Serikali yataka kumaliza tofauti za kisiasa Arusha kwa mazungumzo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yataka kumaliza tofauti za kisiasa Arusha kwa mazungumzo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ortega, Jan 6, 2011.

 1. Ortega

  Ortega Member

  #1
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  [​IMG]
  Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Raia Mh. Shamsi Vuai Nahodha akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao Mkuu ya Wizara hiyo jijini Dar es salaam mchana huu kuhusiana na vurugu zilizotokea jana wakati polisi walipozima maandamano ya wanachama wa Chadema mkoani Arusha jana.

  Mh. Shamsi Vuai Nahodha ametangaza kwamba katika vurugu hizo watu wawili wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa wakati wa zoezi la kuzima maandamano hayo jana.

  Ameongeza kwamba Serikali imeamua kuutatua mgogoro huo katika ya pande mbili zinazokinzana katika mkoa wa Arusha ambapo amesema njia nzuri ya kumaliza mgogoro huo ni kuwasuluhisha kwa njia ya Mazungumzo ili kuleta amani mpya katika mkoa huo.

  Katika picha kushoto ni Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema ambaye ndiye aliyetoa amri ya kutoruhusu maandamano na kuruhusu mkutano wa hadhara kuendelea huku akisisitizia kwamba jeshi la polisi litaongeza ulinzi zaidi ili kuleta amani katika mkutano huo, wakati akizungumza wa waandishi wa habari siku moja kabla ya maandamano hayo.
   
 2. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii kauli ingetangulia mwanzo pasingemwagika damu. Baada ya kumwaga damu uko zanzibar tunakushukuru kwa kuja na kasi mpya bara ya kunyonya damu za watu wanaodai haki. Tuachie Tanganyika yetu urudi kwenu Zanzibar au nenda kabisa Afghanistan ukajiunge na ndugu zako magaidi wa Alqueda. Wizara yako si ya usalama wa raia ni ya usalama wa CCM
   
 3. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Alikuwa wapi huyo 'Nahodha' mpaka meli imeenda mrama. CDM waliomba serikali iingilie kati muda mrefu wakakaa kimya hadi vijana wao wamefanya waliyokuwa wanayataka ndipo wanatoa kauli za kisiasa. Watarudisha roho za watu zilizopotea? Acha kesi ilindime kwanza ili waaibike
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hawana hata haya!
   
 5. E

  Epifania Senior Member

  #5
  Jan 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Should I call it a political talk! People are dead, people are suffering!!!!!! Hawakujua madhara ya kutumia nguvu kwa raia wasiokuwa na silaha? Nawashauri wajiuzulu kwa kushindwa kutumia madaraka yao kwa hekima.
   
 6. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Mazungumzo gani wanayoyataka wakati ndio wao wamechakachua wakidhani dola itawasaidia. Hana lolote yeye na Mwema wake wanatakiwa kujiuzulu wapishe uchunguzi wa Ocampo ama JK aunde tume ya kishkaji
   
 7. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2011
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  IGP si mwema ni katili
   
 8. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  PM Pinda alisema by 5th January wangemaliza mgogoro wa umeya Arusha ambao ndio chanzo cha yote hayo, lakini hakuna lolote!! Hii ni geresha nyingine.
   
 9. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huu ndio upuuzi ambao mtu mwenye akili timam utazidi kumuudh, yaani inamaana hadi watu wafe ndo serikali ione haja ya kukaa na kuongea ili kutatua tofauti hizi?????
  walah iko siku hawa viongozi nao watakufa vifo hivihivi wanavyo wasababishia watu wengine!
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,611
  Likes Received: 82,194
  Trophy Points: 280
  Mwinyi alijiuzulu kutokana na mauaji yaliyotokea kule Shinyanga. Huyu Nahodha na wahusika wote wa haya mauaji ikiwemo wakuu wa polisi na FFU wa Arusha wanatakiwa wajiuzulu haraka sana na wale wote waliokamatwa waachiwe mara moja.
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  pumbav kabisa,haya maneno si ya kuyazungumza leo,watanganyika wenzangu kwakwel miaka mitano hii ni ya chaos,unles bei ya umeme ishuke,bdhaa zshuke bei,kipato kiongezeke,naul zcpande,wez wakubwa washugulikiwe,na rais apunguze uswaiba pale juu
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nawaona hawa wawili wote wakiwa The International Criminal Court.

  Mlipewa muda mrefu na Mtoto wa Mkulima akaahidi kuwa atasuluhisha.

  Lowassa akasema pia msuluhishe mambo mapema maana Arusha siyo Tabora.

  Makamba akamwijia juu na kumwaga utumbo wake. Sasa watu wawili wamekufa na wengine kujeruhiwa.

  Kwa nini watu wasipelekewe Hague?

  SOMEBODY MUST PAY FOR THIS.
   
 13. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #13
  Jan 6, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Waliofariki RIP na kwa waliojeruhiwa tunawatakia kupona kwa haraka.
   
 14. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Hapa panaelekea kuwa na shinikizo kutoka sehemu fulani! serikali hii ninayoijua haina kauli laini kirahisi hivi!! The Dreamer nakubaliana nawe kuwa kauli kama hii ingekuwa siku moja kabla ya jana yasingetokea haya.....!!!

  Asante Shamsi kwa hili lakini too late!!

  Lakini hapa naona kuna jambo la kujadili, Hivi Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi amesema kuwa serkali imesalimu amri na kukubali kutatua mgogoro!!! fine lakini kama Waziri wa Mambo ya Ndani ana nafasi katika hili? Kimuundo mgogoro anaopaswa kuutolea tamko ni kati ya CDM na Polisi (Polisi kuuwaua wana CDM) je mgogoro wa uongozi nani atautolea tamko? (TAMISEMI? where ar u?)

  nanukuu maneno ya Solomon Malhangu, Mwanamapinduzi wa SA katika vita vya makaburu na weusi ..."Tell my people that I love them, and my blood will nourish the tree, that will bear the fruits of freedom, ALUTA CONTUNUA"

  I want to tell the Gov that, the blood of our beloved will nourish the tree that will bear the fruits of NEW TANZANIA!! Human blood, is not a joke!!!!!!
   
 15. L

  Lutifya JF-Expert Member

  #15
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 237
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  Mauji ya kijinga ya polisi ya namna hii ndio yaliyowashitua wanzanzibari mpaka wakaamua kuandaa rasmu ya mwafaka. Wamegundua kuwa Polisi ni wauaji.(kumbuka mauaji ya raia wasio na hatia Mwaka 2001). Wametuacha wabara tuhangaike na upuuzi huu wa Jeshi la Polisi. Probably Katiba mpya inaweza kututoa katika ujinga huu usio vumilika hata chembe!!
   
 16. m

  matawi JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ocampo ona hii. Ukitaka nikutafsirie niambie lakini hawa ukiwachanganya na kina William Ruto itapendeza sana. Serikali ieleze waliokufa ni kina nani na wamekufaje. Andengenye umesahau kazi yako?
   
 17. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Nahodha acha UNAFIKI. Ulikuwa wapi mpaka watu wamepoteza maisha?????

  Wewe na IGP Mwema lazima mjiuzulu kuonyesha uwajibikaji. Fuateni nyayo za Rais mstaafu Mwinyi aliyejiuzulu miaka ya 1970s kwa MAUAJI YA WATU KWA TUHUMA ZA UGANGA NA UCHAWI yaliyofanywa na Jeshi la Polisi.

  Kama kweli mko serious na kumaliza mgogoro huu kwa njia ya majadiliano/kusuluhisha kwa pande mbili yaani CHADEMA na CCM basi muanze KWA KUWAACHIA HURU VIONGOZI NA WANACHAMA WOTE WA CHADEMA AMBAO JESHI LA POLISI BADO LINAWASHIKILIA.
   
 18. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #18
  Jan 6, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Yes, that is where they belong.
   
 19. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #19
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  wanaona watu wanakufa ndio wanaleta unafiki wa kusema watakaa chini na kuongea, walikuwa wapi? waalah damu za watu waliokufa lazima zitawafata, kwani malipo ni hapa hapa duniani.
   
 20. k

  kwamagombe Senior Member

  #20
  Jan 6, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hakika ni upuuzi mtupu, watu wamekufa ndio unatoa tamko la maridhiano, wewe waziri bure kabisa, tafadhali jiuzuru kwa hiari pamaoja na IGP hatuwataki, mtaweza kuwafufua watu waliopoteza maisha, hii tanzania vipi watu wapo wapo tu wanapewa madaraka makubwa wakati hawana uwezo au utu
   
Loading...