The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 586
- 1,697
DODOMA: SERIKALI imetangaza kuvunjwa kwa mkataba tata kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Kampuni ya ROM Solutions wa zaidi ya Sh.Trilioni moja na kusema kwa kufanya hivyo hakuna hasara au madai yeyote ambayo itadaiwa kutokana na pande zote mbili kuridhia kuvunjwa kwake.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kupitia hati ya makubaliano iliyoingiwa baina ya aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Polisi na Ukoaji Thobias Andengenye kwa niaba ya Jeshi hilo na Kampuni ya Rom Solutions.
Akizungumza Machi 13 na waandishi wa habari Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene amesema hatua hiyo ilitokana na maagizo ya Rais John Magufuli aliyoyatoa ya kupitiwa mkataba huo ambapo wamebaini kuwepo na mapungufu mengi ikiwemo Kamishna kutokuwa na sifa ya kuingia mkataba huo.
“Serikali baada ya kupitia Mkataba huo uliokuwa kwa ajili ya kununua vifaa vya jeshi hilo,iliona haina haja ya kuendelea na makubaliano husika kutokana na kutokuwa na tija kwa nchi hivyo Februari 12, mwaka huu iliamua kuvunja mkataba na hakuna hasara au madai yeyote ambayo itadaiwa kutokana na pande zote mbili kuridhia,”amesema.
Mkataba huo ulisababisha kutumbuliwa kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola na aliyekuwa Kamishna wa Jeshi hilo, Thobias Andengenye.