Serikali yateua wakurugenzi wapya wa halmashauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yateua wakurugenzi wapya wa halmashauri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BigMan, Jun 21, 2012.

 1. B

  BigMan JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  [h=3]SERIKALI YAFANYA MABADILIKO YA WAKURUGENZI NCHINI‏[/h]
  Masoud Masasi,Dodoma  SERIKALI imefanya mabadiliko katika halmashauri hapa nchini kwa


  kuwateua wakurugenzi wapya 14 huku ikiwavua madaraka wengine nane

  ambao walionekana kushindwa kuwajibika ipasavyo katika halmashauri zao

  na kufanya ubadhirifu wa fedha za halmashauri zao.  Pia katika mabadiliko hayo wakurugenzi kumi na moja wamepewa onyo


  kali huku wengine 22 wakihamishwa vituo vya kazi ambapo wakurugenzi

  watatu wakipumzishwa kufanya kazi katika halmashauri hizo kutokana na

  sababu mbalimbali ikiwemo ubadhilifu wa fedha .  Akitangaza mabadiliko hayo mbele ya waandishi wa habari jana mjini


  Dodoma Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za

  Mitaa(Tamisemi)Hawa Ghasia alisema mabadiliko hayo yanatokana na

  kuboresha nidhamu na utendaji wa kazi kwa wakurugenzi hao.  ‘’Wakurugenzi 14 wameteuliwa ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi huku


  wakurugenzi nane wakivuliwa madaraka hayo na Waziri Mkuu wengine

  watatu wakipumzishwa kabisa ambapo wakurugenzi 22 wakihamishwa katika

  vituo vyao na kupelekwa sehemu nyingine”  “Mabadiliko haya ni kuboresha utendaji wa kazi katika halmashauri zetu


  pamoja na kuongeza nidhamu na uwajibikaji wa kazi kwa wakurugenzi

  ambao walikuwa si waadilifu katika kutelekeza majukumu yao”alisema

  Ghasia.
  Waziri huyo aliwataja wakurugenzi wapya walioteuliwa kuwa ni Jenifer


  Omollo ambaye anakuwa mkurugenzi wa Mji wa Kibaha,Fidelica

  MyovelaMkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Musoma na Khadija Maulid

  Makuwani ameteuliwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.  Aliwataja wengine kuwa ni Ibrahim Matovu ameteuliwa kuwa mkurugenzi


  halmashauri ya Muheza,Idd Mshili halmashauri ya Mtwara,Julius Madiga

  Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa yaMorogoro na Kiyungi Mohamedi

  Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Shinyanga.  Wengini ni Lucas Mweri ameteuliwa Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya


  Nanyumbu,Miriam Mmbaga halmashauri ya Kigoma,Mwamvua Mrindoko

  Mkurugenzi mtendaji Nachingwea,Pendo Malembeja Halmashauri ya Kwimba

  huku Pudenciana akiteuliwa mkurugenzi wa Ulanga,Ruben Mfume

  Halmashauri ya Ruangwa na Tatu Selemani amekuwa mkurugenzi mtendaji

  halmashauri ya wilaya ya Kibaha ambapo waziri Ghasia alisema uteuzi

  huo ulifanyika april 24 mwaka huu.  Waziri huyo alisema wakurugenzi waliovuliwa madaraka kutokana na


  makosa mbalimbali katika Halmashauri zao kuwa ni Consolata

  Kamuhabwa(Karagwe),Ephraim Kalimalwendo(Kilosa),Elly Jesse

  Mlaki(Babati),Eustach Temu(Muheza),Jacob Kayange(Ngorongoro),Hamida
  Kikwega. (Chato),Majuto Mbuguyu(Tanga) na Raphael Mbunda halmashauri

  ya Manispaa ya Arusha.  Waziri Ghasia aliwataja wakurugenzi ambao wamepewa onyo kali kuwa ni


  Judetatheus Mboya(Newala),Lameck Masembejo(Masasi),Abdallah

  Njovu(Tandahimba),Jane Mutagurwa(Shinyanga),Silvia

  Siriwa(Sumbawanga),Kelvin Makonda(Bukombe),Alfred

  Luanda(Ulanga),Fanuel Senge(Tabora),Maurice Sapanjo(Chunya),na
  Beatrice Msomisi halmashauri ya Wilaya ya Bahi.  Pia waziri huyo alibainisha kuwa katika mabadiliko hayo wakurugenzi


  watatu ambao ni Xavier Tiweselekwa wa halmashauri ya Wilaya ya

  Misungwi,Erica Mussica kutoka halmashauri ya Sengerema na Theonas

  Nyamhanga wamepumzishwa kufanya kazi katika halmashauri hizo.

  “Maamuzi haya yalifanyika katika kipindi cha mwaka 2011/12 na hawa

  waliopewa onyo walitendeka makosa yao katika halmashauri zao hivyo

  pia wakurugenzi 22 wamehamishwa katika vituo vyao vya kazi na

  kupangiwa sehemu nyingine ili waweze kuimarisha utendaji kazi

  wao”alisema.  Alisema tayari wakurugenzi wanne waliotuhumiwa katika ubadhilifu


  mbalimbali katika halmashauri zao wameshafikishwa mahakamani huku

  wengine wakiendelea kufanyiwa uchunguzi ambapo amesema wakibainika

  watapelekwa mahakamani pia.  Alisema wale ambao walionekana hawakuhusika katika ubadhilifu katika


  vituo vyao vya kazi walipangiwa kazi nyingine huku wale walionekana

  utendaji wao sio mzuri walipumzishwa kabisa.

  Waziri huyo pia aliwataka wakurugenzi wapya walioteuliwa na wale wa

  zamani kuhakikisha wanafanya kazi kwa uhadilifu ili kuweza kuendelea

  kuboresha utendaji wa kazi katika mamlaka za serikali za mitaa nchini.  Hata hivyo alisema hataweza kumchukulia hatua yoyote mkurugenzi kwa


  kusikia taarifa za mitaani na kuwataka wale wenye malalamiko kupeleka

  ushahidi kwake ambapo atafanya uchunguzi kabla ya mhusika kuchukuliwa

  hatua za kisheria.  ‘’Tukisema tuanze kuchukuwa hatua kwa kusikia taarifa za mitaani basi


  tutajikuta tukifukuza wakurugenzi wote kinachotakiwa ni kuwa na

  ushahidi uletwe na utafanyiwa kazi na hatua zitachukuliwa kwa Yule

  atakayebainika”alisema waziri Ghasia.
   
 2. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Huyu Raphael Mbunda(Arusha) ndiye yule alihakikisha CHADEMA hakiongozi manispaa katika nafasi ya umeya kwa kuamini kuwa madudu yake mengi yangeibuliwa, kumbe alisahau kuwa ukweli hujitetea wenyewe. Akachakachue na huko mahakamani sasa.
   
 3. B

  BigMan JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  mbunda aliondolewa kabla ya uchaguzi na nafasi yake kuchukuliwa na estomiah chang'a ambaye bado anakaimu kilichofanyika hapa ni formality tu kwani aliondolewa na kuwa benchi sasa yapata miaka miwili
   
 4. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Jina langu halipo.... Jamaani
   
 5. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Sad stori kwa baba yangu Temu wa muheza.
   
 6. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Halufu ya udini, uislamu wadau!! Nadhani hili lipo.
   
 7. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Yaani hicho tu ndo ulichokiona?
   
 8. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  hawa ghasia a bogus minister
   
 9. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Huyo Consolata Kamuhabwa, alishushwa cheo na kuhamishiwa Mkoani Arusha kwa tuhuma za ubadhirifu wa mamilioni wa fedha za umma

  Afadhali sasa Waziri Mkuu amebadilisha.

  Na uozo wa Wilaya ya Babati, Serikali ilikaa kimya kwa muda mrefu. Heri sasa Mlaki ameondolewa.
   
 10. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu Pelekaroho jiji la Arusha halina Mkurungenzi toka kipindi cha maandalizi ya kuelekea uchaguzi wa 2010; tuhuma zako si za kweli maana hata aliyemtangaza Lema siyo Mbunda bal- kaimu Mkurugenzi Shag'ah.


  Nilitegemea ungehoji kwanini kwenye huu uteuzi hakuna Mkurungezi wa Jiji la Arusha; wanataka liongozwe na Kaimu Mkurugenzi mpaka lini?
   
 11. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,734
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  jamani hawa wakurugenzi wa wilaya kwanini wasipewe hadidu za rejea na mkataba wa miaka mitatu kama akichemsha piga chini kuliko utaratibu wa sasa unawafanya wanakuwa miungu watu?
   
 12. m

  mchaichai JF-Expert Member

  #12
  Jun 22, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 650
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimefurahishwa sana na hili la arusha ni mwizi kweli alikuwa hutu yaani nimefurahi sana maana alifikia mahali pa kupinga ukweli na akiona wanakaribia kumfikia alifanya kila njama hadi akasababisha fifo vya watu wafuasi wa chadema pale alipochakachua matokeo ya uchaguzi wa maya wa manispaa ya Arusha
   
 13. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #13
  Jun 22, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kiini macho tu hicho.
   
 14. t

  thatha JF-Expert Member

  #14
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  we mwehu sana ww,unadhani ni sumbawanga hapa ambapo waumini wa kanisa waliokuwa wanaipinga chadema walivuliwa uumini.acha uchochezi.
   
 15. t

  thatha JF-Expert Member

  #15
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Ni mwanzo mzuri sana.
   
 16. M

  Mbogo Junior Senior Member

  #16
  Jun 22, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hali ya udini sasa imeshamiri sana.
   
 17. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #17
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ng`wanakidiku Mkuu, umekusudia nini katika dhana yako ya harufu ya udini na Uislamu. Mimi kwa mtazamo wangu finyu, kwanza jina halimaanishi dini, pili tuseme ndio hivyo ulivyodhani wewe, kwenye orodha ya watu 14 (hapa wametajwa 13 tu), je 7 kwa 7 ni udini?
   
 18. Nzenzu

  Nzenzu JF-Expert Member

  #18
  Jun 22, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Imekula kwake! Yule Chang'a alikuwa anakaimu kwani?
   
 19. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #19
  Jun 22, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Mbunda alikuwa safi ktk kampeni batilda akalalamika kuwa u fair anaoufanya mbunda unammaliza,akaondolewa kabla ya uchaguzi..ktk hii orodha ya walotemwa yupo kikafara kafara tu.
   
 20. m

  mkurugenz JF-Expert Member

  #20
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  wanagawana ulaji no new there
   
Loading...