Serikali yataifisha dhahabu yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 2.9

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402
Serikali imetaifisha dhahabu ya Kilogram 27.488 yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 2.9 iliyoingizwa kinyemela kutoka Kenya

Dhahabu hiyo mali ya Mfanyabiashara Bhawesh Chandulal Gandecha, ilikamatwa na Afisa Forodha katika mpaka wa Tanzania na Kenya huko Sirari, May 15, 2020

Meneja wa TRA Mkoa wa Mara, Wallace Mkande, amesema Mfanyabiashara huyo alikamatwa akitaka kuingiza dhahabu hiyo kutoka Kenya kinyemela bila kuwa na nyaraka za kuonesha amelipia ushuru

Mfanyabiashara huyo alipoulizwa alisema ameshalipa ushuru ila hajapewa stakabadhi na kuwa nyaraka nyingine zipo Dodoma huku akipiga simu kwa baadhi ya watu kuwalalamika kwa kushelewesha kuzituma

Alifunguliwa kesi Uhujumu Uchumi katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime na kushtakiwa kwa makosa ya Kuendesha Mtandao wa Uhalifu, Kufanya biashara ya dhahabu bila nyaraka muhimu na kutakatisha fedha
 
Dah! Watu wanapoteza ma billion sisi kwangu kukavu tia mchuzi ukipoteza hata 10000 unatamani hata kung'ata watu hovyo barabarani..😅

Kweli life is not fair.. nitasikitika nikiambiwa jamaa hata hajalia hata tone moja la chozi..!
 
Dah! Watu wanapoteza ma billion sisi kwangu kukavu tia mchuzi ukipoteza hata 10000 unatamani hata kung'ata watu hovyo barabarani..

Kweli life is not fair.. nitasikitika nikiambiwa jamaa hata hajalia hata tone moja la chozi..!
 
Dah! Watu wanapoteza ma billion sisi kwangu kukavu tia mchuzi ukipoteza hata 10000 unatamani hata kung'ata watu hovyo barabarani..😅

Kweli life is not fair.. nitasikitika nikiambiwa jamaa hata hajalia hata tone moja la chozi..!

Hahahhahaaha...sijawahi acha kucheka...dah..wewe nishakugawa...ninacheka hapa balaa ..dah🤣🤣🤣🤣🤣
 
Serikali ilishaagiza mtu akiingia na madini Tz aachwe ilimradi aseme pale mpakani kwa maafisa ili wamuongoze katika masoko, alichokifanya huyo mtu wa TRA ni kuharibu biashara ya watu kuleta madini nchini, akitumbuliwa ndo atatia akili
 
"KUTAIFISHA" si jambo la kujivunia hata kidogo.

Wangepigwa faini kisha walazimishwe kufuata taratibu.

Uko sahihi sio kuwafungulia kesi za uhujumu uchumi huko Ni kukimbiza watanyabiashara...

Kifupi hapo serikali imepola Mali ya mfanyabiashara. Endapo Kama aliinununua kihalali..
 
Serikali imetaifisha dhahabu ya Kilogram 27.488 yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 2.9 iliyoingizwa kinyemela kutoka Kenya

Dhahabu hiyo mali ya Mfanyabiashara Bhawesh Chandulal Gandecha, ilikamatwa na Afisa Forodha katika mpaka wa Tanzania na Kenya huko Sirari, May 15, 2020

Meneja wa TRA Mkoa wa Mara, Wallace Mkande, amesema Mfanyabiashara huyo alikamatwa akitaka kuingiza dhahabu hiyo kutoka Kenya kinyemela bila kuwa na nyaraka za kuonesha amelipia ushuru

Mfanyabiashara huyo alipoulizwa alisema ameshalipa ushuru ila hajapewa stakabadhi na kuwa nyaraka nyingine zipo Dodoma huku akipiga simu kwa baadhi ya watu kuwalalamika kwa kushelewesha kuzituma

Alifunguliwa kesi Uhujumu Uchumi katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime na kushtakiwa kwa makosa ya Kuendesha Mtandao wa Uhalifu, Kufanya biashara ya dhahabu bila nyaraka muhimu na kutakatisha fedha
Hapa sijaelewa huyu amekamatwa akiingiza dhahabu nchini (entry point) inakuwaje iwe ni magendo. Je kama angelipishwa importation duty na fine kulikuwa na kosa lipi.
 
Nadhani hii ni Kama korosho ulivyokuwa wakati serikali imetangaza kununua, zilitoka korosho kutoka Mocambique kukimbilia bei nzuri ya serikali na wakadakwa Kama wahujumu wa uchumi. Sasa kwenye dhahabu, nadhani minada ya madini na serikali kuweka akiba yake kwenye madini Kama ilivyoyanunua take ya Sainunui Laiser, imepelekea wageni kuvutiwa na soko la ndani.
Madhara ni nini?
Nadhani kutakuwa na saturation ya soko la ndani. Pia black market ya madini kwa kuwa sidhani Kama Kenya Kuna mgodi wa dhahabu.
 
Back
Top Bottom