Serikali yatangaza Operesheni Kamata Makahaba na wateja wao

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetangaza kuiunga mkono Polisi nchini katika operesheni ya kukamata wateja wa makahaba kuhakikisha biashara hiyo inakoma nchini.

Waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu alisema takwimu zinaonesha wanawake ndio waathirika wakubwa wa ugonjwa wa Ukimwi, ambapo kati ya Watanzania 10 wanaopimwa, sita ni wanawake na wanaume ni wanne pekee.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Dar es Salaam jana, Ummy alisema si haki kuwakamata wanawake wanaojiuza na kuwaacha wateja wao ambao ni wanaume.

“Ninalipongeza Jeshi la Polisi kwa hatua hiyo kwa sababu imeonesha kutoegemea upande mmoja kwa kuwakamata wanawake makahaba. Wote wanaojiuza na wanaonunua huduma hiyo ni wakosaji wanaostahili kuchukuliwa hatua za kisheria.Tunaungana na Polisi kushiriki operesheni hiyo,” alisema.

Alieleza kuwa, biashara ya ukahaba inayofanywa na wanawake isingekuwepo endapo wateja wasingekuwepo, hivyo, wateja wanastahili kukamatwa pia kwa sababu ndio wanaoichochea.

Ummy alisema familia nyingi zina misukosuko na wanawake wengi wamekuwa wakiteseka na wengine kuambukizwa magonjwa na waume zao wanaoshiriki biashara hiyo.

Katika hatua nyingine, alisema sasa wanataka kuona idadi ya wanaume wateja wa biashara hiyo inatajwa sambamba na ya wanawake wanaokamatwa nao ili ndugu na wake zao wafahamu kuhusu tabia yao hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki, alisema hatua ya kukamata wateja na wauza miili imetokana na makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Dar es Salaam.
 
vijiwe vya bakulutu mbona vitakufa, na mkishawakamata mutawashitaki kwa kosa gani? umkute binti kasimama kando ya bar umkamate tu kisa munasaka machangudoa, sie tunaokwenda kuangalia laliga bar ndo tutajikuta tuko lupango bure.
 
1. Wanawake wanauza miili yao kwa kufanya ukahaba,
2. Ilikuwa siku ya wanawake,
3. Wanawake katika siku hiyo hujidai kutaka haki sawa/sawa na kushindana na wanaume (kinyume cha neno la Mungu),
4. Kwa kuhalalisha hilo, Mwanamke aliye waziri anaagiza wanaume (wateja) wa biashara ya mwanamke (ukahaba) wakamatwe,
5. Ya kwamba hakuna biashara bila wateja!!!!

Na mimi namuuliza, Je! Kuna biashara bila Product/bidhaa?!!

Kwa nini asizuie bidhaa kuingia sokoni ambayo ni primary way kuliko kuiacha halafu ukamkamate mteja?!

Wanawake bhana!
 
Biashara hiyo imeboreshwa sana siku hizi wengi wao wanaifanya kwa simu tu....Anapigiwa simu njoo mahala anaenda... Nadhani badala ya kuidhibiti wangeihalalisha na wapewe vigezo na masharti ingekuwa salama sana kuliko hivi sasa na wangekuwa wamewasaidia wote mtoa huduma na mteja wake..
 
1. Wanawake wanauza miili yao kwa kufanya ukahaba,
2. Ilikuwa siku ya wanawake,
3. Wanawake katika siku hiyo hujidai kutaka haki sawa/sawa na kushindana na wanaume (kinyume cha neno la Mungu),
4. Kwa kuhalalisha hilo, Mwanamke aliye waziri anaagiza wanaume (wateja) wa biashara ya mwanamke (ukahaba) wakamatwe,
5. Ya kwamba hakuna biashara bila wateja!!!!

Na mimi namuuliza, Je! Kuna biashara bila Product/bidhaa?!!

Kwa nini asizuie bidhaa kuingia sokoni ambayo ni primary way kuliko kuiachs halafu ukamkamate mteja?!

Wanawake bhana!
hata yesu makahaba walimshinda, aondoe kwanza grocery kwenye makazi ya watu, kwanza nchi yetu haina makahaba ina madada poa na machangudoa, makahaba wako ulaya.
 
Biashara hiyo imeboreshwa sana siku hizi wengi wao wanaifanya kwa simu tu....Anapigiwa simu njoo mahala anaenda... Nadhani badala ya kuidhibiti wangeihalalisha na wapewe vigezo na masharti ingekuwa salama sana kuliko hivi sasa na wangekuwa wamewasaidia wote mtoa huduma na mteja wake..
na huko whatsap na instagram sijui atawakamataje?
 
Huyu mama anataka kutuharibia vipozeo vya mioyo yetu, sisi tunakimbilia kwa hao kuepuka kutembea na wanafunzi na kuchukua wake za watu, ataongeza kesi za ugoni na mimba za wanafunzi, atuache tu tuendelee wakubwa kwa wakubwa
 
...badala ya kufikiria kuwasaidia makahaba....kwa maana ya kuwagawia condoms ili wajikinge na maradhi....nyie mnafikiria kuwakamata.....hiyo haitasadia..maana watafanya ukahaba wao mafichoni nyie mkiwa mmelala.....mnasahau ukahaba ni biashara kongwe duniani....watengenezeeni makahaba mazingira mazuri....ama wapeni ajira mbadala wataacha hiyo kazi.....kufukuzana nao hamtaweza...
 
Back
Top Bottom