Serikali yasimamisha leseni ya uchapishaji na usambazaji ya gazeti la 'The Citizen' kwa siku 7

Serikali imesimamisha leseni ya uchapishaji na usambazaji wa gazeti la The Citizen kwa muda wa siku 7 kuanzia leo Jumatano, Februari 27, 2019

Gazeti hilo latuhumiwa kuchapisha taarifa za kuporomoka kwa shilingi ya Tanzania

Makala hiyo iliegemea katika kutaarufu maoni ya wataalamu juu ya mdororo huo wa shilingi

Habari hiyo ilichapishwa Februari 23 mwaka huu(2019)

View attachment 1033493



hebu imagine hatua ya kwanza ya kupambana na kuporomoka kwa shilingi ya Tanzania ni kufungia gazeti kwa siku saba....
 
We ni punguani wa unga, unaefikiri kwa makalio, nani asiyejua shilingi imeporomoka, nani asiyejua uchumi unayumba,nani asiyejua miropoko yenu imeleta tafrani kwenye korosho, kikokotoo, michanga ya madini nk.
Haya sasa, ukivaa gwanda unajiita kamanda, msomi, mzalendo, mkombozi. Ukiletewa hoja mezani unaanza matusi. Zungumza facts, unaposema shilingi imeporomoka umeangalia nini? Unaposema uchumi unayumba kwa vigezo gani n.k w.k

Sasa kama mtaweka jazba mbele, mkiandamana tutawapiga, tena tutawapiga kweli.
 
kama limeandika shilingi inaporomoka wakati kweli imeporomoka kuna kosa gani?

kuporomoka kwa shilingi hakupo gizani, kila Mtanzania anaona na/au ku feel effect yake!
INaporomoka kwenda juu au kwenda chini?
wao walipaswa kusema kuwa haiporomoki illla inaongezeka dhamani kwa kwenda chini
 
una roho ngumu sana ! hivi nyie wengine mama zenu wako madarakani au ni ushetani tu ? enzi za jk uliona jeshi likibangua korosho au kukosekana kwa ajira kwa miaka minne mfululizo ?
Usijisumbue na aina hii ya watu. Wakati wa JK dolla haikuwahi kufika shilling 2250
 
Kuporomoka kwa shilingi ni jambo moja, kutangaza kuwa shilingi imeporomoka ni jambo jingine.

Hii ni sawa na kupata VVU, na kutangazwa bila ridhaa yako kuwa una VVU.

kweli Umejibu hivyo...

Mfano wako ni dhaifu mno

Hii ni sawa na kupata VVU, na kutangazwa bila ridhaa yako kuwa una VVU
Usitolee mfano jambo la faragha ya mtu na taifa.... Tambua kuwa kuporomoka kwa shilingi kunatugusa watu wote,
kwa sisi watanzania hualisia ndio huo Shilingi imeporomoka....... labda nikuulize Au unataka kila chombo cha habari kiwe kinaandika mambo ya hadithi za kale na habari za KONKI!
 
Haya sasa, ukivaa gwanda unajiita kamanda, msomi, mzalendo, mkombozi. Ukiletewa hoja mezani unaanza matusi. Zungumza facts, unaposema shilingi imeporomoka umeangalia nini? Unaposema uchumi unayumba kwa vigezo gani n.k w.k

Sasa kama mtaweka jazba mbele, mkiandamana tutawapiga, tena tutawapiga kweli.
Leo shs vs usd ikoje
 
Back
Top Bottom