Serikali yatangaza kutaifisha na kufuta umiliki wa ardhi yote isiyoendelezwa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Serikali imetangaza kuanza ukaguzi na kutaifisha ardhi yote iliyovamiwa ikiwemo ya maeneo ya wazi, pamoja na kufuta umiliki wa maeneo makubwa yakiwemo mashamba yasiyoendelezwa na yanayotumika kinyume na matumizi yaliyoombewa na kurudisha serikalini katika benki ya ardhi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa mradi wa wajibu wa uwekezaji katika mali na ardhi-RIPL-kwa niaba ya Katibu Mkuu, wa wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mpimaji mkuu wa serikali Bwana Nassor Duduma amesema serikali imeunda kitengo maalum cha uwekezaji ardhi kilicho chini ya kamishina wa ardhi ambacho kitazunguka nchni nzima, kikianzia mkoani Dar es Salaam na kuwataka wote waliomiliki ardhi, kinyume na taratibu, wasiondeleza wajiandae kurudisha ardhi serikalini.

Akianisha changamoto katika sekta ya ardhi nchni Mkurugenzi wa jumuiko la maliasili Tanzania Bwana Joseph Olila amesema licha ya kuwepo kwa miongozo na sheria katika sekta ya ardhi lakini bado vitendo vya uvamizi wa ardhi vinaongezeka kutokana na tatizo la elimu kwa wananchi, kwa upande wa vijijini amesema michakato wa uwekezaji hauko wazi kutokana na sheria na miongozo ya kitaifa haipelekwi katika maeneo hayo hali inayosababisha migongano.
 
Hawataweza kabisa. wataishia kuonea maskini tu....subirini mtaona. Wanaomiliki mashamba makubwa TZ ni Ma-tycoon wazito mainly wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa.

Hata maeneo mengi ya wazi ambayo ni strategically very prime yamevamiwa na haohao Ma-tycoon. Nadhani mnakumbuka jinsi nyumba ya mama Rwakatare ilivyopona ile bomoabomoa ya majuzi kati!!!!! Waliishia kubomoa nyumba za maskini tu ila kwa mama Rwakatare wakagota.
 
Sio kurudisha tu serikalini bali yanaporudi yaachwe kama maeneo wazi kwa ajili ya garden au viwanja vya michezo kwa watoto kama ni mijini.
 
Hivi tunataka kila kipande cha ardhi nchi hii kilimwe?kila mahali tuone mahindi? Kabla hujachukua kiwanja changu kwa kutokiendeleza,unajua bei ya simenti,bati na vifaa vya ujenzi?unaweza kulinganisha na mshahara wangu wa laki tatu?kwa kuwa hiyo timu inakuja na watu wanaolipwa posho ya elfu themanini kwa kwa siku na mishahara minene,njooni mtunyanganye sisi masikini halafu mkajisifu jukwaani kwamba sisi masikini ni wazembe tumeshindwa kujenga na nyinyi mungu atawalipa kadri ya uovu wenu
 
Waachane kwanza na mashamba kuna mapori Mengi hayana mtu wanaishi ndege tu,maeneo ya mijini ndio kuna usumbufu wa watu kunyang'anywa maeneo vijijini na porini hawaendi kwanini au hawapaoni?
 
Kwanini wasianze na kutoa ramani za maeneo na kuanzisha upimaji wa viwanja? Kupata hati ya ardhi imekua ngumu kumbe tuna kitengo cha upimaji?
 
1465572110110.jpg
 
Back
Top Bottom