Serikali yashindwa tena kuwaleta Mahakamani watuhumiwa wa Ugaidi, yasema italihamisha shauri Mahakama Kuu

Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
33,233
8,779
SERIKALI YASHINDWA TENA KUWALETA MASHEIKH MAHAKAMANI.

Mawakili wanaowatetea Masheikh (Uamsho) walifika Mahakamani leo kama kawaida yao.

Hata hivyo serikali haikuwaleta viongozi hao wa Dini kutoka gerezani.

Shauri lilipoitwa mbele ya hakimu upande wa serikali ulidai kuwa sasa wanashughulikia kulihamishia shauri hilo Mahakama Kuu ili waanze kulisikiliza na kuthibitisha tuhuma za ugaidi wa Masheikh hao na wafuasi wao.

Pamoja na kutambua kwamba Masheikh hao wako jela kwa zaidi ya miaka sita sasa lakini hawakutaja lini shauri hilo litaanza kusikilizwa huko Mahakama Kuu.

Kwa hakika serikali ya CCM ni mtihani mkubwa kwa haki za raia.
 
Ingependa kuweka kichwa cha habari
SERIKALI IMESHINDWA KUKABIANA NA HOJA YA KESI YA KUWASINGIZIA WANANCHI WASIO NA HATIA NA BADALA YAKE INAAMUA KUHAMISHA KESJ KWENDA MAHAKAMA NYENGINE ILI KUVUTA WAKATI ZAIDI WA KUFIKIRIA NINI CHA KUFANYA.

Katika mkutano wa Membe zanzibar, alisikika akisema kuwa kama atapata ridhaa na kuwa Rais, viongozi wa uamsho atawatoa, huwenda ikawa hii serikali inayoongozwa na CCM wamestuka, na kuona kumbe watu huenda wakapata kura kupitia hawa viongozi!

Mimi naona serikali huenda wakatumia njia hii na wao wakawatoa viongozi wa uamsho ili kuzikosha nyoyo za wazanzibari. Tena huenda ikawa mwisho mwisho karibu na uchaguzi.

Sasa huenda saivi wakawa wanatafuta njia vipi wawaachie? Maana hawa watu kulichowachongea ni kutaka mamlaka kamili ya zanzibar, sasa ndio wakasingiziwa ni magaidi.
 
Mihimili yetu miwili yaani Bunge na Mahakama inachezewa mno..

Katiba imetupa mamlaka yote sisi wananchi kuhakikisha muhimili hii inafanya kazi bila shinikizo

Ni wakati wa kuamka...ewe mtanzania mwenzangu tupa blanket lako machoni kwani kushakucha...

Simama, tetea katiba yako...kama unavyotetea Biblia na Korani mtu akivichezea...katiba is the same !! Ndiyo maana akiapa anaishika!!

Lissu ndiyo jibu la haya yote!! Okoa kizazi chako sasa!! Nchi inakwenda siko.
 
Ingependa kuweka kichwa cha habari
SERIKALI IMESHINDWA KUKABIANA NA HOJA YA KESI YA KUWASINGIZIA WANANCHI WASIO NA HATIA NA BADALA YAKE INAAMUA KUHAMISHA KESJ KWENDA MAHAKAMA NYENGINE ILI KUVUTA WAKATI ZAIDI WA KUFIKIRIA NINI CHA KUFANYA.

Katika mkutano wa Membe zanzibar, alisikika akisema kuwa kama atapata ridhaa na kuwa Rais, viongozi wa uamsho atawatoa, huwenda ikawa hii serikali inayoongozwa na CCM wamestuka, na kuona kumbe watu huenda wakapata kura kupitia hawa viongozi!
Mimi naona serikali huenda wakatumia njia hii na wao wakawatoa viongozi wa uamsho ili kuzikosha nyoyo za wazanzibari. Tena huenda ikawa mwisho mwisho karibu na uchaguzi.
Sasa huenda saivi wakawa wanatafuta njia vipi wawaachie? Maana hawa watu kulichowachongea ni kutaka mamlaka kamili ya zanzibar, sasa ndio wakasingiziwa ni magaidi.

Mola awahukumie hapa hapa duniani hawa madhalimu wa CCM, Aamin
 
Jpili unakuta amepiga magoti kanisani kwa mbwembwe anajifanya mcha MUNGU
Magaidi wanatakiwa wakae ndani maisha. Nani asiyekumbuka vifo na matukio mengine yaliyotokea wakati hawa magaidi wakiwa huru? Baada ya kukamatwa na kuwekwa ndani hayo yote yakaisha.

Amani inatafutwa kwa gharama ikiwa ni pamoja na kuwaweka ndani watu kama hao japo ni vigumu kuthibitisha kwa ushahidi wa kimahakama. Narudia ushahidi wa kimahakama japo ushahidi wa kimazingira uko wazi
 
Kwani serikali inachotaka kwa hawa masheikh ninkitu gani? Kama inataka wafungwe kwa nn isiendeshe kesi ijulikane moja? Lawama nyingine serikali inazitaka yenyewe. Siyo haki kuwashikilia tu bila mwisho. Huu ni uonevu uliopitiliza hata kama waliua
 
Haikuwa na haja kusema au kuomba Dua hii,ikiwa kweli wewe ni Muislam kweli

TAWALA/UONGOZI
Hauombewi laana,Bali wanaombewa Mafanikio na huruma ya kweli juu ya wale wanao waongoza

Sheria yetu ya Dini(Uislam)
Haturuhusiwi kumtukana Kiongozi
Haturuhusiwi kumlaani
Haturuhusiwi kumuonyesha kidole kwa Ubaya

Chief
Turudi katika Dini yetu tena,na tuache mihemko
Mola awahukumie hapa hapa duniani hawa madhalimu wa CCM, Aamin
 
Haikuwa na haja kusema au kuomba Dua hii,ikiwa kweli wewe ni Muislam kweli

TAWALA/UONGOZI
Hauombewi laana,Bali wanaombewa Mafanikio na huruma ya kweli juu ya wale wanao waongoza

Sheria yetu ya Dini(Uislam)
Haturuhusiwi kumtukana Kiongozi
Haturuhusiwi kumlaani
Haturuhusiwi kumuonyesha kidole kwa Ubaya

Chief
Turudi katika Dini yetu tena,na tuache mihemko

Shukrani sana ila hawa si viongozi wetu ni wavamizi wetu na wauwaji

Back
Top Bottom