Serikali yatishia kuivunja Halmashauri ya Jiji la Tanga kama mgogoro wa kisiasa ukiendelea

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Serikali imetishia kuivunja Halmashauri ya Jiji la Tanga iwapo haitamaliza mgogoro wake wa kisiasa.

Akizungumza na viongozi serikali na kisiasa jijini Tanga Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, alisema serikali italazimika kuivunja halmashauri hiyo endapo mgogoro huo hautamalizwa haraka, kutokana na ukweli kwamba tangu kuanza kwa uongozi wa awamu ya tano baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana imeshindwa kufanya vikao vyake halali kwa mujibu wa katiba kutokana na mgogoro wa kisisa bina ya Chama Chama cha Mapinduzi (CCM) na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa, huku wananchi wakishindwa kutatuliwa kero zao kwa wakati hivyo kuzorotesha maendeleo yao.

“Mpaka sasa jiji la Tanga hakuna uongozi uliosimama, sasa hatuwezi kwenda kwa mwendo huu, wananchi wanahitaji maendeleo na kurudia uchaguzi hatuwezi ni gharama kubwa, kilichobaki ni kuivunja halmashauri mpaka hapo muda wa kufanya uchaguzi kwa mujibu wa katiba ya nchi utakapotimia, hivyo kwa maana nyingine kama itavunjwa serikali kuu ndiyo itasimamia shughuli za jiji hili,” alisema Suluhu.

Alisema mkoa huo una mipango mbalimbali ya maendeleo lakini haiwezi kutekelezeka kutokana na mgogoro uliopo na kuwataka viongozi wa mkoa kwa kushirikiana na wazee kukaa chini kutafuta namna ya kuumaliza haraka.

“Jiji ni kioo cha mkoa mzima, sasa kama wazee hawatakaa kitako na viongozi kutafuta suluhu, basi hii mipango yenu yote ya kufufua viwanda itakuwa ni ndoto tu kwa sababu hapa mjini hakupo shwari na tunalitambua hilo,” alisema.

Mgogoro wa umeya Tanga umeibuka baada ya CCM yenye madiwani wachache kushinda nafasi hiyo dhidi ya Ukawa yenye madiwani wengi jambo ambalo linapingwa na umoja huo unaondwa na vyama vya CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi na NLD.
 
Huu ni unafiki uliopitiliza kwa kweli

Leo anauona mgogoro wa Tanga zaidi na kutaka kuchukua hatua, wakati Dar zilipo ofisi zote za serikali uchaguzi wa meya unapigwa danadana NA AMEKAA KIMYA.
AU JIJI LA DAR HALIHITAJI HALMASHAURI KUENDESHA SHUGHULI ZAKE!!

UUnafikirUnafiki
 
Ukawa Bwana hapo wanachotakiwa kujua ni kwamba kuna baadhi ya madiwani wa UKAWA hawakuwa na Imani na Meya aliesimamishwa kwa chama chao ndio mana kura walimpa wa CCM, Tanga kwanza vyama baadae.
 
Anamtishia nani huyu nae? Baada ya kubaka demokrasia anakuja na vitisho? Hivyo viwanda Tanga nani kaviua? Alie viua lazima aifufue kwa sababu alipo viua kulikuwa na uongozi wao katika Halmashauri hiyo, huyu mea wao wa kichina lazima aondoke .
 
I seeee...Hiki pia ndicho kinakuja dar es salaam....CCM wanatengeneza migogorooooo bila sababu hatimaye waseme kama hichi wanachosema Tanga...upuuzi kweli
 
Wavunje hata halmadshauri au sijui manispaa za dar,maana sasa tushachoka na migogoro,NI KAZI TU........
 
Rais. Makamu wake na PM kumbe wanatudanganya na kauli zao kuwa wanadhamira ya kweli ya kuleta Maendeleo. Utaletaje Maendeleo huku unabaka demokrasia kwa manufaa ya chama chako?
Wajue kama wananchi wataondoa imani waliyo nayo sasa itakuwa vigumu kupata ushirikiano wanaouhitaji sana
 
Wazee Tanga Waombwa Kuondoa Tofauti Zao ktk Halmashauri ya Tanga mjini
Published on 28 Feb 2016
Makamu wa Rais,Mhe.Samia Suluhu awataka wazee na viongozi mkoani Tanga kumaliza tofauti ili waweze kuwatumikia wananchi waliowachagua

Source: Simu TV youtube
 
M
Ukawa Bwana hapo wanachotakiwa kujua ni kwamba kuna baadhi ya madiwani wa UKAWA hawakuwa na Imani na Meya aliesimamishwa kwa chama chao ndio mana kura walimpa wa CCM, Tanga kwanza vyama baadae.
nafiki mkubwa wewe...tuliokuwepo na kuhesabu kula tunajuwa alishinda Meya wa CUF lkn kwa maelekezo na kwa "mamlaka aliyopewa" mkurugenzi akaamua kumtangaza Diwani wa CCM kuwa Meya,huu ni ubakaji wa demokrasia,CCM wakubali kuwa kuna maeneo walishindwa na wanahitaji kukabidhi kwa UKAWA,Majiji kama Arusha,Dsm,Tanga na Mbeya CCM ilikataliwa katika sanduku la kura,miji mikubwa kama Iringa na mji mdogo wa Tunduma UKAWA walikubalika zaidi
Hatuwezi kujinadi kuwa tunapiga hatua za kimaendeleo kama hatuheshimu utawala wa sheria na haki za watu kuchagua na kuchaguliwa,Maendeleo ni pamoja na kuwa na demokrasia dhabiti.Hii inatoa taswira kuwa hata katika ubunge kuna maeneo mengi CCM imetumia "ubabe wa nguvu za kidola" kuwatangaza wagombea wake walioshindwa.Tulitegemea damu ya watu wa Arusha mwaka 2011 itawafanya watu wajifunze,lkn mikono imewajaa damu chungu nzima.
Tanga CUF walishinda,nyuma ya pazia mkurugenzi kwa msaada wa Mama Mwantumu Mahiza akahimiza CCM ndio watangazwe,Tunawalaumu kina Nkurunzinza na kina Kagame juu ya utawala wa "mkono wa chuma" tunadhani tabia hiyo ilizuka kama uyoga tu,hizi tabia za "U-Nkurunzinza" zinaanzia kwenye ngazi ya halmashauri na hatimaye Taifa.Dsm mnazungusha zungusha ili Jiji msiwape UKAWA mpaka uchaguzi wa 2020,tena kauli hizi zinatolewa na Mwanamke,Mama na mlezi kama Samia Suluhu??Muislam safi ndani ya wakfu wa hijabu unautamka uwongo kama huu??Wapeni Tanga haki yao kama ambavyo mnapaswa kuwapa wana wa Dsm....Aibu maneno haya kutamkwa na "Mama mlezi" kama Makamu wa Rais....wamama ktk dunia ni chanzo cha amani na si machafuko
 
Huu ni unafiki uliopitiliza kwa kweli

Leo anauona mgogoro wa Tanga zaidi na kutaka kuchukua hatua, wakati Dar zilipo ofisi zote za serikali uchaguzi wa meya unapigwa danadana NA AMEKAA KIMYA.
AU JIJI LA DAR HALIHITAJI HALMASHAURI KUENDESHA SHUGHULI ZAKE!!

UUnafikirUnafiki
Na wala hajui kama Zanzibar kuna mgogoro...
 
Suluhu: suluhisho sio kuvunja Halmashauri ya Jiji. Na wala usiudanganye umma kuwa kuna kurudia uchaguzi wenye gharama kubwa kwani uchaguzi wa Meya hauhitaji wananchi woote wa Jiji la Tanga kwenda kupiga kura. Waite Waheshimiwa Madiwani hao wachague Meya chini ya uangalizi muafaka, na sio wa wa kimaslahi kama ilivyokuwa mwanzo.
 
Wamechukua hatua gani kuzuia hiyo migogoro?
Kwa hali ilivyo huko Dar es salaam inaonekana kabisa serikali ndiye mchichwzi wa hii migogoro.
'Fyoko fyoko' wanazianzisha wenyewe halafu wengine wakijibu wanaziita fujo!!
 
Rais. Makamu wake na PM kumbe wanatudanganya na kauli zao kuwa wanadhamira ya kweli ya kuleta Maendeleo. Utaletaje Maendeleo huku unabaka demokrasia kwa manufaa ya chama chako?
Wajue kama wananchi wataondoa imani waliyo nayo sasa itakuwa vigumu kupata ushirikiano wanaouhitaji sana
Mkuu dalili ya mvua ni mawingu
 
Tanga ilikuwa kama model, kama mambo yangekuwa shwari baada ya mkurugenzi kupindua matokeo na kumtangaza siye hata Dar ingefanyika hivyo.
 
Serikali imetishia kuivunja Halmashauri ya Jiji la Tanga iwapo haitamaliza mgogoro wake wa kisiasa.

Akizungumza na viongozi serikali na kisiasa jijini Tanga Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, alisema serikali italazimika kuivunja halmashauri hiyo endapo mgogoro huo hautamalizwa haraka, kutokana na ukweli kwamba tangu kuanza kwa uongozi wa awamu ya tano baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana imeshindwa kufanya vikao vyake halali kwa mujibu wa katiba kutokana na mgogoro wa kisisa bina ya Chama Chama cha Mapinduzi (CCM) na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa, huku wananchi wakishindwa kutatuliwa kero zao kwa wakati hivyo kuzorotesha maendeleo yao.

“Mpaka sasa jiji la Tanga hakuna uongozi uliosimama, sasa hatuwezi kwenda kwa mwendo huu, wananchi wanahitaji maendeleo na kurudia uchaguzi hatuwezi ni gharama kubwa, kilichobaki ni kuivunja halmashauri mpaka hapo muda wa kufanya uchaguzi kwa mujibu wa katiba ya nchi utakapotimia, hivyo kwa maana nyingine kama itavunjwa serikali kuu ndiyo itasimamia shughuli za jiji hili,” alisema Suluhu.

Alisema mkoa huo una mipango mbalimbali ya maendeleo lakini haiwezi kutekelezeka kutokana na mgogoro uliopo na kuwataka viongozi wa mkoa kwa kushirikiana na wazee kukaa chini kutafuta namna ya kuumaliza haraka.

“Jiji ni kioo cha mkoa mzima, sasa kama wazee hawatakaa kitako na viongozi kutafuta suluhu, basi hii mipango yenu yote ya kufufua viwanda itakuwa ni ndoto tu kwa sababu hapa mjini hakupo shwari na tunalitambua hilo,” alisema.

Mgogoro wa umeya Tanga umeibuka baada ya CCM yenye madiwani wachache kushinda nafasi hiyo dhidi ya Ukawa yenye madiwani wengi jambo ambalo linapingwa na umoja huo unaondwa na vyama vya CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi na NLD.
Ivunje na DSM pia tuanachotaka maendeleo baasi. Siasa tupa kule!
 
Eti kurudia uchaguzi ni gharama sana serikali haiwezi, mbona nchini kwake Jecha ameamua warudie uchaguzi
Huyu mama nimeanza kumchukia kwa kuroooka kwake kwa asiyoyajua. Bora angekaa kimya na kufanya kazi yake ya kikatiba ya kutembea na mkasi au kunsubiri Rais anpokee airport kuliko kujisemea bila uelewa
 
Wametengeneza Migororo Ya Makusudi, Ili Kuwe Na Migongano Ya Kiitikadi!! Mwisho Wake Wafute Hizo Halmashauri Ambazo Wao CCM Wameshindwa Na Wapinzani Kushinda!! Hivyo Sio Kama Ni Vitisho Tu, Huyo Mama Sammia Anasema Kile Kilichopo Ktk Mpango Mkakati Wao!! Ndio Maana Kule Dar Wanafanya Figisu Figisu Za Makusudi, Ili Kupata Chanzo Cha Kuvunja Jiji Na Kuunda Tume Ya Jiji Ya Muda, Ambayo Itakuwa Madarakani Hadi Uchaguzi Mkuu Mwingine!!! Kubwa Ambalo Linalowasibu CCM, Ni Kutaka Kuficha UOZO Uliyopo Ktk. Halmashauri Na Majiji Ya Mengi!! Kuthibitisha Hilo, Tazama Zile Halmashauri Na Majiji Ambayo CCM Wameshinda Wao Hakuna Figisu Figisu Yoyote Ile, Uchaguzi Faster Tu Tokea Mwaka Jana!! Ila Waliposhindwa Ndipo Kwenye Figisu Figisu Za Ajabu Ajabu Tupu!!
 
matatizo mmesababisha wenyewe, jiji mmelitelekeza wenyewe leo wananchi wanachagua mbadala walau waone kama wakawa wanaweza kuwafumbua na kunyesha njia mpya Bado mnang'ang'ania.

Katika informed world hizi tabia za kupora maamuzi ya wananchi ndio inaelekea mwisho,
 
Back
Top Bottom