Serikali yashtukia uzito wa mzigo wa mashangingi ya viongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yashtukia uzito wa mzigo wa mashangingi ya viongozi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Sep 3, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Hili lilishazungumziwa zaidi ya miezi 12 iliyopita, lakini hakuna chochote kilichofanyika. Serikali ya kisanii imeliibua tena sijui kama sasa hivi watakuwa serious.
  Angalia hapa.

  Date::9/3/2008
  Serikali yashtukia uzito wa mzigo wa mashangingi ya viongozi
  Na Ramadhan Semtawa
  Mwananchi

  SERIKALI inafanya marekebisho makubwa ya namna ya udhibiti wa uendeshaji wa magari ya kifahari kwa mawaziri na viongozi wengine kuondokana na matumizi mabaya ya mali za umma.

  Hayo yamo katika ripoti ya Mpango wa Serikali kuhusu Orodha ya Magari yake na Kudhibiti Matumizi ambayo imependekezwa pamoja na mambo mengine magari ya kifahari ya mawaziri maarufu kama mashangingi yanunuliwe kila baada ya miaka saba badala ya miwili ya sasa.

  Utaratibu wa sasa ni kwamba, gari la waziri huweza kununuliwa kila baada ya miaka miwili tangu linunuliwe na kuanza kutumika, kisha hutumiwa na watendaji wa ngazi ya chini, au kuuzwa au waziri 'kujiuzia'.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya serikali ya mwezi Aprili 2008, ambayo gazeti hili imefanikiwa kuona nakala yake mapema wiki hii, jumla ya magari yote ya serikali nchini yamebainika ni kati ya 35,000 hadi 40,000.

  Ndani ya ripoti hiyo ambayo tayari nakala anayo Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo, kati ya orodha hiyo magari ya kifahari ya Toyota Landcruiser Vx na Gx na aina nyingine ya Landcruiser ni kati ya 10,000 hadi 15,000.

  Takwimu za sasa, gari moja aina Toyota VX au Toyota GX, hadi kuliingiza nchini ni kati ya Sh 80 hadi 120 milioni ambayo ni kwa ajili ya serikali, huku gharama za operesheni ikiwa ni pamoja na matengenezo ya kila wiki na mafuta ni kati ya Sh moja hadi 1.5 milioni, kutegemea safari.

  Ripoti hiyo ya kitaalamu ambayo inalenga kuishauri serikali namna ya kupunguza matumizi mabaya ya fedha za umma katika ununuzi na uendeshaji magari ikiwemo hayo ya kifahari, katika mapendekezo yake inaonyesha pia haja ya kupunguzwa kwa orodha hiyo ya magari kwa kiwango cha nusu.

  Katika ripoti hiyo, magari hayo 40,000 ni kuanzia Serikali Kuu na Halmashauri za Wilaya, miji, manispaa na majiji, ambayo ni pamoja na yale ya miradi maarufu kama DFP ambayo hutokana na wafadhili.

  Orodha hiyo inaonyesha sehemu kubwa ya magari hayo ni Toyota Pickup na Hard Top, ambazo zimekuwa zikitumika zaidi vijijini huku mashangingi ya Vx na Gx yakirandaranda mijini.

  Kutokana na mapendekezo ya Ripoti hiyo, chini ya mpango huo pia serikali inashauriwa kupunguza matumizi ya magari hayo ya Gx na Vx katika ngazi za Serikali za Mitaa.

  Pendekezo hilo katika ngazi ya Serikali za Mitaa, linataka Mkuu wa Mkoa pekee ndiye atumie Vx ili kuwezesha Rais anapofika aweze kulitumia huku Wakuu wa Wilaya na watendaji wengine wakitakiwa kupatiwa gari za kawaida kama Toyota Landcruiser si Vx.

  Katika mapendekezo hayo ya kitaalamu ambayo ni dira ya kupunguza matumizi mabaya ya fedha za umma, yanataka pia wakurugenzi wa wizara na watendaji wa mashirika mbalimbali na taasisi za umma, wasitumie Vx badala yake watumie magari ya kawaida.

  Iwapo Ripoti hiyo itatekelezwa, serikali itaweza kupunguza magari yake kwa kiasi cha nusu hivyo pia kuweza kuokoa mabilioni ya shilingi katika kuendesha magari hayo na ununuzi.

  Ripoti hiyo yenye kurasa zaidi ya 100, pamoja na mambo mengine imeanisha magari ya kila wizara, idara, taasisi mbalimbali ikiwemo yale ya miradi.

  Baadhi ya wizara kama Afya na Ustawi wa Jamii, zimeonekana kuwa na magari mengi makao makuu huku katika ngazi za Serikali za Mitaa kukikosekana magari ya kutosha kuhudumia wananchi.

  Pia Ripoti hiyo imeonyesha kwamba, wakati kukiwa na magari mengi makao makuu ya wizara mbalimbali, bado Jeshi la Polisi limekuwa na uhaba wa magari katika maeneo mengi nchini ikiwemo ya mipakani.

  Ripoti hiyo imekamilika wakati kukiwa na malalamiko kutoka kwa wananchi, kuhusu matumizi ya serikali katika kununua magari ya kifahari wakati nchi ni maskini.

  Kutokana na malalamiko hayo, mwaka jana serikali iliamua kuunda timu ya wataalamu ikimhusisha Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu, ili kuona na kupata ushauri wa namna bora ya kupunguza matumizi katika kununua na kuendesha magari ya kifahari na mengine bila sababu za msingi.
   
 2. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kibaya zaidi kwangu mimi magari yote haya hayana bima ( labda kama wameanza kuyakatia sasa)! Yakipata mzinga ndiyo hela imetupwa chooni!
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Hawa watu wanalipwa mishahara na marurupu makubwa, kwa nini waendelee kununuliwa magari wakati wana uwezo wa kununua magari hayo wenyewe? Wanaostahili kununuliwa magari ni Rais, Waziri Mkuu na viongozi wengine wachache ambao hawafiki hata 10 wengine wote wajinunulie magari wenyewe. Hii itapunguza gharama kubwa za uendeshaji serikalini.
   
 4. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kumbe kila baada ya miaka 2 wanaweza kununua VX/ GX nyingine ya Waziri?

  Duh ama kweli serikali yetu inajua kuchezea hela za kodi.!!!!!!!
   
 5. K

  Koba JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  magari 40,000 x 80,000,000Tshs ni sawa na 3,200,000,000,000 (3.2trillion) na budget ya Tanzania kwa mwaka ni around 4 trillions...ukiweka na matumizi ya mafuta basi hapo ni balaa,yaani huwezi amini hawa vilaza wanavyoongoza nchi na bila aibu brand new VX inaendeshwa for 2 yrs then wanajiuzia halafu walipa kodi tunanunua mpya tena,na ukizingatia hazina insurance basi inawezekana wanazigonga tuu wanajiuzia wapate mpya...yaani huwezi amini kama JK na serikali yake ni binadamu wale? wanashindwa kuwalipia wanafunzi wa udaktari Russia school fees watakaokuja kuokoa maisha ya mamilioni na wajukuu zao kumbe matumizi yenyewe ndio haya? cha ajabu hata uwaeleze vipi wananchi hii waste na ufisadi wa CCM ndio chanzo cha umaskini wao lakini wataishia kuwa vote in hao hao wanaowalalia.....nafikiri tuna deserve hii mpaka tupate akili,then guess what hata ununuzi wa hayo magari ni kutumia third party kwa wahindi wapate 10% zao,hizi deal hazina tofauti na Richmond walivyotufanya...yaani ni umafia mtupu unaendelea chini ya hawa CCM,time to wake up sasa vijana maana hawa wazee wanatuchezea akili na ndio chanzo cha umaskini,ujinga na ufukara wa hali ya juu,bila sacrifice hapa ya kupambana na hawa wazee haya ndio maisha yetu milele yatakuwa!
   
 6. T

  Tom JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2008
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Limbukeni wa magari hawa, wengi wa viongozi wetu siasa ndio biashara yao, hivyo kabla ya kua viongozi ni kwamba biashara haikuchanganya na hawakuwa na chochote, sana sana walikua na uwezo wa 10yrs second hand COROLLA. Kupata uongozi ndio imejipa na ndio muda wa kutanua na kukutambieni na mashangingi. Eti wengine wanasema VX ni gari ya kawaida? Kwa uwezo wa Tanzania gari za viongozi isizidi uwezo wa injini ya 2.5cc na zinunuliwe kila baada ya miaka sita, saba.
  Pia JK na CCM yao waache hizo, wasiwape ama wasitumie magari ya fahari ili kuloga ama kuwarubuni viongozi kuunga mkono maovu ya serikali. Bei za mafuta zimepanda weee, lakini bado wapo tu na GX, VX, akili zao hamnazo kweli kweli, eti ni pesa ya umma. Watz nao wamelogwa kweli kweli, utasikia wajomba zao wanavyowaunga mkono hao kwa hayo ma GX...
   
 7. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #7
  Sep 4, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Nadhani wengi wao vile vile wanasafiri First Class kwa ndege! Kama nimewasingizia, samahani.
   
 8. BadoNipo

  BadoNipo Senior Member

  #8
  Sep 4, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tatizo la viongozi wetu ni ulimbukeni na ushamba. Karibu viongozi wetu wote wametoka katika familia za kimaskini na wameishi maisha ya umaskini, ingebidi wao ndo wawe mfano bora lakini ndo hivyo tena.
   
 9. BadoNipo

  BadoNipo Senior Member

  #9
  Sep 4, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tatizo la viongozi wetu ni ulimbukeni na ushamba. Karibu viongozi wetu wote wametoka katika familia za kimaskini na wameishi maisha ya umaskini, ingebidi wao ndo wawe mfano bora lakini ndo hivyo tena.
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kinacho uma zaidi sijui hayo magari baada ya miaka 2 yanapelekwa wapi?wao wanachukulia kama ni chakavu tayari nahisi ndo hayo wanayo jiuzia wenyewe kwenye minada ya serikali utakuta gari bado zuri wao wanadai tayari chakavu mtu au kigogo ananunua kwa bei ya kutupwa fikiria VX mtu ananunua kwa sh.5mil.

  Bado serikali inaenda kwa kina Bush kutembeza makuli kuomba omba wakati huku nyumbani matumizi makubwa kuliko uwezo wetu gari VX jipya ndani ya miaka 2 inahesabika chakavu kigogo anabadilishiwa jipya nime mwona hata Kandoro naye kabadilishiwa V8 mpyaaaa anazunguka nayo mitaani.Uliza bei yake utakimbia na inasemekana yapo maVX 40,000 duh piga mara be i ya kununulia kifisadi fisadi si chini ya milioni 80 mara magari yote duh kweli sisi ni masikini???
   
 11. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivi mnafahamu kwamba budget ya Harvad university ni nusu ya budget ya Tanzania, sasa inakuwaje nchi masikini kama hii inashindwa hata kujua vipaumbele vyake???????
   
 12. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Tatizo tuna watawala na si viongozi. Mtawala hujali maslahi yake zaidi, lakini kiongozi hujali maslahi ya umma kwanza. Inatia moyo kama wameanza kugundua hilo, ingawa wamechelewa. Hatua zilitakiwa zichukuliwe kama miaka 15 iliyopita, leo tusingekuwa hapa tulipo.
   
 13. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  wanakumbuka shuka asubuhi hawa
   
 14. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2008
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ili kurahisisha matumizi, kwanini kusiwe na min buses kwa ajili ya viongozi? Au walau wanunuliwe RAV 4 badala ya VX, hivi karibuni nilikutana na Waziri aliyetemwa na kikwete anaendesha Escudo, nikagundua kwamba hawa viongozi wanatumia vifa vya ufahari wakati hata wo wenyewe hawadhubutu kumiliki. Gari la Waziri linatumia lita 150 kwa wiki, je hii hela haitoshi kununulia hata madawati kadhaa kwa wanafunzi wanaokaa chini?

  Kuna haja ya kupunguza ufahari, haina maana mtu mmoja kutumia gari la Milioni 150 halafu unaenda jimboni unawasaidi wananchi shilingi laki tatu kwa ajili ya kununua mabati, wakati pembeni umepaki gari la milioni 150...!

  Kweli tuta-anza-nia kwa kudanganyika.....!
   
 15. K

  Koba JF-Expert Member

  #15
  Sep 5, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ..waige Serikali ya Rwanda labda inaweza kusaidia kupunguza hizo waste!
   
 16. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #16
  Sep 5, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Hata wakijua hawa jamaa kwa kupenda ujiko na kushindana huwatoi.

  Waberoya
   
 17. selemala

  selemala Senior Member

  #17
  Sep 7, 2008
  Joined: Feb 14, 2007
  Messages: 139
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Wazo zuri. Kwa wasio na uwezo wakopeshwe. Mfumo huu unafanya kazi vizuri Rwanda!!! Kufikia hapo unahitaji kiongozi mwenye nia na mamlaka (e.g Kagame - Rwanda)
   
 18. M

  Mtu Kwao JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2008
  Joined: Jan 15, 2008
  Messages: 258
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  sIO UNADHANI NDIO HIVYO.
   
 19. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Tuache kulipa kodi kama wanazitumia bila kujali maslahi ya wananchi. Huwezi nunua magari ya kifahari na eti kila mara. Yanunuliwe kisha akiacha mtu anapewa mwingine na sio kufanya tunu ya uongozi wakati ni wito wao wamechukulia biashara. Aibu sana. Hata nchi zote mali ya serikali hutunzwa vizuri na kupita vizazi hadi vizazi na sii kila mto na nguo mpya kisha hodi hodi kuomba na kupiga mizinga nchi nyingine. Watu wenyewe magari mazuri kwa ajili ya rough roads kisha wanashinda Dar mpaka kurudi tena jimboni kampeniii!
   
 20. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #20
  Sep 8, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Ninavyofahamu mimi mawaziri wote ni wabunge kwa hiyo wamewezeshwa kujinunulia magari. Ni ubinafsi umetujaa.

  Kwa wenzetu magari yote yanakuwa kwenye pool ambapo yanatumika na kila anayeyahitaji kwa wakati huo! Kwa nini kila kiongozi aende na gari lake Dodoma badala ya kutumia gari moja.

  Na zaidi ya hayo utakuta kwenye mawizara hayo hayo WATENDAJI wanakuwa na matatizo makubwa ya usafiri hata kwenye shughuli za kiofisi. Mtendaji haruhusiwi kugusa gari la boss! Na dereva wa boss ni boss hivyo hauwezi kumwomba (?) akupeleke kwenye kikao!

  Hatufiki.................
   
Loading...