Serikali yasitisha leseni ya kuchapisha na kusambaza Gazeti la Tanzania Daima kuanzia Juni 24, 2020

Serikali kupitia kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema kuwa kufuatia kusitishwa kwa lesini ya gazeti hilo, halitaruhusiwa kuchapishwa wala kusambazwa popote nchini au nje ya nchi

Serikali imebainisha kuwa uamuzi huo umetokana na kukithiri na kujirudia kwa makosa yanayokiuka sheria ya nchi na maadili ya uandishi wa habari na kuwa juhudi za kuwaonya na kuwaelekeza Wahariri wa gazeti hilo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa hazijazaa matunda

Taarifa ya Serikali inasema Mkurugenzi wa wa Idara ya Habari, amefuta leseni ya gazeti hilo ikiwa ni baada ya kulionya kwa zaidi ya mara 10 huku gazeti lenyewe likilazimika kuomba radhi mara mbili kwa uvunjifu wa maadili ya Kitaaluma na Sheria za nchi ikiwemo kuchapisha habari za uongo, uchochozi na uzandiki

Aidha, Serikali imesema kwa mujibu wa Sheria Wachapishaji wa gazeti hilo wanayo fursa ya kuomba tena leseni kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari ili kuruhusiwa kurejea tena kuchapisha na kusambaza watakapoona wamejitafakari na kuwa tayari kufuata taratibu

View attachment 1486923
Mwananchi naye ajiandae. Mwenzako akinyolewa wewe kichwani tia maji, tunaitaji kusoma magezeti ya uhuru na Mzalendo magezeti ya chama. Mungu ibariki Tanzania
 
Achana na mimi, fanya mambo yako mzee.

1592941811638.png
 
Hata wewe kwa hakilizako ambazo hujapitia uandishi wa habari! Hivi habari ya askofu bagonza kutangaza maandamano ilikuwa yakuandikwa na waandishi hodali na wasomi na baadaye kuhaririwa na wahariri wenye weredi wa tanzania daima ?
Hii ilikuwa drama ya makusudi kukwepa aibu , maana takukuru tangia waanze kuchunguza account za chadema, moja ya mianya iliyokuwa inatumiwa na chadema kuiba fedha za rudhuku za watanzania walipa kodi ni gazeti hilo.

Saivi pesa haziendi tena. Gazeti lao halinunuliwi mitaana lakini lilikuwa likichapishwa kwakutumia fedha za rudhuku kumlida mbowe na kumnufaisha maana analimiliki yeye.
Hakili-akili
Hodali- hodari
Jitahidi kurudi shule elimu ya watu wa wazima bado ipo.
 
Chadema nichama cha heche,mbowe, lema, msigwa, myika, na wale wakusagana wawili.
Wengine ndani ya chadema ni bendera fata upepo.
Sugu na mbilinyi ni wa daraja la pili.

Tafakari, chukua hatua.

Huu uzi wako umekaa kimbea mbea tu! Hata hueleweki umelenga nini hasa! Umeanza kwa kulihusisha hilo gazeti la Tanzania Daima na Takukuru!

Mara Chadema ni chama cha Heche, Mbowe, nk! Kuandika kwenyewe tu nako ni tatizo!! Mh. Mnyika unamuita myika! Hata hufahamu Sugu na Mbilinyi ni mtu huyo huyo!!

Kama kweli na wewe unalipwa buku 7 kwa siku hapo Lumumba, basi chama kinaingia hasara ya kujitakia.
 
Mh samia suruhu Ebu turudishie raha ya uhuru kwa vyombo vya habari

Life ban ya Tz daima tupia jicho la tatu na mengine mengi kurudisha mshikamano wa Taifq
 
Back
Top Bottom