Jeanclaude
JF-Expert Member
- Aug 30, 2013
- 259
- 238
Serikali kupitia kwa Naibu Waziri Elimu, Mhandisi Stella Manyanya imesisitiza marufuku yake kwa shule za Umma za msingi na sekondari, kutoza wanafunzi michango yoyote kuanzia January, 2016. Imewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kufuatilia na kuwachukulia hatua za kisheria watakaokiuka agizo hilo. Rais Dr. John Magufuli wakati anahutububia Bunge alisema anaposema bure lazima iwe bure kweli.