Serikali yatangaza utaratibu ununuzi korosho msimu huu

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
1569062399985.png

SERIKALI imesema wanunuzi wa korosho msimu huu watatakiwa kujisajili kwenye Bodi ya Korosho kupitia mfumo wa Wizara ya Kilimo wa kusimamia biashara za kilimo (ATMIS).
Vilevile, imeeleza inadaiwa na wakulima wakubwa wa korosho Sh. bilioni 50 kutokana na kununua korosho zao msimu uliopita.

Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, alipozungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam. "Msimu wa 2019/2020 mfumo wa ununuzi wa korosho utakuwa kwa njia ya mnada wa wazi kwa kutumia Jukwaa la Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), hakutakuwa na matumizi ya masanduku ya mnada," Waziri Hasunga alisema.

Aliongeza kuwa wanunuzi watakaosajiliwa na kukidhi vigezo watatakiwa kulipa Kinga ya Dhamana kutegemeana na kiasi cha korosho mnunuzi anachotaka kununua kupitia kwenye akaunti ya usuluhishi inayomilikiwa na Soko la Bidhaa. "Mfumo huu utaruhusu wanunuzi mbalimbali kutoka maeneo mbalimbali duniani kushiriki katika mnada.

Wanunuzi wa nje ya nchi wataweza kushiriki katika mnada moja kwa moja na hawatalazimika kufungua kampuni nchini," alisema. Waziri huyo alisema wanunuzi hao watadhaminiwa na benki za malipo (Settlement Bank) zinazotambuliwa na Soko la Bidhaa (TMX) hivyo kuongeza ushindani katika minada.

kwa mujibu wa taratibu za soko," alisema. Hasunga alibainisha kuwa wanunuzi wa ndani na nje ya nchi wataruhusiwa kununua korosho ghafi kwa mafungu kati ya tani 50 na tani 500 kulingana na mahitaji. "Korosho hizo katika mafungu zitapangwa kulingana na vigezo vya ubora na daraja.

Kiwango cha korosho kitakachouzwa katika kila kikao (mnada) kitatokana na taarifa zilizopo katika katalogi ya mauzo," alisema. "Mnunuzi atalazimika kununua kiasi chote cha korosho kilichoko katika fungu katika kikao kimoja ili kuwezesha utoaji wa korosho katika ghala kwa kutumia utaratibu wa korosho za kwanza kuingia ndizo za kwanza kutoka (first in, first out- FIFO)," alifafanua.

Alisema wanunuzi wenye leseni watapewa msimbo (code) maalum wataoutumia kuingia kwenye mfumo na kushiriki katika minada. Alisema mnunuzi atakayeshinda katika mnada atawajibika kulipia korosho alizoshinda ndani ya siku tatu baada ya mauzo kufanyika.

Waziri Hasunga alisema lengo la utaratibu huu mpya ni kupanua wigo wa soko ambao wanaamini utaongeza chachu ya ushindani na kuwezesha bei nzuri zaidi kupatikana kulingana na mwenendo katika soko la dunia. "Msimu wa ununuzi wa korosho Mwaka 2019/2020 kwa sasa umefunguliwa rasmi. Katika msimu wa 2019/2020, tunategemea kuzalisha tani 300,000 za korosho ghafi kutoka tani 224,000 zilizozalishwa 2018/2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 34," alisema.

Alisema Wizara yake kupitia Bodi ya korosho imeongeza maeneo mapya yanayolima korosho kutoka mikoa mitano ya awali ambayo ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Tanga na kufikia mikoa 17. Mikoa mingine inayolima korosho kwa sasa ni Dodoma, Singida, Tabora, Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Katavi, Morogoro, Songwe, Kigoma, Njombe na Shinyanga," alisema.

Katika musimu wa mwaka 2018/2019 serikali iliamua kununua korosho zote toka kwa wakulima kutokana na kuyumba kwa bei ya korosho katika soko la minada. "Hatua hii ilikuwa ni ya dharura iliyochukuliwa ili kulinda maslahi ya mkulima, kuanza mkakati wa kubangua korosho zote hapa nchini, kufufua viwanda vya kubangua korosho vilivyopo na kuongeza ajira kwa Watanzani," alisema.

Wazir kuu tunataka utuambie kwa nn TAMISEMU haiwapandish madaraja wafanyakaz ili ninyi mnatembelea magar mazuri mnavaa vizuri weupe na weus unang'aaa? Make huku tukiwauliza MAFISA UTUMISHI wanatujib kuwa taarifa zote ziko TAMISEMI na hawajui kwa nn hampandishwi hata wao wataman tupandishwa lkn serikali iko kimyaaaa. Axhen roho mbaya akina Majaliwa ba Jaffo.
 
Wao ccm waliweka au kununua kinga ya dhamana walipotaifisha korosho za wafanya biashara?! Kama walifanya hivyo mbona hawalipi deni hilo la zaidi ya Tsh 50 bilioni?!
Msimu huu nao watazinunua wao ccm tu, au la waache wanunuzi wa korosho kama walivyo wakuta.
 
mh hii process mbona ndefu sana?,yaani inabidi kwenda semina kabisa,,Mr masunga punguza mlolongo
 
Lengo zuri kumsaidia mkulima apate hela nyingi direct

Lakini wameshafanya Utafiti na kuangalia options tofauti tofauti iwapo plan yao haitafanya kazi?.
Je wana plan. B, Plan C na kuendelea?

Lakini pia utaratibu wao huu unaondoa Kangomba, lakini Kangomba ni Mtanzania, kupitia korosho anapata rizki na anatoa ajira pia, Huwezi kumuondoa Kangomba abruptly namna hii ukadhani unasolve tatizo

Kangomba alitakiwa atungiwe sheria, kumsaidia akue, maana Kangomba wa leo ndiyo mfanyabiashara mkubwa wa korosho wa kesho!

Halafu Wizara ni kama haijui reality za Watanzania masikini huko vijijini, Huko vijijini korosho ndiyo chumvi ndiyo sukari, ndiyo dela kwa akina mama, ndiyo ngoma ya kumcheza mwali sasa Kangomba huweza kuprovide pesa in advance kumsaidia mkulima huyu kukidhi haja zake in exchange ua kulipwa korosho msimu ukifika, Sasa kwa nini uweke mazingira ya kumuondoa huyu Kangomba?

Kangomba ni rafiki wa mkulima siyo adui
 
View attachment 1212792

SERIKALI imesema wanunuzi wa korosho msimu huu watatakiwa kujisajili kwenye Bodi ya Korosho kupitia mfumo wa Wizara ya Kilimo wa kusimamia biashara za kilimo (ATMIS).
Vilevile, imeeleza inadaiwa na wakulima wakubwa wa korosho Sh. bilioni 50 kutokana na kununua korosho zao msimu uliopita.

Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, alipozungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam. "Msimu wa 2019/2020 mfumo wa ununuzi wa korosho utakuwa kwa njia ya mnada wa wazi kwa kutumia Jukwaa la Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), hakutakuwa na matumizi ya masanduku ya mnada," Waziri Hasunga alisema.

Aliongeza kuwa wanunuzi watakaosajiliwa na kukidhi vigezo watatakiwa kulipa Kinga ya Dhamana kutegemeana na kiasi cha korosho mnunuzi anachotaka kununua kupitia kwenye akaunti ya usuluhishi inayomilikiwa na Soko la Bidhaa. "Mfumo huu utaruhusu wanunuzi mbalimbali kutoka maeneo mbalimbali duniani kushiriki katika mnada.

Wanunuzi wa nje ya nchi wataweza kushiriki katika mnada moja kwa moja na hawatalazimika kufungua kampuni nchini," alisema. Waziri huyo alisema wanunuzi hao watadhaminiwa na benki za malipo (Settlement Bank) zinazotambuliwa na Soko la Bidhaa (TMX) hivyo kuongeza ushindani katika minada.

kwa mujibu wa taratibu za soko," alisema. Hasunga alibainisha kuwa wanunuzi wa ndani na nje ya nchi wataruhusiwa kununua korosho ghafi kwa mafungu kati ya tani 50 na tani 500 kulingana na mahitaji. "Korosho hizo katika mafungu zitapangwa kulingana na vigezo vya ubora na daraja.

Kiwango cha korosho kitakachouzwa katika kila kikao (mnada) kitatokana na taarifa zilizopo katika katalogi ya mauzo," alisema. "Mnunuzi atalazimika kununua kiasi chote cha korosho kilichoko katika fungu katika kikao kimoja ili kuwezesha utoaji wa korosho katika ghala kwa kutumia utaratibu wa korosho za kwanza kuingia ndizo za kwanza kutoka (first in, first out- FIFO)," alifafanua.

Alisema wanunuzi wenye leseni watapewa msimbo (code) maalum wataoutumia kuingia kwenye mfumo na kushiriki katika minada. Alisema mnunuzi atakayeshinda katika mnada atawajibika kulipia korosho alizoshinda ndani ya siku tatu baada ya mauzo kufanyika.

Waziri Hasunga alisema lengo la utaratibu huu mpya ni kupanua wigo wa soko ambao wanaamini utaongeza chachu ya ushindani na kuwezesha bei nzuri zaidi kupatikana kulingana na mwenendo katika soko la dunia. "Msimu wa ununuzi wa korosho Mwaka 2019/2020 kwa sasa umefunguliwa rasmi. Katika msimu wa 2019/2020, tunategemea kuzalisha tani 300,000 za korosho ghafi kutoka tani 224,000 zilizozalishwa 2018/2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 34," alisema.

Alisema Wizara yake kupitia Bodi ya korosho imeongeza maeneo mapya yanayolima korosho kutoka mikoa mitano ya awali ambayo ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Tanga na kufikia mikoa 17. Mikoa mingine inayolima korosho kwa sasa ni Dodoma, Singida, Tabora, Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Katavi, Morogoro, Songwe, Kigoma, Njombe na Shinyanga," alisema.

Katika musimu wa mwaka 2018/2019 serikali iliamua kununua korosho zote toka kwa wakulima kutokana na kuyumba kwa bei ya korosho katika soko la minada. "Hatua hii ilikuwa ni ya dharura iliyochukuliwa ili kulinda maslahi ya mkulima, kuanza mkakati wa kubangua korosho zote hapa nchini, kufufua viwanda vya kubangua korosho vilivyopo na kuongeza ajira kwa Watanzani," alisema.

Wanadaiwa bilioni 90 baada ya kununua... au baada ya kukopa?
 
Lengo zuri kumsaidia mkulima apate hela nyingi direct

Lakini wameshafanya Utafiti na kuangalia options tofauti tofauti iwapo plan yao haitafanya kazi?.
Je wana plan. B, Plan C na kuendelea?

Lakini pia utaratibu wao huu unaondoa Kangomba, lakini Kangomba ni Mtanzania, kupitia korosho anapata rizki na anatoa ajira pia, Huwezi kumuondoa Kangomba abruptly namna hii ukadhani unasolve tatizo

Kangomba alitakiwa atungiwe sheria, kumsaidia akue, maana Kangomba wa leo ndiyo mfanyabiashara mkubwa wa korosho wa kesho!

Halafu Wizara ni kama haijui reality za Watanzania masikini huko vijijini, Huko vijijini korosho ndiyo chumvi ndiyo sukari, ndiyo dela kwa akina mama, ndiyo ngoma ya kumcheza mwali sasa Kangomba juweza kuprovide pesa in advance kumsaidia mkulima huyu kukidhi haja zake in exchange ua kulipwa korosho msimu ukifika, Sasa kwa nini uweke mazingira ya kumuondoa huyu Kangomba?

Kangomba ni rafiki wa mkulima siyo adui
Hawa maccm? Siku wakija na plan b au c hapo tutakuwa na taifa lenye kujitambua...
 
View attachment 1212792

SERIKALI imesema wanunuzi wa korosho msimu huu watatakiwa kujisajili kwenye Bodi ya Korosho kupitia mfumo wa Wizara ya Kilimo wa kusimamia biashara za kilimo (ATMIS).
Vilevile, imeeleza inadaiwa na wakulima wakubwa wa korosho Sh. bilioni 50 kutokana na kununua korosho zao msimu uliopita.

Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, alipozungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam. "Msimu wa 2019/2020 mfumo wa ununuzi wa korosho utakuwa kwa njia ya mnada wa wazi kwa kutumia Jukwaa la Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), hakutakuwa na matumizi ya masanduku ya mnada," Waziri Hasunga alisema.

Aliongeza kuwa wanunuzi watakaosajiliwa na kukidhi vigezo watatakiwa kulipa Kinga ya Dhamana kutegemeana na kiasi cha korosho mnunuzi anachotaka kununua kupitia kwenye akaunti ya usuluhishi inayomilikiwa na Soko la Bidhaa. "Mfumo huu utaruhusu wanunuzi mbalimbali kutoka maeneo mbalimbali duniani kushiriki katika mnada.

Wanunuzi wa nje ya nchi wataweza kushiriki katika mnada moja kwa moja na hawatalazimika kufungua kampuni nchini," alisema. Waziri huyo alisema wanunuzi hao watadhaminiwa na benki za malipo (Settlement Bank) zinazotambuliwa na Soko la Bidhaa (TMX) hivyo kuongeza ushindani katika minada.

kwa mujibu wa taratibu za soko," alisema. Hasunga alibainisha kuwa wanunuzi wa ndani na nje ya nchi wataruhusiwa kununua korosho ghafi kwa mafungu kati ya tani 50 na tani 500 kulingana na mahitaji. "Korosho hizo katika mafungu zitapangwa kulingana na vigezo vya ubora na daraja.

Kiwango cha korosho kitakachouzwa katika kila kikao (mnada) kitatokana na taarifa zilizopo katika katalogi ya mauzo," alisema. "Mnunuzi atalazimika kununua kiasi chote cha korosho kilichoko katika fungu katika kikao kimoja ili kuwezesha utoaji wa korosho katika ghala kwa kutumia utaratibu wa korosho za kwanza kuingia ndizo za kwanza kutoka (first in, first out- FIFO)," alifafanua.

Alisema wanunuzi wenye leseni watapewa msimbo (code) maalum wataoutumia kuingia kwenye mfumo na kushiriki katika minada. Alisema mnunuzi atakayeshinda katika mnada atawajibika kulipia korosho alizoshinda ndani ya siku tatu baada ya mauzo kufanyika.

Waziri Hasunga alisema lengo la utaratibu huu mpya ni kupanua wigo wa soko ambao wanaamini utaongeza chachu ya ushindani na kuwezesha bei nzuri zaidi kupatikana kulingana na mwenendo katika soko la dunia. "Msimu wa ununuzi wa korosho Mwaka 2019/2020 kwa sasa umefunguliwa rasmi. Katika msimu wa 2019/2020, tunategemea kuzalisha tani 300,000 za korosho ghafi kutoka tani 224,000 zilizozalishwa 2018/2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 34," alisema.

Alisema Wizara yake kupitia Bodi ya korosho imeongeza maeneo mapya yanayolima korosho kutoka mikoa mitano ya awali ambayo ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Tanga na kufikia mikoa 17. Mikoa mingine inayolima korosho kwa sasa ni Dodoma, Singida, Tabora, Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Katavi, Morogoro, Songwe, Kigoma, Njombe na Shinyanga," alisema.

Katika musimu wa mwaka 2018/2019 serikali iliamua kununua korosho zote toka kwa wakulima kutokana na kuyumba kwa bei ya korosho katika soko la minada. "Hatua hii ilikuwa ni ya dharura iliyochukuliwa ili kulinda maslahi ya mkulima, kuanza mkakati wa kubangua korosho zote hapa nchini, kufufua viwanda vya kubangua korosho vilivyopo na kuongeza ajira kwa Watanzani," alisema.

acha maneno mengi wewe mh. waziri tunadai za mwaka jana hazijalipwaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom