GEITA: Serikali yatenga zaidi ya Sh. Bilioni 6 za kuchimba visima Chato!

Azim Sokoine

JF-Expert Member
Aug 20, 2014
1,379
2,533
Habari wakuu,

Serikal ya JPM imetenga zaid ya bilion 6 kuchimba visima na kusambaza maji kutoka ziwa victoria wilayani Chato mkoani Geita

Source: ITV

=======

maji(18).jpg


Serikali imetenga fedha zaidi ya shilingi bilioni sita kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji mijini na vijijini katika wilaya ya Chato mkoa wa Geita kwa kuchimba visima virefu 30 na kuvuta maji kutoka Ziwa Victoria kwa lengo la kuwapunguzia wananchi adha ya kutembea umbali mrefu kati ya kilometa 5 hadi 10 na wengine wakipoteza maisha kwa kuliwa na mamba wakisaka maji kandokando ya Ziwa Victoria.

Amebainisha hayo Mbunge wa Jimbo la Chato ambaye pia ni Naibu Waziri wa nishati na madini Dkt Medadi Kalemani wakati akizindua mradi wa maji ya kisima kirefu kilichochimbwa katika kijiji cha Buzirayombo ambacho kinakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji safi na salama kama anavyobainisha diwa wa kata ya Bukome Bi.Thereza Sibngh wakati akimkaribisha mbunge huyo.

Baada ya kutembelea mradi wa maji Buzirayombo Naibu Waziri wa nishati na madini dkt Medadi kalemani mbunge wa Chato amezindua ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana emau katika kijiji cha Itale huku akiwahakikishia wananchi kuwasambazia nishati ya umeme kila kitongoji kwa lengo la kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika wilaya ya Chato iliyosheheni rasilimali za kutosha huku viongozi wa shule ya Emau wakibainisha changamoto zilizopo katika sekta ya elimu.


Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom