Serikali yataka mradi wa maji wa Orkusementi Simanjiro kumalizika haraka

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga ameitaka kampuni ya Jandu Plumbers iliyopewa kandarasi ya mradi wa maji wa Orkusementi, Simanjiro kukamilisha kazi hiyo kama ilivyo katika mkataba.

Mhandisi Sanga ametoa maelekezo hayo baada ya kukagua mradi huo na kubaini kazi ya kuhakikisha maji yanawafikia wananchi hairidhishi.

Mradi huo ukikamilika utanufaisha zaidi ya wakazi 52,000 pamoja na mifugo.

Mradi wa Orkusementi unatekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Nchi za Kiarabu kwa nchi za Afrika (BADEA) na Mfuko wa Maendeleo wa Nchi zinazozalisha Mafuta (OFID) kupitia mkopo wa masharti nafuu kwa kiasi cha Dola za Marekani milioni 18.42.

 
Back
Top Bottom