Serikali yatangaza ajira za Waalimu wa Sayansi na Hisabati kwa Shule za Sekondari

MP CHACHANDU

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
875
615
TANGAZO KWA UMMA – AJIRA WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI KWA SHULE ZA SEKONDARI.

Serikali inatarajia kuajiri walimu wa masomo ya sayansi na hisabati kwa shule za sekondari.

Ajira hii ni kwa walimu wa stashahada na shahada za mafunzo ya ualimu wa masomo ya hisabati na sayansi, waliohitimu mwaka 2015. wahitimu hao wanatakiwa kuwasilisha nakala za vyeti vyao vya elimu ya sekondari (kidato cha nne na sita) na taaluma ya ualimu (stashahada na shahada) kwa ajili ya uhakiki.

Nakala hizo ziwasilishwe kupitia barua pepe ya wizara info@moe.go.tz kuanzia tarehe ya tangazo hili hadi ijumaa tarehe 16/12/2016.

yeyote ambaye vyeti vyake havitahakikiwa hatafikiriwa katika uajiri.

Tangazo hili linapatikana pia kwenye tovuti za ofisi zifuatazo: OR-TAMISEMI, NECTA, TCU na NACTE.

imetolewa na:

Katibu Mkuu

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia


1481642329477.jpg
 
mtoa mada umethibitisha km tangazo hili linapatikana kwenye website hizo tajwa hapo juu!
 
wizara ya Sayansi, Elimu na Tchnologia....sizani kama ipo hii wizara utawala wa huyu JPM

hii mbona wizara mara ya mwisho ilikuwa utawala wa Rais Benjamini Mkapa???
 
uongo mtupu tangazo la kijinga kama hilo haliwezi kutolewa na taasisi ya serikali....
 
Kwa vile pamekosekana msemaji anayeweza kulitoa ufafanuzi wa kueleweka hili suala la ajira,wacha kila mmoja ajipime uwezo wake wa IT.Yaani kila mtu anajua kabisa akija kwa kutumia kiki ya ajira chapisho lake litabamba japokuwa anajua kbsa kuwa litakanushwa dakika chache baadae.

Ila kilichonishangaza zaidi nikuona eti latest news iliyopo kwenye tovuti ya TAMISEMI ni ya tarehe 17/02/2016 hapo ndo nimebaki mdomo wazi!!Au labda nimeona kwa makengeza?yeyote atayeona vinginevyo anaweza kunisahihisha!
 
Back
Top Bottom