Serikali yasitisha uuzaji Wanyama Nje: Waziri Mkuu papo kwa papo

Katika Maswali ya Papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Asubuhi ya leo Mh. Chiku Abwao CDM kamuuliza Waziri Mkuu kwa nini katika Muungano huu Zanzibar wameendelea kupeperusha Bendera yao ya Awali na ile ya Tanzania...Yaani bendera ya Tanzania na ile ya Zanzibar wakati Tanzania tunapeperusha Bendera ya Tanzania na ya Tanganyika haipeperuki tena

PM: Jibu ni jepesi tu, hayo ndio yalikuwa makaubaliano ya pande mbili wakati huo

ABWAO: Swali la Nyongeza...Huoni kama upande wa pili haukutendewa Haki katika kuruhusu pia bendera ya Tanganyika kupeperushwa?

PM: Huo ni utashi wako na unavyopenda wewe lakini utaratibu wa Kikatiba hausemi hivyo


???????????????????????????
 
Lakini bado mimi simuelewi huyu Spika! Mbunge anauliza: Mheshimiwa Spika, naomba kumuuliza Waziri Mkuu blah blah blah! Ghafla Spika anajibu! Kwani kaulizwa yeye??? Shame on her!!
 
Suala la Mabomu ya Gongo la Mboto yamejitokeza tena ambapo waziri Mkuu kaulizwa Serikali inachukua hatua gani kuhakikisha Wananchi waliopoteza maisha, Ulemavu na hasara za majengo wanapewa Fidia

PM: Tayari serikali imefanya Tathmini na inatambua hasara, uharibifu na kuanishwa wanaotakiwa kupewa Fidia na kujengewa majengo mapya. Matofali elfu ishirini na tano yameishafyatuliwa na kinachoandaliwa ni fungu la Fedha na utaratibu utakapokamilika Zoezi hilo litaanza baada ya muda si mrefu
 
KUB Mh. Mbowe.
Mh. Waziri mkuu, sasa ni miezi kumi impita tangu kuisha kwa uchaguzi mkuu. Baada ya uchauguzi kuna kesi 37 ambazo zimefunguliwa kutokana uchaguzi huo. Mh. Waziri mkuu, Kwa kuwa, Kwa mujibu sheria ya uchaguzi ni lazima kesi hizi ziishe ndani ya mwaka moja. Na kwa kuwa, Jaji mkuu ameshasema hana fedha za kuendesha kesi hizo kutokana na serikali kutompa fedha husika. Na kwa kuwa hata kama fedha hizo zitapangwa ktk bajeti hii, haiwezi kuwahi muda uliowekwa ktk sheria ya uchaguzi zilizotungwa na Bunge hili.
Je, Serikali ya inatoa Tamko gani?

Majibu, kwa kuwa hii utataratibu tuliojiwekea, serikali itafanya kila kila liwezekanalo kutimiza matakwa hayo.

Chiku abwao- Chadema
Baada ya Muungano tulikubaliana kuungana na tukaamua kupeperusha bendera moja. Lakini baadaye wazanzibar wakaruhusiwa kupeperusha bendera yao na ya muungano.
Mh. Waziri mkuu, kwa kuwa wazanzibar wamekubaliwa kupeperusha bendera yao, Kwanini Watanganyika wasipewe haki yao?

Waziri mkuu, Hivyo, ndivyo tulivyokubaliana.

Swali la Nyongeza;
Je, wewe waziri mkuu huoni kama watanganyika hawajapewa haki yao?

Waziri mkuu, Inawezekana wewe ukaona hivyo, lakini si kila mtu anaona kama wewe unavyoona.
 
MH LAIZER MICHAEL LEKULE: Ofisi ya waziri Mkuu inachukua jukumu hani kuhakikisha Wabubge wanapata Ofisi maana wabunge wengi hawana Ofisi kwa sasa
 
PM: Kabla Hajajibu
SPIKA: Bibi kiroboto anasimama na kusema jukumu hilo ni la Ofisi ya Bunge na kuwa Ramani na tathmini ya fanicha inafanyika ili kuhakikisha kuwa fanicha zinakuwa za mtindo na standard mojan kwa ofisi zote na kwamba bado lipo katika mchakato

Suala muhimu hapa ni kuhakikisha Bunge linaepukana na Ofisi Binafsi za Wabunge majumbani kwao (BRO MASHA UPO HAPO?)
 
MAUZO YA WANAYAMAPORI......

Prudencia Kikwembe: Kamuuliza Waziri Mkuu Inakuwaje serikali inaendelea kujihusisha katika biashara ya kuuza wanyama nje ya nchi huku biashara hiyo haina tija na inaendeshwa kwa misingi ya sheria?
 
Prudencia: Uhujumu unaonekana dhahiri katika biashara hii inayoendeshwa kisheria, serikali inasemaje kwa hilo?
 
PM: Anaanza kwa kung'aka...Ingependeza swali hili alijiubu waziri wa Maliasili na Utalii (MBONA GONGOLAMBOTO HUKUSEMA MWINYI AJIBU - Huyu PM Bwana)
 
Majibu: Ni eneo ambalo katioka vikao vyetu vya jana tumekubaliana kulitazama upya na Ikiwezekana tuweke mikakati mipya

Breaking News: SERIKALI IMEKUBALI KUSIMAMISHA KWA MUDA BIASHARA YA USAFRISHAJI WA WANYAMA NJE YA NCHI
 
Kwa mpango huo tunakusudia kuzipitia sheria hizo upya kabla ya kuamua kujiridhisha kuruhusu biashara hiyo na pia kutazma ni aina gani ya wanyama ambao tutaruhusu sasa kuendelea kujumuishwa katiak Biashara hii ya usafirishwaji wa wanyama Nje ya Nchi

Na pia Tozo ambalo wanatoa ni dogo mno ambalo wao wanafaidi mara mbili huku sisi tunatapata hasara.

Suala hili linashughulikiwa
 
Version unayoisoma ni Delayed LIVE kutokana na sababu zilizo nje ya Uwezo ila Hansad ya GHOST inafanya kazi zaidi ya TAPE recorder
 
Kaulizwa na Jirani yake huko Jimboni kuhusiana na Ahadi aliyoitoa ya Barabara
 
Uliahidi ujenzi wa barabara huko katika kata ambazo sikuzinasa majina kwa haraka kutokana na kidogo majina hayo ni ya kienyeji sana ...katika kipindi cha mwaka 2005 wewe mwenyewe na mpaka leo Ahadi hiyo haijatekelezeka je una majibu gani?
 
SPIKA: Bi kiroboto anaingilia kati, kwa kuwa swali hilo ni lako nan ulitoa ahadi mwenyewe basi waziri Mkuu jibu (Mhh sasa sijui alitaka kumjibia au vipi!!)
 
PM: ndugu yangu hili swali ungekuja hata kuninong'oneza ningekuelewa maana linatuhusu sote huko kwetu. Ila natambua umefanya hivyo ili wapiga kura nao wakuone na watambue kuwa unalifuatilia kwa ukaribu.

Nimeshafanya taratibu zote na nimeongea na TANROAD nao watusaidie baadhi ya maeneo maana ni sehemu ya barabara za serikali kuu, kwa hiyo Ahadi hiyo ipo na Itashughulikiwa.
 
Back
Top Bottom