singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
Naibu Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Jinsia Watoto na Wazee Dk Khamis Kigwangala akizungumza na Abdul Juma Ofisa Huduma wa Mpango wa wa taifa wa Damu Salama (NBTS)wakati alipotembelea katika taasisi hiyo Ilala jijini Dar es salaam na kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika katika taaisis hiyo pamoja na changamoto zinazoikabili taaisis hiyo, Katikati ni Dk. Adelin Mgasa Meneja wa Kanda ya Mashariki.
Naibu Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Jinsia Watoto na Wazee Dk Khamis Kigwangala akimsikiliza Abdul Juma Ofisa Huduma wa Mpango wa wa taifa wa Damu Salama (NBTS) wakati alipokuwa akitoa maelezo kuhusu shughuli zinazofanyika katika taaisis hiyo, kulia ni Dk. Adelin Mgasa Meneja wa Kanda ya Mashariki.
Baadhi ya wataalam wakipima damu iliyokwisha kusanywa kutoka vituo mbalimbali jijini Dar es salaam ili iweze kuchujwa na kuhifadhiwa na tayari kwa matumizi ya wagonjwa katika hospitali mbalimbali jijini Dar es salaam.
...................................................................................................................
Serikali imezitaka kila halimashauri nchini kuhakikisha kuwa inatenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya damu ili kuwezesha wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo kuipata na kuepusha kupoteza maisha ya watu hususan wakina mamawajazwazito na watu waliathirika na ajali.
Aidha Serikali imesema damu hutolewa bure, hivyo mtu yoyote atakayeuziwa damu ataoe taarifa kwa mkuu wa wialaya , mkuu wa mkoa au wizarani ili wahusika waeze kuchukuliwa hatua. Hivyo Watanzania wasikubali kutoa rushwa kwa ajili ya kupata damu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangala aliyoifanya leo katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu zilizopo jijini Dares Salaam.
Awali akitembelea ofisi hizo, Dkt Kingwangala alielezwa na Dkt . Avelina Mgasa kwamba changamoto zilizopo katika upatikanaji wa damu nchini ni halimshauri kutenga bajeti za kutosha kwa ajili ya huduma hiyo.
“ Mganga Mkuu au Mkurugenzi ambaye ahatawajika kukaikisha damu inakuwepo katika vituo vya kutolea huduma ataripotiwa kwa mmlaka zilizomteua ili ziweze kumchukulia hatua,” alisema Dkt. Kingwangala.
Dkt. Kingwangala aliitaka mifumo ya bima nchini kuhakikisha iligharamia mifuko ya kuhifadhi damu na reagent(vitenganishi) kwa wagonjwa waowalipia huduma za afya ili kuweza kusiadi changamoto inayoikabili ofisi hiyo.
Aidha Dkt. Kingwangala aliitaka ofisi hiyo kuwa na mfumo wa kieletroniki wa kuwatambua watu wanaochangia damu, kutoa taarifa jinsi damu zao zilivyookoa miasha ya wagonjwa na kuwapa motisha ili waweze kuwa wachangiaji endelevu.