Serikali yatishia kulifungia gazeti la Mwananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yatishia kulifungia gazeti la Mwananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlachake, Oct 20, 2010.

 1. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Serikali Imetishia kulifungia Gazeti la mawanachi kwa kuandika Habari Za uchochezi zidi ya Serikali Iliyopo madarakani. Habari zaidi mwanachi ya leo tar 20/10/2010  [​IMG]

  SERIKALI imetishia kulifunga au kulifutia usajili gazeti la Mwananchi kwa madai kwamba linaandika habari za uchochezi dhidi ya serikali ya awamu ya nne.Barua ya serikali yenye kumbukumbu namba ISC/N.100/1/VOL.V/76 iliyoandikwa kwa mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi, inaonya kwamba kama gazeti hili litaendelea kuandika habari ambazo imeziita za uchochezi dhidi yake, haitasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za nchi.

  Hata hivyo, barua hiyo haijaweka bayana habari hizo ilizozielezea kuwa ni za mtazamo hasi dhidi ya serikali na ambazo imedai kuwa ni za uchochezi.

  "Kwa barua hii unatakiwa kuacha mara moja tabia ya kuandika habari za uchochezi na kuidhalilisha nchi na serikali kwa kisingizio cha uhuru wa habari na uhuru wa kutoa mawazo ulioanishwa katika katiba ya nchi yetu," inaeleza barua hiyo ya Oktoba 11 iliyosainiwa na Raphael Hokororo kwa niaba ya Msajili wa Magazeti.

  "Aidha ukiendeleza tabia hiyo, serikali haitasita kuchukua hatua stahiki za kulifungia gazeti lako au kulifutia usajili kwa mujibu wa sheria za nchi."

  Barua hiyo, ambayo imebeba kichwa cha habari kisemacho "Karipio kali kwa kuandika habari zenye mwelekeo wa uchochezi wa kudhalilisha", ni mwendelezo wa barua nyingine iliyoandikwa na mkurugenzi wa Idara ya Habari, Clement Mshana kwenda kwa mhariri wa gazeti hili Septemba 24, 2010.

  Katika barua hiyo ya Mshana, serikali imedai kuwa gazeti la Mwananchi limekuwa na mtazamo hasi dhidi ya serikali na ikamtaka mhariri ajieleze.

  Barua hiyo yenye kumbukumbu namba ISC/N.100/1/VOL.V/70, bila ya kutoa mifano, inadai kuwa Mwananchi imekuwa ikiandika habari hasi tu kana kwamba serikali haina zuri linalofanywa kwa wananchi wake na kutaka maelezo.

  "Katika kipindi kirefu sasa, na zaidi wakati huu wa kampeni za uchaguzi, gazeti lako limekuwa likiandika habari zenye mtazamo hasi dhidi ya serikali. Habari hizo zimekuwa zikidhalilisha serikali iliyo madarakani ya awamu nne," inasema sehemu ya barua hiyo.

  Katika majibu ya barua hiyo ya kwanza, Mwananchi Communications Ltd (MCL), ilieleza kuwa baada ya kutafakari kwa kina ilishindwa kuelewa msingi wa tuhuma hizo ambazo hazina mifano yoyote ya habari inayodaiwa kuwa ni hasi kwa serikali.

  "Baada ya kupitia barua yako na kuitafakari, imetuwia vigumu kuelewa msingi wa tuhuma zako kwa gazeti hili kuhusu mtazamo hasi dhidi ya serikali bila hata kutoa mifano ya habari ambazo zinabeba tuhuma zako kwa gazeti hili hasa unaposema kuwa kwa kipindi kirefu sasa, hasa wakati huu wa kampeni za uchaguzi," inasema barua hiyo yenye kumbukumbu namba MCL/RN/09/VOL.1.27 iliyoandikwa na mhariri mtendaji wa MCL, Theophil Makunga.

  Barua hiyo ya MCL inaeleza kuwa kimsingi habari za kampeni za uchaguzi katika kipindi hiki zinahusu vyama vya siasa na kuhoji sababu za serikali kujiona inaandikwa vibaya na Mwananchi wakati ni vyama ndivyo vinavyoshiriki kwenye kampeni.

  Mhariri wa Mwananchi anaeleza katika barua hiyo kuwa kwa sasa gazeti lake linaandika habari za wagombea uongozi kutoka vyama mbalimbali na sera zao ili wananchi wafanye uamuzi siku ya kupiga kura na hakuna chama kilichoandika barua ya malalamiko.

  "Kwa taarifa yako tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi Agosti 21, 2010, gazeti la Mwananchi halijawahi kupata malalamiko kutoka chama chochote cha siasa kinachoshiriki katika kampeni hizo juu ya kuandikwa vibaya. Kimsingi Mwananchi linachofanya ni kuripoti wanachosema wagombea wa vyama mbalimbali au kufanyiwa katika mikutano ya kampeni," inasema barua hiyo ya MCL kwenda kwa Msajili wa Magazeti.

  Katika barua hiyo, MCL inaiomba serikali kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu kuhusika kwa serikali katika kampeni za uchaguzi hadi gazeti hili lionekane lina mtazamo hasi.

  "Kwa msingi huo, tunaomba ufafanuzi zaidi hapa; serikali inahusika vipi katika kampeni mpaka Mwananchi ionekane ina mtazamo hasi kwa serikali wakati vinavyoshiriki katika kampeni ni vyama vya siasa na wagombea wake," inasema barua hiyo.

  Baada ya barua hiyo, Msajili wa Magazeti alijibu kwamba majibu yaliyotolewa na MCL hayaridhishi na hivyo ofisi yake haikuridhika na utetezi huo.

  "Kama tulivyoeleza kwenye barua yetu kwako kuwa katika kipindi kirefu sasa na zaidi wakati huu wa kampeni za uchaguzi, gazeti lako limekuwa likiandika habari zenye mtazamo hasi dhidi ya serikali. Gazeti lako sasa limeamua kufanya ‘house style' yake ya kuandika habari zenye uchochezi na kudhalilisha nchi na serikali iliyopo madarakani," inasema barua hiyo.

  Katika onyo lake, serikali inasema kwamba picha, habari zinazopewa kipaumbele katika ukurasa wa kwanza wa gazeti zinatiwa chumvi kwa lengo la kuchochea wananchi waione serikali yao haijafanya chochote kwa maendeleo yao.

  Akiongelea hatua hiyo ya serikali, Makunga alisema kwamba MCL imeshtushwa na karipio hilo ambalo halikuonyesha ni habari ipi ambayo gazeti la Mwananchi limekosea.

  "Msajili hakunukuu hata sheria moja ya vyombo vya habari kuonyesha jinsi gani gazeti limekosea wala habari au kichwa cha habari chenye mtazamo hasi kwa serikali," alisema Makunga.

  Alisema Mwananchi imechukulia hatua hiyo ya msajili kuwa inatishia uhuru wa vyombo vya habari hasa katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi ambacho kinahitaji uvumulivu baina ya taasisi mbalimbali katika jamii.

  Makunga alisema kwa kuwa Mwananchi na msajili inaonekana kutokubaliana katika suala hilo, wameamua kupeleka taarifa Baraza la Habari Tanzania (MCT) liweze kufanya uchunguzi kwa mujibu wa katiba yao.

  Alisema msimamo wa sera ya uhariri ya MCL inasimamia kwenye ukweli na weledi pasipo kushurutishwa na vikundi vyovyote vya nje na ndani.Makunga alisema Mwananchi itaendelea kuandika habari za ukweli bila ya kumuonea mtu au taasisi yoyote kwa maslahi ya Tanzania.


  Source: MWANANCHI
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,748
  Trophy Points: 280
  Kulifungia kwa sababu zipi? Mbona habari ni nusunusu hivyo?
   
 3. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  :jaw:
   
 4. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Yetu macho lakini kwa mtazamo serikali imelichukulia jambo hilo kwa ujumla. Mbona Daily News lilipoandika kwa Dr Slaa hawezi kuwa rais wa awamu ya tano hawakusema kitu au gezeti la Tanzania Daima inajulikana ni la nani na huwa haliandiki habari zenye mtazamo chanya kwa serikali?
  Kifupi Mwananchi ndilo gazeti lenye wigo mpana zaidi kuliko magazeti yote sasa kama watakuwa watu wa kunyoosha nadhani impact yake ni kubwa.
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Mh, jamani hii si kuwatisha watu? Mbona sijaona uchochezi kwa hili gazeti au sielewi maana ya uchochezi? Huwa naona kama wanajaribu kubalance haya mabo ya siasa za uchaguzi. " In africa, we are yet to have true democracy, leaders propagate democracy but are happy when the mass becomes demo crazy!" source: Popular quotes
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Inaelekea zile pesa nyingi ambazo serikali kupitia sisi m waligawa kwa vyombo vya habari ili iandikwe vizuri ziligonga mwamba hapa. Au kama walizipokea basi hawakufanya kilichotarajiwa kwa lugha nyingine waliwekwa ndani. Na hapa sasa naanza kuelewa kwa nini vyombo vingi vya habari vimekuwa mstari wa mbele kulipoti tu yale ya sisi m na kubagua vyama vingine.

  Sasa vitisho visivyo na msingi havina nafasi katika nchi hii. Narudia tena kwa msajili wa magazeti kwamba vitisho tu visivyo na ground havina nafasi na kwa kweli msajili wa magazeti amechelewa sana na kwa kufungia gazeti kwa sababu hizo alizoandika atakuwa amewasha moto mkubwa tena moto wa ajabu.

  Ningefurahi kama angelionya gazeti la uhuru pia kwa kuandika habari hasi kuhusu vyama vingine maana hilo pia linakosanisha wananchi na vyama vyao. Tena nilitegemea angetoa onyo kwa magazeti na vyombo vya habari vilivyotayarishwa kuwachafua baadhi ya wagombea urais kwa makusudi mbele ya jamii.

  Ni nafasi yake ya kuangalia na kujikagua tena kabla hajachukuliwa binafsi hatua za kisheria. Uzuri kadri tusogeavyo mbele ndivyo tunavyozidi kuelewa kuwa tuna utawala wa sheria na ni rahisi hata kumpeleka mahakamani mtu kama msajili kudai haki yako kisheria. Na isitoshe kwa sasa inaingia serikali mpya madarakani. Hiyo haitakuwa na minyororo dhidi ya vyombo vya habari.
   
 7. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi nasoma Mwananchi tu ninapotaka kupata habari za ukweli!! CCM wana kiwewe maana wanataka wananchi wasihabarishwe na kuambiwa ukweli ili wafanye maamuzi yanayotokana na ukweli.

  Serikali ya CCM imeoza kama chama chao, imejaa watu wa kujipendekeza pendekeza na waoga! Muulizeni huyo msajili wa magazeti ni chama gani kimelalamikia uandishi ktk gazeti hilo?

  Ama kweli siku ya kufa nyani (ccm) miti yote huteleza!!!!! je gazeti la Mtanzania la fisadi Rostam limeisha onywa au kufutwa???? Hokororo na Mshana wasilete za kuleta hapa, nchi hii ni nchi yetu wote sisiem, chadema, cuf na vyama vingine vyote!
   
 8. Mkimbizi

  Mkimbizi JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  serikali imechoka haswa... MWananchi wanaripoti mambo ya kampeni na vyama, eti serikali inasema inadhalilishwa!! Hahaha mwaka huu chokozeni tunaingia mtaani na mtatuua sisi ila ni kwa faida ya vizazi vijavyo! Tumechoka na udhalimu wenu! Grrrrr
   
 9. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kweli linaleta uchochezi, Very GOOD serikali imeliona

  itakuwa vizuri kulifungia
   
 10. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hata Mwanahalisi limepewa karipio!! Haya ndio matunda ya katiba mbovu - Rais ndio huyo huyo Mgombea Urais - very ridiculous!!!!

  Daily News walipotangaza matokeo ya Urais 2010, walipewa karipio? Kwa nini Mwananchi gazeti ambalo limeonekana kutoa habari bila kuegemea upande wowote na Synovate walifanya uchunguzi na kulipa sifa hiyo kuwa la kwanza?

  Hii ni mbinu chafu ya CCM, huko ni kushindwa kwa hoja.

  Na sasa watakoma Mzee Mengi nae ameanza kuzingatia professionalism na ethics za uandishi wa habari kwenye vyombo vyake vya habari. Check the Guardian ya jana front page photo
  [​IMG]
   
 11. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Mbona hawafungii vijarida vya al.huda na al.nuuur vinavyochochea udini?
   
 12. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Mimi linanichochea kumchagua Dr. Slaa!!
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  Oct 20, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Huyu Mhariri wa MWANANCHI yuko sahihi kabisa, Serikali ieleze ni habari ipi ilikuwa hasi na inayoleta uchochezi badala ya kuelezea jumla jumla! Gazeti la MWANANCHI msiogope chochote endeleeni na kutujulisha habari kama zilivyo! After all mimi sioni zuri lililofanywa na Serikali ya awamu ya nne ambalo linastahili kuandikwa kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti, hata la udaku!
   
 14. Mkimbizi

  Mkimbizi JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nilitaka niandike hivyo ila nikakumbuka ile mada ya udini nikaacha! Kacheki magazeti ya kikristu habari zake na hayo Al. Huda! Tofauti kabisaaaa!!!!! Ila haya tunayoyaweka kiporo iko siku yatalipuka tu!!
   
 15. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Mwananchi siku kuanzia tarehe 30 mpaka 10 Nov 2010 andikeni matukio yote kama manavyoandika kwa sasa kuanzia kuonekana kwa malori yakiwa na shehena ya masanduku ya kura, kuchakachua matokeo, vurugu zitakazo letwa na Green Guard, kuanguka kwa Kikwete jukwaani, na kuapishwa kwa Dr. Slaa, JK na family yake kuhama Ikulu. Na wana bahati Sakina Datoo alihama huko.
   
 16. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hapo ni changa la macho, MCL ni ya Rostam, habari zinazoandikwa ni katika propaganda zao, kwa hiyo wanamtumia jamaa ili watu wengi walisome lipate umaarufu ili mchezo mchafu utakapochezwa waseme mbona mwananchi halikuandika?
   
 17. F

  Fanfa JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 25, 2009
  Messages: 538
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huu ni ujinga. Wanadhani kuweka vitisho ndio kuziba midomo ya watanzania. Na bado, joto litapanda, kama ni homa itapanda. kama ni malaria sugu itawapeleka ahela mwaka huu.

  Longolongo zote hizi za nini. Ukisoma gazeti la Uhuru unapata kichefuchefu maana ni habari za kichochezi
   
 18. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hakuna haja ya kuchekeana kama serikali yao inavyofanya, ametoa shutuma aseme! na afungie kabisa gazeti hilo.
   
 19. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #19
  Oct 20, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Serikali ya Kikwete ina laana.

  Inataka kusifiwa hata kwa unafiki kama wanavyofanya Uhuru, Mtanzania, HL na DN.

  Viva Mwananchi. Na litauza(Mwananchi) sana mwaka huu!!! Kwanza leo nimelinunua. Jana vilevile. Kesho kama kawa. 7/week*(majuma kwa mwaka)52*500*(watu)1000000 = TZS 182 000 000 000 000.

  Hard to swallow, right??

  Poleni sana mafisadi
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Oct 20, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Alishauza hisa zake kitambo
   
Loading...