Serikali yatoa kibali cha ajira kuziba nafasi zilizoachwa na waliokutwa na vyeti feki

Evans-Arsenal

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
868
1,385
Waziri Angela Kairuki amesema kwamba serikali itaanza kuajiri watumishi wa serikali kwa kada mbalimbalk hususani katika sekta ya Afya na Elimu kutokana na upungufu wa asilimia 70% waliokumbwa na sakata la vyeti vyeki.

Pia ameongeza kwa kusema mishahara itapanda kutokana na agizo la Rais Pombe Magufuli na kwamba mishahara itapanda kutokana na ukuaji wa uchumi na mfumuko wa bei pamoja na kima cha chini cha mshahara kupanda kwa asilimia mia mbili 200% na kwamba mshahara umetoka kuanzia 100,000/= mpaka kima cha chini kuwa 300,000/=

Akijibu swali la Mbunge Lucy Mollel kwamba mafunzo kwa watumishi bado yanaendela na kwamba serikali haijafuta mafunzo kwa watumishi wa umma.

Waziri Kairuki amesema kwamba kwa sasa wanasubiri taarifa toka Tamisemi ili waweze kujua idadi ya watumishi wanaohitajika katika kila idara katika halimashauri mbalimbali nchini.

------
Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mh.Angela Kairuki amesema tayari serikali imeshatoa kibali cha ajira 15000 kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliobainika kuwa na vyeti feki katika zoezi lililofanyika nchi nzima la kuwabaini na muda si mrefu nafasi hizo zitajazwa.

Mh.Kairuki amesema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati aijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalum iringa mh.Rita Kabati aliyetaka kufahamu juu ya ujazwaji wa nafasihizo ambaye amekiri upungufu huo kusababisha usumbufu mkubwa katika taasisi mbalimbali za umma hivyo kuwahakikishia wananchi na kuwa tatizo hilo litakwisha hivi karibuni.

Katika hatua nyingine akijibu swali la Mbunge wa Mtwara mjini Mh.Maftaha Abdallah Nachuma aliyetaka uboreshwaji wa bandari ya Mtwara kwa kudai kuwa imesahaulika licha ya kuwa na kina kirefu katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati,Naibu waziri wa ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano Mh.Edwin Ngonyaniamesema serikali inampango wa kuboresha na kuendeleza bandari zote nchini ikiwemo bandari ya Mtwara ili kuipunguzia mzigo bandari ya Dar es Salaam.

Mh.Ngonyani amesema kwani tayari imeshatenga fedha kwaajili ya ujenzi wa gati katika bandari ya Mtwara yenye urefu wa meta 350 itakayogharimu zaidi ya shiling bilioni137 inayotarajiwa kukamilika ndani ya miezi 21.

Chanzo: ITV
 
Hizo taarifa wanasubiri mpaka lini wakati idadi ya waliotumbuliwa inajulikana na idadi
ya uhitaji kutoka kila mkoa na halmashauri nchini unajulikana.
Wakiendelea na hii kasi yao ya kobe, wajue tuna waundia tume kama ya mchanga wa madini.

NB: wasije kutulaumu kwa mapendekezo ya tume ya ajira.
 
Huyu bibi bora akae kimya tu.

Walianza kusema wataajiri watu 70000 wakapunguza 50000 na leo wanasema wansubiri taarifa kutoka Tamisemi ili wajue idadi ya watumishi wanaohitajika katika kila idara huku anasema afya kuna upungufu wa 70% sasa hiyo 70% wameitolea wapi?

Waziri kudanganya haipendezi.
 
Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mh.Angela Kairuki amesema tayari serikali imeshatoa kibali cha ajira 15000 kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliobainika kuwa na vyeti feki katika zoezi lililofanyika nchi nzima la kuwabaini na muda si mrefu nafasi hizo zitajazwa.

Mh.Kairuki amesema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati aijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalum iringa mh.Rita Kabati aliyetaka kufahamu juu ya ujazwaji wa nafasihizo ambaye amekiri upungufu huo kusababisha usumbufu mkubwa katika taasisi mbalimbali za umma hivyo kuwahakikishia wananchi na kuwa tatizo hilo litakwisha hivi karibuni.

Katika hatua nyingine akijibu swali la Mbunge wa Mtwara mjini Mh.Maftaha Abdallah Nachuma aliyetaka uboreshwaji wa bandari ya Mtwara kwa kudai kuwa imesahaulika licha ya kuwa na kina kirefu katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati,Naibu waziri wa ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano Mh.Edwin Ngonyaniamesema serikali inampango wa kuboresha na kuendeleza bandari zote nchini ikiwemo bandari ya Mtwara ili kuipunguzia mzigo bandari ya Dar es Salaam.

Mh.Ngonyani amesema kwani tayari imeshatenga fedha kwaajili ya ujenzi wa gati katika bandari ya Mtwara yenye urefu wa meta 350 itakayogharimu zaidi ya shiling bilioni137 inayotarajiwa kukamilika ndani ya miezi 21.

Chanzo: ITV
 
Uongo halmashauri bado hazijapokea vibari hii serikali inawalaghai wananchi kwa nini?
 
Back
Top Bottom