Serikali yashindwa kuwalipa 'Intern Doctors' Muhimbili; waamua kugoma

Dec 5, 2011
78
93
Serikali imeshindwa Kwa miezi miwili kuwalipa intern doctors MNH Hali iliyosababisha wao kuamua kugoma rasmi kuanzia Leo hadi watakapopewa hela yao.
Hii imetokana na wengine kushindwa kupata nauli ya kufika kazini au hela ya kujinunulia chakula. Inasemekana Hali hii ya kutopewa hela zao ni Kwa intern drs wote Tz.

Source: eye witness.
 
Haya sasa kazi hiyo si tuseme ukweli tu kuwa tumeishiwa?kumbuka mficha maradhi~~~
 
mi mpaka leo nawashangaa kwa nn hali ya mnh ni mbaya kwa utendaji wa kazi nyie mnafukuzana tu na damu! Mnh no diagnostic facilities,kuna siku theatre hakuna nguo,no drugs lakini mko kimya. Kumbukeni waliopandisha mishahara ya health workers ni inten. Nyie miezi miwili hamjalipwa hela mnaendelea kuivumilia hii serikali ya matapeli? You are very important people in management of patients at mnh,lakini inapofika kwenye maslahi yenu inabidi muwe imara.
 
Sijiui idadi kamili ya vifo vitakavyotokana na mgomo huo watatueleza? Waandishi wahabari, naomba iingizeni kama habari ya uchunguzi mkafukunyue vingi, msiwe wa kuripoti tu.
 
Jana nilikuwa maeneo ya muhimbili mida ya saa 1 hivi kulikuwa na msafara wa kikwete ukielekea muhimbili labda alienda kuchonga nao.

Ndiyo mana wataalam wengi na wasomi wanaamua kujiingiza kwenye siasa.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
mambo yamewiva.wabunge wanajipandishia posho huku madaktari wakikosa hata kile kidogo wanachostahili.
 
Patachimbika idara zote za upasuaji matumbo yataoza na wajawazito watajuta. Inatisha sana.
 
MADAKTARI 229 walioko katika mafunzo kwa njia ya vitendo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, wamegoma wakishinikiza kulipwa jumla ya Sh176 milioni, zikiwa ni posho zao za kijikimu.Mgomo huo ulianza jana mchana na madaktari hao wamesema hautakwisha hadi hapo watakapolipwa fedha zao.

Madaktari hao ni wa kada za tiba ya vinywa, maabara, dawa na wafamasia ambao wametishia mgomo huo utaenea hadi katika Hospitali za Mnazi Mmoja, Zanzibar, Bombo mkoani Tanga, Temeke, Amana na Mount Meru, jijini Arusha ambako wenzao nao hawajalipwa kwa miezi miwili.

Wakizungumza mbele ya Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa. aliyekwenda Muhimbili kuwasikiliza madai yao, madakatari hao walisema maisha yao yamekuwa magumu kwa sababu ya kukosa fedha za kujikimu.
Mmoja wa wataalamu hao, Dk Frank Kagoro, alisema tatizo lililopo ni kukosekana kwa uwajibikaji kwa upande wa Serikali.

“Mnachukulia mambo kirahisi sana tupo katika mafunzo lakini tutawezaje kufanya kazi bila fedha. Tunajua tuna wagonjwa na wanaumia kwa sababu ya hatua hii, hivi nani hapa asiyejua kuwa muda huu alitakiwa kuwa wodini akiwapitia wagonjwa, hivi kweli mnatupa kipaumbele," alihoji Dk Kagoro.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa madaktari hao, Dk Mally Deogratius, alisema madai yao ni zaidi ya Sh176 milioni, zikiwa ni posho za kati ya Novemba na Desemba mwaka jana, kipindi ambacho hawakulipwa.
Hata hivyo, Dk Mtasiwa aliwahakikishia kuwa malipo yao yatafanyika leo na kwamba yamechelewa kutokana na taratibu za Serikali katika malipo. Are You Sure?

Mgogomo wa madaktari hao, unakuja wakati wanafunzi wa udaktari waliokufuzwa katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi cha Sayansi za Tiba cha Muhimbili, wakiwa wameomba radhi, kufuatia vurugu walizofanya mwezi uliopita.

Wanafunzi hao walifanya hivyo jana ambapo walisema wametafakari na kujiridhisha kuwa walifanya makosa yaliyosababisha kukosekana kwa amani na utulivu katika chuo hicho.Wanafunzi hao walifanya fujo Desemba 8 na 10 mwaka jana wakishinikiza kusikilizwa kwa madai yao.
 
Kuna mtu alisema hapa kuwa sasa hivi migomo ndiyo solution ya mwisho ya watumishi wa nchi hii!...
Kwanini waajiri wasubiri ifikie hatua hii?....ni dharau za kazi za watu!
 
Hivi inawezekana kwa Serikali kujitangaza kuwa imefilisika?
 
Eti bila aibu anawaambia kuwa ni taratibu za kiserikali kuhusu malipo?! miezi miwili, watatu umeingia?! Mi nadhani kuna wakati ambapo juhudi zetu za kujitetea panapotokea madhaifu zinaweza kutufanya tuonekane wajinga zaidi :smash:!!
Wanafikiri hao madaktari wanaishije sasa? Ndio vishawishi vya kuanza kuomba rushwa kwa wagonjwa vinapotokea!! hapo unakuta mtoto anadai ada na unifomu! mwenye nyumba nae kila asubuhi yuko kwako! si anaona kila siku Dr. anaenda kazini mapemaa na kurudi usiku na siku nyingine analala huko kabisa eti yuko zamu?! na ni lazima kula pia, tena bei za vitu zimepanda vile vile!!
Hapa,sijaribu kuhalalisha rushwa maana kuna wanaoomba na wanavyo tele, ila naangalia mtu anavyoweza kujaribiwa kulingana na uwezo wake.
Na mbona walipoidhinisha malipo mapya ya posho kwa wabunge walianza wakati huo huo?! au ndo wanatufikishia ujumbe kuwa taratibu za kiserikali zinachagua maeneo ya kufuatwa!
 
Serikali imeshindwa Kwa miezi miwili kuwalipa intern doctors MNH Hali iliyosababisha wao kuamua kugoma rasmi kuanzia Leo hadi watakapopewa hela yao.
Hii imetokana na wengine kushindwa kupata nauli ya kufika kazini au hela ya kujinunulia chakula. Inasemekana Hali hii ya kutopewa hela zao ni Kwa intern drs wote Tz.

Source: eye witness.


Hii serikali si ndio ilikuwa na hela za ziada hadi za kuongezea posho wabunge? Inashindwaje kuwalipa hao madokta?
 
Naifananisha Serikari ya JK na sharubaroo.pamba kari watu nje wamuone matawi ya juu, nyumbani analala njaa.Miaka 50 ya uhuru matumizi ni Billions of money, Watumisha wa uma wanapiga miayo njaa kari.Tutafika kweli?Kazi kwelikweli!!
 
Back
Top Bottom