Serikali yatenga ml. 30 kwa chai na bil. 20 kwa masofa ya wakubwa@ yr, je ni haki

Chamkoroma

Senior Member
Sep 6, 2010
186
11
Wapenda wenzangu wana wa ukweli na uwazi, serikali kutenga bil 20.3 kwa jali ya anasa wakati wanafunzi wa shule za serikali bado wanakaa kwenye mawe na wengine chini ya mwembe au chini ya tembe tuwafanye nini hao wanaokula nchi kama chatu anayekula mbwa kwa mbwa kumkimbilia badala ya kukimbia? Jamani tukubali tusikubali mwisho mwema utaletwa na wa TZ wenye uchungu wa kweli wakijua wazi kuwa kura yako ni ukombozi wa Taifa lako, kwa pamoja kwa umoja tutashinda, lkn tukiwaangalia usoni nakuwaona kama ndugu zetu maisha yetu na ndugu zetu yataendelea kuwa mambaya sn.
 
Mkuu tunaomba utuwekee source ya data zako ili hata tukitaka kutumia hoja hiyo tuwe na nguvu.
 
Ndio hapa sasa tujitahidi TUKAPIGE kura siku hiyo ya uchaguzi,hamasisha MAMA yako,BABA yako,WAJOMBA na SHANGAZI zako wote wapige kwa watu unaofikiria wanaweza kuona vipi ni VIPAUMBELE na sio hanasa tuuuuu zisokua na mwisho,manake STAREHE haziishi bwana,ukiamua kila siku inaweza kua sikukuu tu au vipi.
 
Sio haki! Ndio maana unapaswa kuichagua CHADEMA - Udiwani, Ubunge na Urais! La sivyo kaa kimya uwaache WATANUE na ufisadi wao! Tumeelewana?
 
data muhimu ndugu,umetoa wapi taarifa?usije ukatupeleka chaka

nimewahi kuona taarifa ya Ofisi ya mbunge ambaye ni spika aliyemaliza muda illiyokaabatiwa kwa gaharama kubwa za ajabau.

Inashanganza mbunge wa urambo mkoa wa tabora ambako kuna mbao za miti migumu anakosa creativity kama si idea ya busara kusema japo viti vya wageni viwe supplied within wilaya kama si mkoa.

Ofisi ya mbunge inaagiza thamani na viti mpaka vya kukalia wageni kutoka dar na Dar nao wanaagiza kutoka china sio keko . Kama wabunge hawaonyeshi kwa vitendo kussuport bidhaa za ndani nani awe mfano?

Kuna vitu vingine ingawa ni vidogo vidogo can make +ve difference. Lakini hawa jamaa hawavioni.
 
Back
Top Bottom