Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Serikali imetangaza kuanzisha Mkoa mpya wa kipolisi katika wilaya za Mkuranga, Kibiti, Rufiji na Mafia ili kuimarisha usalama katika maeneo hayo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amelieleza Bunge leo Jumanne katika hutoba yake ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2017 /18
Nchemba amesema Mkoa huo utaitwa Mkoa wa Kipolisi wa Rufiji.
Kibiti kumekuwa na matukio mbalimbali ya mauaji ambayo yamegharimu maisha ya baadhi ya wananchi.