Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,159
- 3,997
Mwanza, Mganga mkuu wa Serikali, Profesa Abel Makubi amewaagiza wakaguzi wa dawa, wataalam na watumishi wote wa sekta ya afya nchini kudhibiti uuzaji, ununuzi na matumizi holela ya dawa bila cheti wala maelekezo ya daktari.
Akifungua mafunzo kwa wakaguzi wa maduka ya dawa kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo Alhamisi Desemba 10, 2020 Profesa Makubi amesema matumizi holela ya dawa bila ushauri wa daktari siyo tu inahatarisha maisha ya wananchi, bali husababisha usugu wa dawa.
“Tudhibiti matumizi holela ya dawa zinazohitaji cheti cha daktari kuokoa maisha ya wananchi na kuepuka athari za usugu wa dawa,” ameagiza Profesa Makubi.
Mganga mkuu huyo wa Serikali pia ameliagiza baraza la Famasi kukagua maduka yote ya dawa kubaini kama yamefunguliwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu na iwapo watoa huduma wana sifa za kitaaluma.
Kuhusu utendaji na uwajibikaji, Profesa Makubi ameagiza wataalam na watumishi wote wa sekta ya afya kushirikiana katika majukumu yao bila kujali wizara wanazotoka kwa sababu sekta ya afya ni moja.
“Baadhi ya watumishi wa sekta ya afya ngazi ya halmashauri wanatumia vibaya dhana ya ugatuaji wa madaraka kwa kudhani hawawajibiki kwa viongozi wa Wizara ya Afya; hii siyo sahihi kwa sababu sekta ya afya ni moja na Wizara ya Afya ndiyo msimamizi mkuu,” amesema Profesa Makubi
Akizungumzia mafunzo hayo ya siku mbili kwa wakaguzi kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Geita, Simiyu, Sinyanga na Kagera, Msajili wa Baraza la Famasi, Elizabeth Shekalaghe amesema yanalenga kukumbushana maadili, majukumu na uwajibikaji kazini.
Washiriki wa mafunzo hayo pia wataelimishwa kuhusu kanuni mpya sita za ukaguzi, uhakiki na usimamizi wa masuala ya dawa.
Chanzo: Mwananchi