Serikali yatishia walimu watakaogoma, wasambaza form walimu wajaze kama wanataka mgomo au kazi!

Waalimu wakitishika wamekwisha! Kama swala kweli liko mahakamani hizo fomu ni za nini? Hivyo ni vitisho tu hakuna kurudi nyuma. Hata sensa hakuna kushiriki
 
Asiyeridhika na mshahara akatafute ajira kwingine..! Ni bora ikaeleweka wazi kuwa hatuna walimu kuliko kuwa na walimu ambao serikali yetu haina uwezo wa kulipa Tsh 7,500,000/=kwa kila mwalimu kwa mwezi.
 
Vurugu zote hizi matatizo yanamwendea mwanafunzi,huo ndo ukweli,wasipotumika kwenye miradi ya waalimu,basi wanabakia kumaliziwa hasira wao.
 
Nimeona form kama hiyo mda c mrefu.
Kwenye form hiyo kati ya walimu 47, walimu 43 wameridhia kuwa watagoma na walimu 4 wamekataa.
Hizi form hazijawatisha hata kidogo.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Katika hali ya kustaabisha serikali kupitia kwa maafisa elimu wilaya wamesambaza form zinazowataka walimu wajaze kama wanaunga mkono mgomo au la.

Huku ni kujikanganya kwani chombo pekee kisheria chenye mamlaka ya kuwauliza wafanyakazi kama wanataka mgomo au la ni CHAMA CHA WAFANYAKAZI KILICHOSAJILIA NA CWT WANAKIDHI KATIKA HILO.

To my fellow teachers:

Tusikubali hata kidogo kupewa kitisho hiki ambacho naweza kuita cha kijinga na DHAIFU letu liwe moja TUSIENDA KAZINI JAPO HIZI SIKU TANO TUWAPE MUDA WA KUSHUGHULIKIA MADAI YETU LA SIVYO HAWA WATATUTAKA TULIPIE KODI HATA HII PUMZI YA BURE TUIVUTAYO

Source: AFISA ELIMU MZALENDO NA MWENYE MACHUNGU NA WALIMU KWA NAE NI MWALIMU ALIYEPANDA CHEO HIVI KARIBUNI

Serikali wanatumia mbinu zilezile walizotumia kwa Dr.kwa kuwaada wananchi ili walimu waonekane wabaya.Hapa kuna issue mbili mbali ya walimu kudai nyongeza ya mishaara na posho lakini wanamadai ya msingi wa malimbikizo ya madai yao kwa serikali kitu ambacho hakizungumziwi zaidi ya kuwaada kuwa serikali wapo kwenye mchakato kitu ambacho akitoi majibu mujarabu kwa walimu.Ili kuwanyamazisha walimu serikali wanataka kuwatumia kwenye sensa kitu ambacho siyo automatic lazima uombe na vigezo vitazingatiwa na ni zoezi la muda tu.
Serikali hii ya kukimbilia mahakani kila siku itawafikisha wapi?
 
kweli mfa maji haishi kutapatapa mara mahakamani kuzuia migomo mara maafisa elimu na fomu za kuzuia migomo...huu ni upuuzi usiweza kuvumilika..hatuwezi kuendelea kuona mahakama zikitumika kama chaka la kuminya haki za watanzania..walimu wamesisitiza mgomo serikali inasema ni kinyume cha sheria lakn wakati huo huo serikali inachukua hatua za kiutawala na haiambiwi kwamba inavunja sheria..kama mahakama imeshatoa uamuzi na ukapuuzwa kwa nn mahakama hiyo hiyo isitoe adhabu ya kupuuzwa kwa amri amri yake...badala yake serikali ndo inafanya hivyo kwniaba ya mahakama...hii haikubaliki...mamlaka hizi sasa zimekosa uhalali wa umma/ these state authorities have lost public legitimacy altogether...and one should expect them to be respected....this seriously outrageous
 
Fomu za kuwajazia walimu walio katika mgomo kwa wasiohudhuria mashuleni zimesambazwa kila shule huku wakuu wa shule wakiamrishwa kuwajazia wasiofika kazini ni kuziwakilisha serikalini.Hii nimeiona ktk baadhi ya shule nilizoweza kutembelea na kuwakuta walimu waliofika wakiwa wapo vijiweni wakipiga soga na huku walishasaini kuwepo kazini na wanafunzi kuwepo mitaani wakilandalanda kama mbuzi wasio na mchungaji.
Nilipoona fomu hizo zilinidhihilishIa ni jinsi gani watawala wetu uwezo wa kimaamuzi ulivyo wa kukurupuka na usio na mwisho mzuri kwa taifa.Nikajaribu kujiuliza maswali machache
1. Hivi kwa aliye na akili timamu kuna tatizo gani kama mwalimu atafika shule kila siku bila kufanya kazi?
2. Je kuwepo kwake kutakuwa kumemaliza tatizo?
3. Je inawezekana akalazimishwa kufundisha wakati hataki?
4. Je wamejiridhisha kuwa walimu wakuu wanaopewa hizo fomu kujaza wenyewe hawajagoma?
5. Je walimu wakuu wenyewe wanalizika na maslahi wanayopewa?
6. Na hivi kwa mwalimu mkuu mwenye akili timamu aweza kumchongea mwenzie ambaye wanateseka pamoja?

Lakini pia hii imenionesha ni jinsi gani wanafunzi wetu wanaomaliza shule za sekondary na msingi bila kujua kusoma wala kuandika ni faraja kwa watawala wetu ambao watoto wao wanasoma shule binafsi na wengine nje ya nchi na kuwaandaakuja kutawala mbumbumbu wa shule zetu za kata baada yao.

AKILI ZA MBAYUWAYU HIZI........
 
hata huku bunda nimeona afisa elimu na kamati ya ulinzi na usalama wakijiandaa kupeleka fumu hizo mashuleni
 
hata huku bunda nimeona afisa elimu na kamati ya ulinzi na usalama wakijiandaa kupeleka fumu hizo mashuleni

Wapeleke tu kwani walimu watasaini na hawatafundisha Kama ambavyo madaktari wanasaini na hawafanyi kazi, wamefukuza intern doctors nenda Kcmc hakuna clinic za kawaida za wagonjwa Wa nje. Wanarudishwa kila wagonjwa wakienda
 
Walimu wagangamale kama tu mpaka kieleweke. Hii ya mgomo baridi serikali ya Bongo hawajali kwani haiwaaffect watoto wao wala Vyeo vyao. Ila mgomo wa kikweli kweli kwa vile unatishia uhai wa CCM watajitahidi kuumaliza kwa kila mbinu kama walivyofanya kwa Madaktari.
 
Back
Top Bottom