Serikali yatangaza Sh 58bn kila wilaya za "Kilimo Kwanza"

Mpogoro

JF-Expert Member
Dec 7, 2008
386
58
Nimesoma habari yenye kichwa cha "Serikali yatangaza Sh 58bn kila wilaya za Kilimo Kwanza" kwenye gazeti la Mwananchi leo na inasema kiasi hiko cha pesa kitatumika kwa ununuzi wa magari,pikipiki na baiskeli zitakazotumika katika utendaji wa kazi za maofisa wa kilimo mashambani.

Napata kigugumizi kidogo maana kiasi hiko cha pesa ni kikubwa sana na najaribu kuangalia programu hii ambayo imekuja hivi karibuni inapata msukumo huu mkubwa na kuacha programu nyingine zikiwa zimelala....serikali hii inayomwaga pesa hizi kwenye kilimo kwanza mbona imeshindwa kuweka pesa katika ujenzi wa maktaba na maabara katika kila shule ya sekondari iliyojengwa kwa nguvu za wananchi.

Nashawishika kuona kuwa pesa katika nchi inapatika ku-finance programu ya kiserikali kama kunakuwa na msukumo fulani wa kisiasa...sioni kwa nini tuna kawaida ya kufanya vitu nusu nusu na tunachukuliwa na upepo kitu kipya!

Je,ni kweli hizi pesa zitatumika kununua hivi vitu wanavyosema?Na,je kuwepo kwa magari,pikipiki na baiskeli kwa ajili ya wataalamu wa kilimo kutaleta mapinduzi ya kilimo?Tunaponunua hivi vitu na maslahi ya mtaalamu wa kilimo yakabaki kuwa ya chini na wataalamu wangapi watakubali kuendelea kufanya mashambani tu kwasababu kuna magari?

Nielewesheni jamani ila kwangu mimi naona hili suala la kilimo kwanza mmh....I am skeptical!
 
Mbona pesa hizo ni zaidi ya pesa za budget ya mwaka 2009/2010 kwa wilaya zote tanzania au ni waandishi makanjanja.

Mikoa 25 x wilaya 5 kila mkoa x 58 billion=7.2 trillion
 
Sawa wakulima watalima sana mwaka huu.

Je serikali inawahakikishia wakulima kupata soko la uhakika la mazao yao?

Je serikali itaacha tabia yake ya kuzuia wakulima kupeleka mazao yao nje ya nchi ambako kuna bei nzuri ya mazao kuliko wanayopata hapa nchini?
 
Hiyo sera ya kilimo kwanza imezingatia tatizo la mvua kwa baadhi ya maeneo ya nchi? Na je imejiandaa vipi kukabiliana na hili tatizo, namaanisha kuna mikakati yoyote ya uboresha kilimo cha umwagiliaji kuliko kutegemea mvua kila mwaka?
 
Kwa maoni yangu nadhani Tz ina matatizo mengi katika kila sekta (including agricultural sector) na fedha zilizopo haziwezi kutatua matatizo yote katika sekta hii.

Tukiongeza mabwana/mabibi shamba bila kuongeza uzalishaji wa mbolea hatujafanya chochote. Tukiongeza uzalishaji wa mbolea huku tukitegemea mvua bado njaa itatufika. Tukijenga barabara hadi mashambani bila kuwa na large scale farmers ni kazi bure na ni hasara. Tukiwapa wakulima vitendea kazi wakaongeza uzalishaji bila kuwapa market guarantee tumefulia. Tukiongeza uzalishaji bila kuwekeza katika utunzaji wa nafaka napo tumeula wa chuya. Tukiwanunulia magari maofisa wakilimo bila barabara za kwenda huko mashambani tumekula hasara.

Kwa hivyo basi piece-meal approach kwenye sector ya kilimo haiwezi kuzaa matunda, na resource tulizonazo hazitoshi kuchukuwa a wholesale approach.
 
Back
Top Bottom