Serikali yatatua kero ya maji Maili Moja

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
2,000
Wananchi wa Maili Moja, mtaa wa Muheza, Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani wameishukuru serikali kwa kumaliza kero ya maji iliyokuwa ikiwakabili kwa muda mrefu.

Furaha ya wananchi hao ilionekana wakati wa mahojiano maalum mwisho wa wiki iliyopita. Wengi wa wananchi waliohojiwa wameonyesha kufurahishwa na juhudi za serikali kuwapatia wananchi wa eneo hilo huduma ya maji safi na salama na wamempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa kutatua kero ya maji iliyokuwa inawakabili kwa muda mrefu.

"Kabla ya mradi huu kukamilika tulikuwa tukitembea umbali mrefu kutafuta maji ambapo tulikuwa tunalazimika kuamka saa nane za usiku na kurudi saa mbili asubuhi lakini kwa sasa tumesogezewa huduma ya maji karibu na makazi yetu tena kwa gharama ndogo," amesema Zawia Salum.

Filemoni Shila, mkazi wa siku nyingi eneo hilo amesema kusogezwa karibu huduma ya maji kwenye makazi yao kumesaidia kupata muda wa kufanya shughuli za kuwaingizia kipato ambapo kabla ya kuwepo mradi huo muda mwingi walikuwa wakitumia kutafuta maji.

Naye mwanafunzi wa Shule ya Msingi Maili Moja, Hamisi Salum Ally, amesema alikuwa anafuata maji mabondeni kwa ajili kufulia sare zake za shule lakini kutokana na kusogezewa huduma ya maji karibu imemsaidia kupata muda wa kujisomea.

Akizungumzia mradi huo, Mhandisi wa Maji Mji Kibaha, Grace Lyimo amesema mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa kwa wakazi wa Muheza ambapo ulikuwa na lengo la kuhudumia wananchi 911 lakini mpaka sasa unahudumia zaidi ya wananchi 2000.

"Mradi wa maji Muheza umejengwa kwa Shilingi Milioni 359 ambapo hutoa lita 100,000 kwa siku," ameongeza mhandisi Grace.

Mradi huo wa maji unaendeshwa na wananchi wa eneo hilo, ambapo hukusanya mapato ya mradi huo na kuziweka benki ambapo matumizi ya fedha hiyo ni pamoja na matengenezo madogo madogo ya mradi huo.
 
andjul

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
17,320
2,000
....Wengi wa wananchi waliohojiwa wameonyesha kufurahishwa na juhudi za serikali kuwapatia wananchi wa eneo hilo huduma ya maji safi na salama na wamempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa kutatua kero ya maji iliyokuwa inawakabili kwa muda mrefu.....

Hivi kila jambo lazima atajwe rais? Waziri wa maji hahusiki katika hili?
Nakumbuka zamani waziri wangu wa Elimu Jackson Makweta alivyokuwa anasifiwa,nakumbuka uchapa kazi wa Kawawa, alitajwa kila kona ya nchi. Kuna nini utawala huu mawaziri hawafanyi kazi zao kiasi kwamba wameshindwa kuzikonga nyoyo za wananchi?
 
kwani wakimpongeza rais kuna shida gani?pia juhudi za waziwazi za rais MAGUFULI zimeonekana kwenye jambo hili ndugu
 
DrLove69

JF-Expert Member
Jan 20, 2018
3,127
2,000
....Wengi wa wananchi waliohojiwa wameonyesha kufurahishwa na juhudi za serikali kuwapatia wananchi wa eneo hilo huduma ya maji safi na salama na wamempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa kutatua kero ya maji iliyokuwa inawakabili kwa muda mrefu.....

Hivi kila jambo lazima atajwe rais? Waziri wa maji hahusiki katika hili?
Nakumbuka zamani waziri wangu wa Elimu Jackson Makweta alivyokuwa anasifiwa,nakumbuka uchapa kazi wa Kawawa, alitajwa kila kona ya nchi. Kuna nini utawala huu mawaziri hawafanyi kazi zao kiasi kwamba wameshindwa kuzikonga nyoyo za wananchi?
Ulitaka apongezwe Mbowe na Tundu Lissu kwa kuwapelekea Maji wakazi wa Kibaha Maili moja!?
 
ccm mtoto wao

JF-Expert Member
Dec 19, 2018
564
500
Ni mambo mazuti atakayo kuyasikia jiwe maana mengine tunaambia tunachafua serikali. Nashauri wanunue na fagio watu wakiichagua wao wafagie kutoa uchafu. Na huku kwetu watulipe ela ya koro-show
Wananchi wa Maili Moja, mtaa wa Muheza, Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani wameishukuru serikali kwa kumaliza kero ya maji iliyokuwa ikiwakabili kwa muda mrefu.

Furaha ya wananchi hao ilionekana wakati wa mahojiano maalum mwisho wa wiki iliyopita. Wengi wa wananchi waliohojiwa wameonyesha kufurahishwa na juhudi za serikali kuwapatia wananchi wa eneo hilo huduma ya maji safi na salama na wamempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa kutatua kero ya maji iliyokuwa inawakabili kwa muda mrefu.

"Kabla ya mradi huu kukamilika tulikuwa tukitembea umbali mrefu kutafuta maji ambapo tulikuwa tunalazimika kuamka saa nane za usiku na kurudi saa mbili asubuhi lakini kwa sasa tumesogezewa huduma ya maji karibu na makazi yetu tena kwa gharama ndogo," amesema Zawia Salum.

Filemoni Shila, mkazi wa siku nyingi eneo hilo amesema kusogezwa karibu huduma ya maji kwenye makazi yao kumesaidia kupata muda wa kufanya shughuli za kuwaingizia kipato ambapo kabla ya kuwepo mradi huo muda mwingi walikuwa wakitumia kutafuta maji.

Naye mwanafunzi wa Shule ya Msingi Maili Moja, Hamisi Salum Ally, amesema alikuwa anafuata maji mabondeni kwa ajili kufulia sare zake za shule lakini kutokana na kusogezewa huduma ya maji karibu imemsaidia kupata muda wa kujisomea.

Akizungumzia mradi huo, Mhandisi wa Maji Mji Kibaha, Grace Lyimo amesema mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa kwa wakazi wa Muheza ambapo ulikuwa na lengo la kuhudumia wananchi 911 lakini mpaka sasa unahudumia zaidi ya wananchi 2000.

"Mradi wa maji Muheza umejengwa kwa Shilingi Milioni 359 ambapo hutoa lita 100,000 kwa siku," ameongeza mhandisi Grace.

Mradi huo wa maji unaendeshwa na wananchi wa eneo hilo, ambapo hukusanya mapato ya mradi huo na kuziweka benki ambapo matumizi ya fedha hiyo ni pamoja na matengenezo madogo madogo ya mradi huo.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
andjul

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
17,320
2,000
Ulitaka apongezwe Mbowe na Tundu Lissu kwa kuwapelekea Maji wakazi wa Kibaha Maili moja!?
Hao ulio wataja ndio mawaziri wa wizara husika? Unadhani wote tunao hoji ni upinzani? Pevuka ubongo wako
 
DrLove69

JF-Expert Member
Jan 20, 2018
3,127
2,000
Hao ulio wataja ndio mawaziri wa wizara husika? Unadhani wote tunao hoji ni upinzani? Pevuka ubongo wako
CRDB Ilipokuwa inafanya Vizuri kuna siku hata moja ulisikia anasifiwa branch manager au Operation Manager!? Sifa zote alikuwa anabeba Dr. Charles Kimei. Na ndivyo ilivyo hapa. Kama unateseka Kufa.
Pathetic!
 
andjul

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
17,320
2,000
CRDB Ilipokuwa inafanya Vizuri kuna siku hata moja ulisikia anasifiwa branch manager au Operation Manager!? Sifa zote alikuwa anabeba Dr. Charles Kimei. Na ndivyo ilivyo hapa. Kama unateseka Kufa.
Pathetic!
Kitangaze chama chako sio jina la kiongozi. Tukiwa nje ya nchi yetu Tanzania ndilo jina linakuwa midomoni mwetu,sio chama wala jina la kiongozi wa nchi. Mkapa aliwatahadharisha kuhusu suala hilo(dakika ya 19-20) kwa sababu lina madhara.Wakuzeni kwa kuwatangaza mawaziri wenu kwa kazi nzuri wanazozifanya maana ndio marais wajao.

Rejea ushauri wa Mkapa dakika ya 19

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom