamoja na duka la dawa,” alisema.

Akizungumza kuhusu nidhamu ya fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika kila halmashauri alisema serikali imeridhia kutoa Sh bilioni 177 kwa halmashauri zote nchini kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

Aliwataka wakuu wa idara, wakurugenzi, mameya pamoja na wakaguzi wa ndani kuhakikisha fedha zinazotolewa na serikali zinakwenda katika miradi ile iliyokusudiwa na si vinginevyo.

Alisema Mkoa wa Arusha umepokea Sh bilioni 54 katika halmashauri zote kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kusisitiza kuwa serikali si kwamba haina fedha ila imeminya matumizi ya hovyo hovyo yaliyokuwa yakifanyika kwenye halmashauri au kubadilishwa fedha za matumizi ya miradi iliyokusudiwa.

Alisisitiza kuwa ni vyema maofisa maduhuli kukusanya maduhuli ili kuongeza mapato ya ndani yanayokusanywa ndani ya halmashauri ili kuwezesha bajeti za halmashauri kutekeleza mambo mbalimbali.

Wahamiaji haramu

Kuhusu wahamiaji haramu, Waziri Mkuu alisema inashangaza kuona hivi sasa kuna wimbi la watu wanaoingia katika maeneo mbalimbali ya mipakani na kuleta madhara mbalimbali ikiwemo kuzagaa kwa silaha za aina mbalimbali.

Alisema serikali haizuii wageni kutoka nje ya nchi kuingia nchini, lakini ni lazima udhibiti wa wageni hao ufanyike kwa ukamilifu ili kufahamu wanaingia nchini kufanya nini na wanakaa kwa siku ngapi ili kudhibiti wingi wa watu wanaoingia nchini.

“Fanyeni misako kwenye nyumba za wageni na sehemu nyingine ili kudhibiti watu wanaoingia nchini maana uingizwaji wa silaha zisizokuwepo nchini umeongezeka. Ni lazima tujue zinaingia kwa nini,” alisema.

Uwajibikaji serikalini

Akizungumzia nidhamu katika utumishi wa umma, Waziri Mkuu aliwasihi watumishi wa idara mbalimbali za serikali kuhakikisha wanafanya kazi kwa nidhamu kwa kuwatumikia wananchi wanaohitaji huduma mbalimbali.

Alisema baadhi ya wananchi hawana uelewa juu ya wapi wapeleke malalamiko yao, lakini kwa kuwa watumishi wa umma wapo, wanapaswa kuwasikiliza na kuwapa maelekezo sahihi ni wapi waende ili matatizo yao yatatuliwe na si kuwatolea maneno yasiyozingatia maadili.

“Serikali hii haitishi watumishi, hapana bali inasisitiza nidhamu ya kazi makazini, hivyo ni lazima kila mtu afanye kazi kadri anavyotakiwa kutekeleza majukumu yake. Serikali italipa madeni yote ya wafanyakazi wanayoidai, kwani hivi sasa inamalizia kulipa madeni ya ndani halafu watumishi watalipwa stahiki zao.”

Aliwataka wakuu wa mikoa na wilaya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kusoma vitabu vya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuyafanyia kazi yale yote yaliyokuwepo katika idara husika.

Alisisitiza Jiji la Arusha na halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya wazi ili kuwezesha wananchi kupata mahali pa kupumzikia, kwani hivi sasa hakuna maeneo ya kupumzikia kutokana na kila mtu kujenga nyumba hadi kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kwa ujenzi.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akisoma taarifa ya kwa Waziri Mkuu, alisema mkoa huo unajitahidi kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inaimarika.

Alisema hata hivyo unakabiliwa na upungufu wa walimu kwenye maeneo yaliyopo pembezoni mwa miji na hivi sasa wanalifanyia kazi suala hilo ili kuhakikisha walimu wanapelekwa kwenye shule zilizopo pembezoni.

Chanzo:Habari Leo
 
Hivi kampeni bado zinaendelea??
Itakuwa.Juzi kwenye taarifa ya habari nilimskia msemaji wa MUHAS akisema madakrari walio hitimu na ambao watahitimu mwaka ujao 2600.Sasa hai 8000 wanapatikana wapi?Au kwa msaada wa USAID.
 
wameongeza hela ya dawa kutoka kutoka billion 40 mpk trillioni moja? nna waiwasi na hizi figure
 
Siiaminigi tena hii serikali, hata pesa nyingine huwa zipo kwenye matamshi ila kiuhalisia hazipo/hawana.
 
Itakuwa.Juzi kwenye taarifa ya habari nilimskia msemaji wa MUHAS akisema madakrari walio hitimu na ambao watahitimu mwaka ujao 2600.Sasa hai 8000 wanapatikana wapi?Au kwa msaada wa USAID.

~~>>>Hao ni MUHAS pekee........ Changanya na wa Bugando, KCMC, IMTU, Hubert Kairuki n.k.
 
Yaaani makusanyo ya mwezi mmoja yote yaende kwenye dawa?

Basi serikali yetu inahela za kutosha.
 
Zinatumika pesa za ajira mpya! Maana kusitishwa kwake kumetunyima pesa nyingi sana
 
Yaaani wametoa bilioni 177 kwa halmashauri zote nchi nzima, halafu halmashauri za Arusha pekee zimepewa bilioni 54!? ......mbona hakuna uwiano hata kidogo.!
 
AHADI ya serikali ya kuanza kusambaza dawa katika hospitali zote nchini kutokana na madai ya kuwepo kwa uhaba wa dawa za aina mbalimbali, imeanza kutekelezwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ziarani mkoani Arusha amesema Serikali imetoa Sh trilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa dawa na kuhakikisha pia madaktari 8,000 wanasambazwa kwenye hospitali mbalimbali za mikoa na wilaya ili kutatua changamoto za afya na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Katika hatua nyingine, Majaliwa amewataka watendaji wa Idara ya Uhamiaji kufanya misako kwenye nyumba za wageni na kudhibiti wageni wanaoingia kwenye mipaka mbalimbali nchini kutokana na kushamiri kwa wahamiaji haramu.

Aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa idara na taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na Wilaya ya Arusha.

Ukosefu wa dawa.

Akizungumzia upatikanaji wa dawa, Majaliwa alisema serikali imetoa Sh trilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa dawa za aina mbalimbali ili kuondoa upungufu wa dawa kwenye hospitali nchini.

Akieleza namna serikali ilivyo na nia ya dhati ya kumaliza tatizo la dawa nchini, Majaliwa alisema; “Awali tulitoa Sh bilioni 40 kwa ajili ya dawa na sasa tumeongeza fedha hadi kufikia shilingi trilioni moja.

“Tunataka kero ya upungufu wa dawa hospitalini iishe. Naagiza kila hospitali kuhakikisha inakuwa na dirisha la huduma za bure kwa wazee pamoja na duka la dawa,” alisema.

Akizungumza kuhusu nidhamu ya fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika kila halmashauri alisema serikali imeridhia kutoa Sh bilioni 177 kwa halmashauri zote nchini kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

Aliwataka wakuu wa idara, wakurugenzi, mameya pamoja na wakaguzi wa ndani kuhakikisha fedha zinazotolewa na serikali zinakwenda katika miradi ile iliyokusudiwa na si vinginevyo.

Alisema Mkoa wa Arusha umepokea Sh bilioni 54 katika halmashauri zote kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kusisitiza kuwa serikali si kwamba haina fedha ila imeminya matumizi ya hovyo hovyo yaliyokuwa yakifanyika kwenye halmashauri au kubadilishwa fedha za matumizi ya miradi iliyokusudiwa.

Alisisitiza kuwa ni vyema maofisa maduhuli kukusanya maduhuli ili kuongeza mapato ya ndani yanayokusanywa ndani ya halmashauri ili kuwezesha bajeti za halmashauri kutekeleza mambo mbalimbali.

Wahamiaji haramu

Kuhusu wahamiaji haramu, Waziri Mkuu alisema inashangaza kuona hivi sasa kuna wimbi la watu wanaoingia katika maeneo mbalimbali ya mipakani na kuleta madhara mbalimbali ikiwemo kuzagaa kwa silaha za aina mbalimbali.

Alisema serikali haizuii wageni kutoka nje ya nchi kuingia nchini, lakini ni lazima udhibiti wa wageni hao ufanyike kwa ukamilifu ili kufahamu wanaingia nchini kufanya nini na wanakaa kwa siku ngapi ili kudhibiti wingi wa watu wanaoingia nchini.

“Fanyeni misako kwenye nyumba za wageni na sehemu nyingine ili kudhibiti watu wanaoingia nchini maana uingizwaji wa silaha zisizokuwepo nchini umeongezeka. Ni lazima tujue zinaingia kwa nini,” alisema.

Uwajibikaji serikalini

Akizungumzia nidhamu katika utumishi wa umma, Waziri Mkuu aliwasihi watumishi wa idara mbalimbali za serikali kuhakikisha wanafanya kazi kwa nidhamu kwa kuwatumikia wananchi wanaohitaji huduma mbalimbali.

Alisema baadhi ya wananchi hawana uelewa juu ya wapi wapeleke malalamiko yao, lakini kwa kuwa watumishi wa umma wapo, wanapaswa kuwasikiliza na kuwapa maelekezo sahihi ni wapi waende ili matatizo yao yatatuliwe na si kuwatolea maneno yasiyozingatia maadili.

“Serikali hii haitishi watumishi, hapana bali inasisitiza nidhamu ya kazi makazini, hivyo ni lazima kila mtu afanye kazi kadri anavyotakiwa kutekeleza majukumu yake. Serikali italipa madeni yote ya wafanyakazi wanayoidai, kwani hivi sasa inamalizia kulipa madeni ya ndani halafu watumishi watalipwa stahiki zao.”

Aliwataka wakuu wa mikoa na wilaya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kusoma vitabu vya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuyafanyia kazi yale yote yaliyokuwepo katika idara husika.

Alisisitiza Jiji la Arusha na halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya wazi ili kuwezesha wananchi kupata mahali pa kupumzikia, kwani hivi sasa hakuna maeneo ya kupumzikia kutokana na kila mtu kujenga nyumba hadi kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kwa ujenzi.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akisoma taarifa ya kwa Waziri Mkuu, alisema mkoa huo unajitahidi kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inaimarika.

Alisema hata hivyo unakabiliwa na upungufu wa walimu kwenye maeneo yaliyopo pembezoni mwa miji na hivi sasa wanalifanyia kazi suala hilo ili kuhakikisha walimu wanapelekwa kwenye shule zilizopo pembezoni.
Tamko jingine ........
 
Serikalini hutumia fedha kutekeleza majukumu yake kufuatana na bajeti iliyoidhinishwa na bunge. Nashangaa serikali kutoa fedha kwa majukumu yaliyotengewa fedha inaitisha waandishi wa habari. Au huamua kutoa taarifa kama vile wamefanya jambo ambalo halikupangwa kufanya ila inalitekeleza kwa mpango wa dharura.
Lengo lake ni nini?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom